Labda sisi tusiweke nia ya kwenda kupora rasilimali za nchi nyingine kama DRC, lakini mbona kila mkoa Tanzania una rasilimali nyingi na hazinufaishi Tanzania wala mkoa husika
Mfano, Shinyanga licha ya kuwa wanalima mpunga na pamba amapo pamba ni zao la biashara na mchele zao la chakula na biashara, pia kuna madini ya dhahabu na almasi
Shinyanga ina migodi 3 na tupo mbioni kuweka wa 4, maisha ya watanzania kule ni ya kusikitisha na wengi ni maskini na mafukara
Je? Kwa muktadha huo wa kwako sisi tunaibiwa na nani na kwa nini anatuibia na kwa nini hatuchukui hatua ili badala ya kwenda kuiba nchi jirani, tujinufaishe kwa urithi wetu tuliopewa na Muumba?