Kwanini Rwanda wametuzidi katika hili?

Kwanini Rwanda wametuzidi katika hili?

Utakuwa Mnyarwanda haramu pekee uliyebakia nchini, kila wakati kusifia tu KAGAME, huna kazi ya kufanya? kuna hata Idara ya uhamiaji kuwamulika mamluki wa Rwanda mlioko humu JF, hata jana kibaraka wa KAGAME hapa nchini amesikika bungeni akitaka Tanzania iunde chombo cha kusuluhisha mgogoro tena kwa akili yake ya kidato cha nne anasema chombo hicho kianzie kazi yake hapa nchini. Mada hizi zinazidi kunifanya ni connect dots.
Utakuwa hujielewi wewe mtu amekupa taarifa toka ITV wala haihusiani na Mbowe wewe unafuka povu, kama ushauri wa Mbowe ulikuwa mbaya mbona Kikwete kaomba suluhu kupitia kwa Museven, elimika kidogo.
 
Kupitia taarifa ya Habari ITV saa 2, taarifa imesema katika utafiti uliofanyika na benki ya dunia katika nchi 100 Rwanda imekuwa nchi ya 7 kati ya 100 ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kila mwaka na mfumuko wa bei umeshuka kwa kasi sana,
Najua wengi tunaichukia Rwanda na Kagame na hasa kutokana na mtafaruku na Raisi wetu lakini wenzetu wanafanya vizuri katika kupanga mipango yao na utawala wao unafuata sheria na hakuna ufujaji wa fedha za umma kama huku kwetu na hili linafanyika kutokana na Kagame kuwa mkali, tunatakiwa tujifunze mazuri kutoka huko ili nasi tuendelee.
Ndugu yangu mbona kama huna macho? Uchumi wa rwanda unakua haraka kutokana na kupora madini ya congo. Ndio maana anashikwa na wazimu akifikiria kama congo itapata uwezo kulitosa jeshi lake la m23 nje ya mipaka ya nchi yao. Jisomee habari zaidi kuhusu kagame ili kumuelewa yeye na utawala wake.
 
Daaa kwa comment hizi tanzania tuna miaka mia ijayo kumfikia kagame
Ni kweli mkuu mtoa hoja kaleta data tena kutoka taarifa ya habari ITV badala ya kujadili hoja wanaanza kumuita ni mnyarwanda huu ni ujuha uliopitiliza kiasi hata kama tuna conflict na Kagame lakini facts haziwezi kufichika.
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .
Kwa hiyo Tanzania tunasubiri vita vya Congo viishe ili tuwazidi Rwanda kiuchumi....akili za matope hizi.
 
Muongo wewe, hakuna ubishi kuwa Kagame amedhibiti ufisadi Rwanda na matumizi mabaya ya rasilimali za umma, fuatilia hata magari wanayotumia viongozi wa Rwanda,
Kama uchumi wa Rwanda unakua kutokana na rasilimali zinazibwa DRC, je Tz yenye rasilimali nyingi na haina vita mbona imeshindwa kupata maendeleo endelevu?
Ukweli ni kwamba wenzetu wako serious na maendeleo ya taifa lao, sisi Tumeacha mafisadi wakituibia na kujificha kwenye kivuli cha chama dola.

maendeleo yaliyopo tanzania siyo ya kubeza kwa binadamu yeyote mwenye akili timamu, idadi ya barabara moja tu mfano barabara kuu ya kutoka arusha -dar rwanda yote mpaka vichochoro vya panya vitakuwa na lami, kitu ambacho rwanda hata bara bara za misingi kabisa hazina lami.
 
Labda sisi tusiweke nia ya kwenda kupora rasilimali za nchi nyingine kama DRC, lakini mbona kila mkoa Tanzania una rasilimali nyingi na hazinufaishi Tanzania wala mkoa husika

Mfano, Shinyanga licha ya kuwa wanalima mpunga na pamba amapo pamba ni zao la biashara na mchele zao la chakula na biashara, pia kuna madini ya dhahabu na almasi

Shinyanga ina migodi 3 na tupo mbioni kuweka wa 4, maisha ya watanzania kule ni ya kusikitisha na wengi ni maskini na mafukara

Je? Kwa muktadha huo wa kwako sisi tunaibiwa na nani na kwa nini anatuibia na kwa nini hatuchukui hatua ili badala ya kwenda kuiba nchi jirani, tujinufaishe kwa urithi wetu tuliopewa na Muumba?

maisha ya kusikitisha unalinganisha na nchi gani? kama usa sawa, lakini hata kenya wanaojigamba uchumi wao upo juu hata raia wao wenyewe wanashangaa kwani maisha yao ni magumu kuliko ya mwanachi wa kawaida wa tanzania.
 
na zako zinazoporwa na wazungu kule mwanza ..tanzanite kupitia mirahaba uzioni...embu kubali ukweli ukusaidie hata kama sio wewe basi wajukuu zako..leo mtoto wa rwanda shule ya msingi ajui upe ajui ada anasomea computer ...wako umejiandaaje kujua hili???

tusingeijua rwanda tungeweza kuaminishwa na upuuzi wako.
 
