Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Sasa mbona unajikanganya mwenyewe? Hizi statement hazipo sahihi hata kidogo.
Wewe ndo hujaelewa. Iraq Inapakana na sryria akini Iraq haipakani na Russia.

Kuna border ya Syria/Turkey kwa upande wa Russia.

Mara zote Russia hulinda nchi zinazopakana na Yeye ili. Marekani asiweke kambi maana huwezi kuacha adui akuchungulie dirishani.
Iraq ingepakana na Russia Putin angemlinda sAdam. Wala hawana habari kama unaua raia Wako. Kwa sumu hilo haliwahusu. Ilimradi utalinda maslahi yako.

Western ndo kwa jicho la. Mbali ndio huangaliaga hizo mambo.

View attachment 1575837

Screenshot_20200921-100730.jpg
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania (wale tu mnaofuatilia siasa za kimataifa kwa muda mrefu kama mimi);

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila kwa sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria ilhali nchi hizi mbili zinapakana?

Tafadhali tazama ramani ndogo ya nchi za mashariki ya kati hapo chini;

View attachment 1575807

Ndio tuseme kuna unafiki unaendelea ndani ya baraza la usalama la umoja wa mataifa (UNSC)?

Russia na China walisusia kupiga kura turufu (VETO) jambo lilipelekea wanachama wengine wa baraza la usalama la umoja huo (U.S.A, France and the United Kingdom) kuridhia kwa pamoja uvamizi dhini wa Saddam Hussein wa Iraq. Kwanini Russia hao hao hawakususia kupiga kura ya VETO dhidi ya Syria ya Assad?

NB: Ninaomba mtu asije akaongelea ama kuuliza kwanini Russia haikumtetea Muammar Gadaffi kwa maana Iraq na Libya ni mbali sana ukilinganisha Iraq na Syria.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Taam sana hii ya leo. Nipo siti ya mbele.
 
Kuna border ya Syria/Turkey kwa upande wa Russia.
Hapana boss. Ninakataa katakata.

Russia has boundaries with 14 countries: Norway, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland (via the Kaliningrad Oblast), Belarus, Ukraine, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, Mongolia, the People's Republic of China and North Korea.
 
Mbona Obama aliudanganya ulimwengu kuhusu Assad kumiliki WMD lakini Russia akaweka kifua mbele kumkinga huyu Rais wa Syria?...
Hivi unaelewa mtu anaposema hoja ni UN Security Council Resolution?! Btw, nimesema hoja ni George Bush kuidanganya au George Bush KUFANIKIWA kuidanganya UN hadi ikapitishwa resolution kwamba Iraq MUST be disarmed?

Kuna resolution ya aina hiyo ambayo ilipita dhidi ya Syria?!
 
US walipotaka kuivamia Iraq kwa kigezo cha kusaka WMD, Russia akakataa katakata...
ACHA UONGO! Unapinga nini walishaunga mkono Security Council passed Resolution 1441 ambayo ilisema Iraq MUST be disarmed?! But all in all, issue sio kupinga kwa maneno bali kwa vitendo kitendo ambacho hawakufanya kwa sababu na wenyewe waliunga mkono UN hapo kabla!
 
Baada ya lile shambulizi, Russia walikuwa na uhakika kuwa Assad anazo silaha za sumu na wakaongoza juhudi za UN za kuwapokonya kwa njia za kistaarabu...
Unaweza kutaja ni UN Resolution namba ngapi ambayo iliitaka Syria MUST be disarmed?! Iraq ilikuwa 1441, ya Syria?
 
Wakuu vile vile tusisahau mabadiliko ya kiungozi yaliyotokea Russia,kwani naamini yanamchango mkubwa sana kwa yanayoendelea kwenye siasa za kimataifa.Ni kweli Saddam Hussein alikuwa ni mshirika mkubwa wa Marekani na CIA na wao ndio waliomuingiza madarakani.CIA walimtumia almarhum Saddam kuwavuruga IRAN na kufanya unyama mkubwa kwa raia wa IRAN.Sababu pekee ya IRAN kutoshindwa vita hiyo ni msaada alioupata kutoka URUSI.

