Kwanini sekta ya Bodaboda isifutwe? Ni kimbilio la waliofeli, wanajazana mochwari na wazalishaji wa wajane mtaani

Mkuu baharia 1 naona umeshiba zako umekaa miguu juu hapo smart mkononi unadhani maisha ndivyo yalipaswa kuwa kwa kila mmoja,ushauri wangu weka akiba ya maneno then tafuta kitanda upumzishe fuvu kesho nayo siku.
Sawa
 
😂😂😂😂
 
Hawa sio wasafirishaji tena, sasa hivi wamekuwa vibaka wa mchana kweupe. Kazi yao kubwa mjini ni kuvizia wadada wanaotembea kwa miguu au watu wanaoshuka kwenye magari, wanakupita kwa kasi ya ajabu na kukushandua simu au mkoba kisha wanatokomea kusikojulikana. Wamegeuza chombo cha usafiri kuwa vifaa vya ujambazi
 
Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo.
Hawa sio wasafirishaji tena, sasa hivi wamekuwa vibaka wa mchana kweupe. Kazi yao kubwa mjini ni kuvizia wadada wanaotembea kwa miguu au watu wanaoshuka kwenye magari, wanakupita kwa kasi ya ajabu na kukushandua simu au mkoba kisha wanatokomea kusikojulikana. Wamegeuza chombo cha usafiri kuwa vifaa vya ujambazi
 
Ulipaswa kushauri namna ya kuwachambua wanaotekeleza vitendo hivyo na kuwadhibiti ila sio kuwajumuisha bodaboda wote na kusema ifutwe sekta nzima.
Hizo sio akili ni Hisia.
Kimsingi ukiona driver pikipiki anafanya hayo ya wizi huyo si bodaboda ni kibaka tu anaetumia pikipiki kutekeleza uhalifu wake.
 
Nakujibu kesho nikitulia
 
Umesema kweli boss, sema shida hii ni Tanzania ya CCM, sio kwamba tunapenda kuwa boda, kumbuka zile point za shule, lack of capital, poor government support, poor infrastructure, bad leadership etc, kama wewe umetoboa upo kwenye kundi la wachache, uku mtaani watu ugari tu kuupata ni kazi hali ngumu sana, kama mungu amekupa waombee wengine wapate sio kuwasimanga, a 90% ya bodaboda hawapendi hiyo kazi ni maisha tu yanawapelekea kufanya hiyo kazi na pesa inayopatikana ni ya kujikim tu lakini huwezi pata mtaji ndio mana unaona mtu ana 50yr bado ni boda hivyo tu
 
Nikweli
 
Hili bandiko lako ni zuri ila umetumia ukali sana but all in all hakuna mzazi yoyote angependa mwanae awe boda boda

Mala nyingi usafiri wangu ni huo pamoja na kuzingatia boda boda msafi na mlefu bado kufika salama unapoenda ni 50/50
 
Watafutiwe suluhisho, binafs naona bodaboda kufutwa sio sahihi

Wengine wanasema ni laana “ nimepoteza ndugu +marafiki wazidio 7 roho inaniuma sana na wengine wamenusurika ulemavu kama sio akiba na M/Mungu kutia neema zake wangekuwa walemavu

Binafsi naona inawezekana kutafutiwa suluhisho kwani boda boda ni ajira kwa wengi sana na wanaendesha familia zao ila wanapata ajali sana mpaka unaweza kuhofia kutumia usafiri huo
 
Boda watambulike na wajisajili kwa vigezo maalumu sio kila anayetaka anachkua boda anapaki kuanza kazi No
 
Boda watambulike na wajisajili kwa vigezo maalumu sio kila anayetaka anachkua boda anapaki kuanza kazi No
Tuwe wa kweli, nchi yetu rushwa imekithiri ni kubwa mno ndyo inasababisha vyote hivyo

Ukiangalia mitaa/jamii zetu ni kama zinajiendesha zenyewe karibia nchi nzima, mifumo yetu ni ovyo na duni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…