Kwanini sauti ya Diamond Live ni mbaya lakini nzuri kwenye nyimbo tofauti?

Kwanini sauti ya Diamond Live ni mbaya lakini nzuri kwenye nyimbo tofauti?

Nilichokiona ni kua Diamond alipania sana ile show.Na pia si lazima acheze na densa wake kwa 100%..Hii nayo ilichangia kumpoteza.
 
Kama li Jaguar!! Lina mafanikio na pesa lakini kuimba kwake sasa bora hata Shilole!
 
Kuna kitu kinaitwa "auto tune" yaani sauti inachezewa na computer kule studio kupata sauti nzur zaid ya sauti ya msanii mwenyew. wasanii wengi huwa wanatumia hii kitu. Na mmoja ya wasanii marufu duniani ambaye hata wenzie huko marekani wanamlalamikia ni T-PAIN. Mpaka jay-z aliwahi kumuimba huyu jamaa kwenye "death of autotune". So nahis diamond anatumia hii kitu japo sina uhakika zaidi.
 
sio diamond tu mkuu,mimi ni mpenzi wa live shows hasa za mbele,sijawahi kusikia sauti ya live show iliyofanana na iliyorekodiwa kwenye cd,hata kwa kina wizkid siku ile kwenye mtvmama sauti yake haikuwa sawa na ya kwenye CD
Labda kwa Lucky Dube na Bob Marley
 
Wabongo saluti wasanii wanaofanya live bongo ni lady jaydee & christian bella na baadhi wachache wengine wanatumia play back cd. Ikiwemo mondi , kiba na nk.
 
Kwa hela alizonazo ningekuwa naweza kumshauri ningemwambia awezeke kwenye yafuatayo:

1. Anunue vyombo vya kisasa kabisa na atafute wapigaji wazuri na waimbaji waliosimama ile mbaya.

2. Kisha aingie kwenye extensive vocal classes na aendeleze mazoezi sana ili aongeze uwezo wa kupiga live performances vizuri zaidi.

3. Kuhakikisha ana technical team nzuri sana ya muziki (waliosomea kabisa muziki sio wale wa kusikiliza tu redioni) pamoja na wataalamu wa masoko au kumtangaza. Nafikiri kwenye masoko ana watu wazuri ndio maana hata jina lake limepaa ila sasa kwenye technical ili ajihakikishie kubaki kwenye game mpaka anazeeka ndipo nafikiri angewekeza zaidi. Mfano, moja ya kazi za technical team ingekuwa ni kumpa assessment ya kila performance na kum-guide cha ku-improve; asiwekeze kuongeza wapambe tu bali awekeze kwenye technical team..

Kwa uwezo wa jamaa na kwa juhudi alizonazo angetisha sana.
 
Tanzania kama sio Afrika nzima msanii anayeongoza kwa kuongelewa vibaya ni DIAMOND PLATNUMZ,na kama wewe ni mfuatiliaji wa hizi tuzo utakumbuka kuwa mwaka jana kwenye tuzo hizi za MTV mama MTUMBUIZAJI BORA AFRICA ALIKUWA NI YEYE DIAMOND PLATNUMZ.
Yani we jamaa hutaki kabisa diamond akikosolewa ata kama kakosea kazi yako kuficha makosa
 
Jamani diomond anapendwa maana ni kama maji !!hii ngekewa uliipata wapi nami nipite huki chibu?!!
 
Yani we jamaa hutaki kabisa diamond akikosolewa ata kama kakosea kazi yako kuficha makosa
Si kweli kwamba sitaki MOND akosolewe, ila wengi hawaongei hoja ila wanaongea CHUKI, na ndio maana kwenye hilo swala la kuimba live nikawapa na mfano wa kwamba yeye ni mmoja wa waimbaji bora wa live kwa Africa na ndio maana mwaka jana alishinda tuzo ya BEST LIVE ACT,NA HII TUZO NI KWA MSANII AMBAYE ANALIMUDU JUKWAA KAMA HULIMUDU JUKWAA HUWEZI KUPATA HIYO TUZO. Sasa mtu haje kujenga hoja hapo.
 
Account yake ya bank inasoma sh ngap vilee? Je Saut ya Young thuggin je au Lil Wayne?
hao uliowataja ni rappers sio vocalist kama diamond, Diamond yuko vizuri ila ajinoe zaidi katika vocal.Siko katika team zenu mi ni Team Tamadunu Muzik hahah Nikki Mbishi Songa One....
 
Sio Diamond tu, wasanii bongo/Africa wengi wanasauti mbaya live show.
 
Kucheza na kuimba at the same time ni tofauti na kuimba ukiwa umekaa kwenye kiti kama mfalme juha
 
Back
Top Bottom