Kwanini Rwanda wametuzidi katika hili?

Utakuwa hujielewi wewe mtu amekupa taarifa toka ITV wala haihusiani na Mbowe wewe unafuka povu, kama ushauri wa Mbowe ulikuwa mbaya mbona Kikwete kaomba suluhu kupitia kwa Museven, elimika kidogo.
 
Ndugu yangu mbona kama huna macho? Uchumi wa rwanda unakua haraka kutokana na kupora madini ya congo. Ndio maana anashikwa na wazimu akifikiria kama congo itapata uwezo kulitosa jeshi lake la m23 nje ya mipaka ya nchi yao. Jisomee habari zaidi kuhusu kagame ili kumuelewa yeye na utawala wake.
 
Daaa kwa comment hizi tanzania tuna miaka mia ijayo kumfikia kagame
Ni kweli mkuu mtoa hoja kaleta data tena kutoka taarifa ya habari ITV badala ya kujadili hoja wanaanza kumuita ni mnyarwanda huu ni ujuha uliopitiliza kiasi hata kama tuna conflict na Kagame lakini facts haziwezi kufichika.
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .
Kwa hiyo Tanzania tunasubiri vita vya Congo viishe ili tuwazidi Rwanda kiuchumi....akili za matope hizi.
 

maendeleo yaliyopo tanzania siyo ya kubeza kwa binadamu yeyote mwenye akili timamu, idadi ya barabara moja tu mfano barabara kuu ya kutoka arusha -dar rwanda yote mpaka vichochoro vya panya vitakuwa na lami, kitu ambacho rwanda hata bara bara za misingi kabisa hazina lami.
 

maisha ya kusikitisha unalinganisha na nchi gani? kama usa sawa, lakini hata kenya wanaojigamba uchumi wao upo juu hata raia wao wenyewe wanashangaa kwani maisha yao ni magumu kuliko ya mwanachi wa kawaida wa tanzania.
 

tusingeijua rwanda tungeweza kuaminishwa na upuuzi wako.
 
Wao wanaiba wanaendelea, wanatumia akili kubwa, sisi na ubongo wetu wa utapiamlo tuna kila kitu lakini hatuendeleai. Tunategemea biashara ya sembe ndio itutoe, mateja wakifa wote na sisi ndio mwisho wetu.

utakuwa mgonjwa wewe, siyo bure.......unasifia ujambazi na vifo vya binadamu wenzio kisa maendeleo?
 
utakuwa mgonjwa wewe, siyo bure.......unasifia ujambazi na vifo vya binadamu wenzio kisa maendeleo?
Wewe ndio mgonjwa, nadhani utakuwa teja, ushahidi ea Kagame kuiba uko wapi, acheni mihemko na chuki zisizo na sababu. Wenzenu wataendelea ninyi mmekalia kuwazushia tu.
 

Kwa hiyo kwa kauli yako na upeo wako wa kuelewa Tanzania uchumi unashindwa kukua kwa kasi kwa sababu ya ukubwa wa nchi na bei ya bidhaa inashindwa kushuka na kupanda kila kukicha kwa sababu ya ukumbwa wa nchi, hayo mawazo yenu ya kipuuzi ndio yanaiangusha nchi hii hizo nchi ambazo Kikwete huwa anaenda kutembelea na mawaziri wake kujifunza baadhi ya mambo mazuri wayafanyayo ya maendeleo ni kubwa kuliko Tanzania? inatakiwa ujue ili tuendelee tunahitaji vitu vinne 1. WATU 2. ARDHI 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA, sisi nchi hii tuna watu na Ardhi lakini kwa upande wa Siasa safi na Uongozi Bora ndio vinatufanya tuwe marofa wa kupindukia hadi sasa
 
kagame kuwa mkali au kuwa dikteta??hizo mali za wakongo wanazochukua kila siku ndo zinawapa kiburi cha uchumi
 
Wewe ndio mgonjwa, nadhani utakuwa teja, ushahidi ea Kagame kuiba uko wapi, acheni mihemko na chuki zisizo na sababu. Wenzenu wataendelea ninyi mmekalia kuwazushia tu.

tunawaambia ukweli na siyo uzushi na wakikataa sasa ni kipondo tu!
 
Daaa kwa comment hizi tanzania tuna miaka mia ijayo kumfikia kagame

Tanzania haipo kushindana na Rwanda. Tuna vipaumbele vyetu, mojawapo ikiwa ni kumshughulikia huyo role model wako. Tukishapata stability upande wa magharibi tutafungua milango mingi ya kiuchumi.
 
hii habari ni ya uongo!
mtu atupie link kama kuna ukweli wowote anaosema!



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…