Hali ilivyombadilikia Saddam ilikuwa ni fursa ya Iran na Russia kuicontrol Iraq.Tusisahau kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wairaq ni mashia wenye mafungamano ya asili na IRAN,na ndio maana wachambuzi wa mambo ya kimataifa wanasema kwenye uvamizi wa Iraq taifa la Marekani lilijikaanga kwa mafuta yake yenyewe na kuwapa ushindi mnono maAyatollah wa Iran.

Kwa upande wa Syria ni hadithi nyingine kabisa kwani kuna makubaliano ya kiulinzi baina ya nchi hizi mbili na vilevile huko nchini Russia kuna mwamba kweli kweli kwenye kiti cha uongozi aitwaye Vladmir Putin, ambae kawekeza juhudi kubwa kwenye kuliboresha jeshi la Urusi.Mbabe huyu aliyabadili matokeo ya vita ya Syria ikiwa Marekani na washirika wake wamebakiza mji mkuu wa Damascus tu kuicontrol Syria nzima.kilichotokea baadae kimebakia kuwa historia.

Putin aliamrisha jeshi lake kuicontrol anga yote ya Syria kwa kupeleka mitambo ya S400 na hivyo kuwanyima aerial support wapiganaji wa ardhini wa washirika wa USA.Pale makomandoo wachache wa russia special forces walipoanza kuwaongoza wanajeshi wa Assad ardhini ndipo ile kasi ya kurudi nyuma kwa majeshi washirika ilipoanza.Kiufupi Syria imebaki kuwa ilivyo kwa sababu Vladmir Putin aliamua iwe hivyo.
 
Russia ya 2002 sio hii ya 2020 kwa sasa wana mabavu kiasi hata cha kuitandika ulaya yote hata wakiamua leo saa saba mchana.
 
Hapana boss. Ninakataa katakata.

Russia has boundaries with 14 countries: Norway, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland (via the Kaliningrad Oblast), Belarus, Ukraine, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, Mongolia, the People's Republic of China and North Korea...
Mzee unakataa hata hiyo habari nimekuwekea ya border ya turkey/Syria.
 
Dogo;
Siku zote nchi kubwa huangalia maslahi mapana ya nchi zao.

Unapotamka vita, hii hugharinu uhai na rasilimali nyingi sana kama silaha nzito nzito na fedha kwa ajili ya luweza kuhusumia wapiganaji au walinzi wa nchi flani isivamiwe.

Hivyo kabla nchi haijaingilia katika masuala ya kivita, huwa wanaangalia kiwa wana maslahi gani na nchi hiyo inayohitajo msaada wa kiulinzi au vita.

Inasemekana kuwa Assad ni mshirika muhimu sana wa Urusi kibiashara hivyo sio tu wanamlinda bali wanalinda maslahi yao ya kibiashara ambapo mwaka 2019 pekee iliwekeza $19B.

Saddam alikuwa mbabe na alikuwa na washirika wachache na wasio na nguvu

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania (wale tu mnaofuatilia siasa za kimataifa kwa muda mrefu kama mimi);

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila kwa sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria ilhali nchi hizi mbili zinapakana?

Tafadhali tazama ramani ndogo ya nchi za mashariki ya kati hapo chini;

View attachment 1575807

Ndio tuseme kuna unafiki unaendelea ndani ya baraza la usalama la umoja wa mataifa (UNSC)?

Russia na China walisusia kupiga kura turufu (VETO) jambo lilipelekea wanachama wengine wa baraza la usalama la umoja huo (U.S.A, France and the United Kingdom) kuridhia kwa pamoja uvamizi dhini wa Saddam Hussein wa Iraq. Kwanini Russia hao hao hawakususia kupiga kura ya VETO dhidi ya Syria ya Assad?

NB: Ninaomba mtu asije akaongelea ama kuuliza kwanini Russia haikumtetea Muammar Gadaffi kwa maana Iraq na Libya ni mbali sana ukilinganisha Iraq na Syria.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hakuna taifa Sadam hakuvurugana nalo. Alikuwa anaongea sana yule mzee. Asadi anatengeneza ujamaa na urusi kimaslahi. Hawawezi mtoa pale
 
Back
Top Bottom