Kwanini Rais wa Tanzania amefanya upendeleo wa makusudi kwa mikoa ya Pwani na Tanga kuwa na Mawaziri wengi kuliko mikoa mingine?

Kwanini Rais wa Tanzania amefanya upendeleo wa makusudi kwa mikoa ya Pwani na Tanga kuwa na Mawaziri wengi kuliko mikoa mingine?

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Shalom,

Tafadhari nakaribisha mjadala wa wazi katika hili. Rais amethubutu vipi kuvunja kwa makusudi utaratibu wa uwiano wa uwakilishi kimimkoa na kikanda katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri, kuna udhaifu gani dhidi ushauri katika misingi ya mila na desturi.

Kuna nini nyuma upendeleo huo wa hio mikoa miwili na hoja za msingi ni nini?

Chamata karibuni kwa mnyukano.

Wadiz
 
Kwa sasa nchi inavyokwenda, mawaziri ninaowakumbuka ni wawili watatu nadhani, Mchengerwa, Mbarawa na Mwigulu!

Tungepata japo ka list ka mawaziri na asili zao, ingesaidia kuwa na mjadala mpana zaidi!
 
Kusini ukiachana na Pm na yule Mzee ambae hajulikani Yuko Wizara gani sijui kama Kuna Waziri mwingine,
Mbeya? Iringa? Nyanda za juu Kusini Wanaotamba kidogo ni Ruvuma, Wana Kapinga yule Dada naibu wake Doto kule nishati,Ndubaro na Mama la mama a.k.a kisiki cha mpingo Jenista Muhagama na wakizidi kujichimbia kwenye Chama Cha mbogamboga Karibu Mkuu na Katibu Mkuu Uvccm.
 
Akili za wana CCM wote ni zile zile so hata akichagua kwa uwiano wa ki kanda ama mikoa bado tutapata idadi ile ile ya majizi ya mali ya umma
 
Kusini ukiachana na Pm na yule Mzee ambae hajulikani Yuko Wizara gani sijui kama Kuna Waziri mwingine
Nape Nnauye ni wa kusini na Jenista Mhagama ni wa kusini
 
Tuacheni utoto, raisi ana taarifa nyingi kuliko raia yeyote...

Kuna mikoa imejaa wachapa kazi, anajua...

Kuna mikoa wamejaa wezi na matapeli, anajua...

Raisi habeti, obvious atachukua kule kwenye sifa za uchapa kazi tu ili wamletee matokeo anayotaka...

Na hii haimaanishi upendeleo, no anajaribu kusajili team bora ya ushindi.
 
Nape Nnauye ni wa kusini na Jenista Mhagama ni wa kusini
Ok!Nape ni Mtama Lindi nilimsahau.Kikanda Nape yupo Kusini maana Lindi na Mtwara ni Pwani ya Kusini.Jenister nimemtaja Hapo huyo Kikanda hayupo Kusini yupo Nyanda za Juu Kusini maana anatokea Ruvuma Mbunge wa Songea vijijini.
 
Back
Top Bottom