Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

How come waliruhusu wakati na wenyewe walipitisha kwa kura ya NDIYO UN Security Council Resolution #1441 ambayo ilitaka Iraq MUST be disarmed?!
Russia walipitisha azimio la kuwapokonya Iraq WMDs lakini hawakuwahi kupitisha azimio la kuwapokonya kwa kutumia nguvu...
========
France and Russia made clear on March 5 2003 that they were ready to use their veto power to block passage of a new Security Council resolution authorizing force against Iraq, but Secretary of State Colin L. Powell said the United States would go to war without United Nations backing if necessary.
 
Huenda ni kwasabab iraq alikua adui wa iran ambaye ni mshirika wa russia
Sadam aliwah kutumia silaha za sumu dhidi ya iran ambaye ni mshirika wa russia kindakindaki
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania (wale tu mnaofuatilia siasa za kimataifa kwa muda mrefu kama mimi);

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila kwa sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria ilhali nchi hizi mbili zinapakana?

Tafadhali tazama ramani ndogo ya nchi za mashariki ya kati hapo chini;

View attachment 1575807

Ndio tuseme kuna unafiki unaendelea ndani ya baraza la usalama la umoja wa mataifa (UNSC)?

Russia na China walisusia kupiga kura turufu (VETO) jambo lilipelekea wanachama wengine wa baraza la usalama la umoja huo (U.S.A, France and the United Kingdom) kuridhia kwa pamoja uvamizi dhini wa Saddam Hussein wa Iraq. Kwanini Russia hao hao hawakususia kupiga kura ya VETO dhidi ya Syria ya Assad?

NB: Ninaomba mtu asije akaongelea ama kuuliza kwanini Russia haikumtetea Muammar Gadaffi kwa maana Iraq na Libya ni mbali sana ukilinganisha Iraq na Syria.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Halaf pia iraq hakua mshirika wa kuaminiwa kumbuka before gulf war sadam alkua mshirika wa USA na alitumiwa hadi kudhoofisha ant usa kama iran
 
Magufuli haitaji kupiga kampeni Mkuu hata akikaa ofisini lazima achaguliwe kwa kishindo Kazi zake zinambeba.
 
Ajenda ya upinzani ni kupinga maendeleo na kumtukana Rais Magufuli.
 
Saddam alikuwa jeuri sana ndo maana wakati anaenda kupigwa WARUSI wakawa wanamtazama tu pasipo kumpa msaada wowote ule.

Hata wanajeshi wake walikuwa tayari washamchoka na ndo maana akatengeneza kikosi kingine kilichoitwa( Republican guard) baada ya kuona kuna uwezekano wa kupinduliwa na jeshi.
Inasemekana kilikuwa kikosi kikubwa sana chenye askari wasiopungua laki 3 na walikuwa wanatumia vifaa vya kikeshi kama vifaru, ndege vita na maroketi.Sehemu kubwa ya askari wa hicho kikosi walikuwa ni watu kutoka kwenye kabila lake na hata malipo yalikuwa makubwa sana tofauti na jeshi la Iraq.
Baada ya uvamizi wa Muungano ulioongozwa na Marekani, makamanda wengi wa jeshi la Iraq walikubali kusign peace deal na Marekani ili kutopiganisha vikosi vyao na majeshi ya Muungano.ila tofauti na Republican guard, wao walitoa upinzani mkubwa sana kwa majeshi ya Muungano na wakakataa kusign deal lolote lile na majeshi ya Muungano.

WARUSI ni watu wenye urafiki wa kweli na mshirika wao mfano mzuri na pale SYRIA tulijua mpaka kufika 2016 basi Assad atakuwa kashatolewa kwenye kile kiti.ila kwa msaada wa WARUSI mpaka leo bado yupo labda atake mwenyewe kuacha ile nafasi.
Venezuela Trump na washilika wake walitaka kutumia nguvu kumtoa Maduro ila ikashindikana baada ya WARUSI kupeleka askari venezuela na ndege zenye uwezo wa kubeba vichwa vya Nuclear.
 
Kwa mawazo yangu Russia ya mwaka 2003,2002, mpaka 2011 ilikuwa dhaifu kiuchumi na kijeshi kushiriki Vita ya nje ya taifa lao. Hebu fikiri miaka ya 98-2000 Russia haikuwa na ndege Vita zilizo tayari kwa Vita ya anga japo kwa asilimia 30. Wangewezaje kupambana? Alipoingia Putin ndo akafanya modernization nzito kuzifanya tu 160,tu 95 nk kua oparational. Lakini wakiwa weak kabisa kuwasaidia wengine.
Huko Iraq wangeendaje?
 
Hapana boss. Ninakataa katakata.

Russia has boundaries with 14 countries: Norway, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland (via the Kaliningrad Oblast), Belarus, Ukraine, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, Mongolia, the People's Republic of China and North Korea...
Na US umeisahau
 
Baada ya shambulizi la chemikali huko Syria, Russia alikuwa na uhakika kuwa ni kweli Assad alikuwa na WMD, lakini hakumuacha afe peke yake. Kwanini?...
Saddamu alikuwa kibaraka wa marekani,,lakini tatizo ni kuwa iraq ilikuwa inakuja juu na kuwa tishio kwa israel kipindi hicho kuanzia miaka ya 90,iraq ilikuwa na uhusiano mzuri na marekani,lakini ilikuwa haijawa na amani na israel,kwani bado ikiwasaidia wapalestine,
Ilitakiwa ipatikane njia ya kuipunguza speed iraq,kwani ilikuwa ikija vizuri,kiuchumi na kijeshi hivyo kuwa tishio kwa israel,.
Saddam alikuwa na mgogoro na kuwait,,waarabu wenzie walimpiganisha na iran,vita ya miaka 8 na hawakuwa tayari kumu compensate,,saddam akataka kuvamia kuwait,,marekani wakamtega,,kisiri siri wakamoa ok,saddamu avamie kuwait mwaka 1991,first gulf war,
Alipovamia tu,saddamu kashangaa marekani wanamgeuka,
Wakamtwanga,japo hawakutaka kumpindua,,wakamwekea vikwazo ili kuua kabisa speed ya iraq kupiga hatua,,
Vikwazo vikadumu miaka 12,,lakini sardamu akaendelea kutawala,
Ndiposa 2003,likaja swala la WMD,
Hivyo tokea mwanzo,saddamu hakuwa swahiba mkubwa wa Russia.
 
Alaska imefanya nini?
Hapo nimejichsnganya kuandika Alaska but Russia na us Wana mmipaka ya majini katika Bering sea, Arctic ña pasifik. Hii ni kutokana na mkataba uliosainiwa na Soviet Russia na US katika 1990 hiyo ni kabla ya total colapse ya Soviet katika 1991 . Hata hivyo mipaka hiyo ipo mpaka leo. Lakini pia Russia imepakana na nchi 16 na si 14
 
Iraq ilisaidiwa na urusi kubusu silaha kwenye vita ya kwqnza na marekani.

Iraq hakutaka kuwa muwazi na kuomba msaada mapema kwa mrusi ivyo ikamfanya mrusi awe neutral.
Pia iraq aliamin asingewezwa na mmaerekani kutokana na kuboresha zana zake.
Mrusi hakubali kuingia kwenye jambo ambalo .umemshirikisha katikati na si mwanzo kwa kua reputation yake ni muhim kwa wafuasi wake.
 
Back
Top Bottom