Wao wanaiba wanaendelea, wanatumia akili kubwa, sisi na ubongo wetu wa utapiamlo tuna kila kitu lakini hatuendeleai. Tunategemea biashara ya sembe ndio itutoe, mateja wakifa wote na sisi ndio mwisho wetu.

utakuwa mgonjwa wewe, siyo bure.......unasifia ujambazi na vifo vya binadamu wenzio kisa maendeleo?
 
utakuwa mgonjwa wewe, siyo bure.......unasifia ujambazi na vifo vya binadamu wenzio kisa maendeleo?
Wewe ndio mgonjwa, nadhani utakuwa teja, ushahidi ea Kagame kuiba uko wapi, acheni mihemko na chuki zisizo na sababu. Wenzenu wataendelea ninyi mmekalia kuwazushia tu.
 
Usilete matusi yako hapa. wewe pia ni mnyarwanda tuna wanyarwanda wengi hapo Mbeya toka miaka mingi. wote wanajulikana kwa majina. Kuna kitu gani cha kujifunza Rwanda? kwa nini unailinganisha TZ na Rwanda? hivi unashindwa kuelewa kuwa mkoa wa mbeya wenyewe ni mkublwa kuliko Rwanda? wewe unaweza kuilinganisha Marekani na TZ?

Kwa hiyo kwa kauli yako na upeo wako wa kuelewa Tanzania uchumi unashindwa kukua kwa kasi kwa sababu ya ukubwa wa nchi na bei ya bidhaa inashindwa kushuka na kupanda kila kukicha kwa sababu ya ukumbwa wa nchi, hayo mawazo yenu ya kipuuzi ndio yanaiangusha nchi hii hizo nchi ambazo Kikwete huwa anaenda kutembelea na mawaziri wake kujifunza baadhi ya mambo mazuri wayafanyayo ya maendeleo ni kubwa kuliko Tanzania? inatakiwa ujue ili tuendelee tunahitaji vitu vinne 1. WATU 2. ARDHI 3. SIASA SAFI 4. UONGOZI BORA, sisi nchi hii tuna watu na Ardhi lakini kwa upande wa Siasa safi na Uongozi Bora ndio vinatufanya tuwe marofa wa kupindukia hadi sasa
 
kagame kuwa mkali au kuwa dikteta??hizo mali za wakongo wanazochukua kila siku ndo zinawapa kiburi cha uchumi
 
Wewe ndio mgonjwa, nadhani utakuwa teja, ushahidi ea Kagame kuiba uko wapi, acheni mihemko na chuki zisizo na sababu. Wenzenu wataendelea ninyi mmekalia kuwazushia tu.

tunawaambia ukweli na siyo uzushi na wakikataa sasa ni kipondo tu!
 
Daaa kwa comment hizi tanzania tuna miaka mia ijayo kumfikia kagame

Tanzania haipo kushindana na Rwanda. Tuna vipaumbele vyetu, mojawapo ikiwa ni kumshughulikia huyo role model wako. Tukishapata stability upande wa magharibi tutafungua milango mingi ya kiuchumi.
 
hii habari ni ya uongo!
mtu atupie link kama kuna ukweli wowote anaosema!



Kupitia taarifa ya Habari ITV saa 2, taarifa imesema katika utafiti uliofanyika na benki ya dunia katika nchi 100 Rwanda imekuwa nchi ya 7 kati ya 100 ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kila mwaka na mfumuko wa bei umeshuka kwa kasi sana,
Najua wengi tunaichukia Rwanda na Kagame na hasa kutokana na mtafaruku na Raisi wetu lakini wenzetu wanafanya vizuri katika kupanga mipango yao na utawala wao unafuata sheria na hakuna ufujaji wa fedha za umma kama huku kwetu na hili linafanyika kutokana na Kagame kuwa mkali, tunatakiwa tujifunze mazuri kutoka huko ili nasi tuendelee.
 
Back
Top Bottom