Kwanini sekta ya Bodaboda isifutwe? Ni kimbilio la waliofeli, wanajazana mochwari na wazalishaji wa wajane mtaani

Mzee sikuhizi unatema facts tu.
 
😂😂😂
 

Amezingua toka uzi wake wa kwanza... alisema wanaume wasio na hela na wana miaka 29+ wavae sketi waolewe na nyinyi mkampa sapoti. Ona sasa kapata bichwa anaendelea kujiaibisha.

Ukiwa na mafanikio hauwez kuponda wasio na mafanikio.

Kwanza hana nyumba.
Ana gar la mill 5.5, alishindwa kulipa sim ya mkopo, alikuwa anatafuta mganga wa kusafisha nyota.

Hizi nyingne ni porojo tu . Kujiona amefanikiwa.
Maisha yanabadilika sana. Na huyu hayajui maisha.
Kuwa na gar asijione boss.
 
Duh
 
Siku ukipanda bodaboda ufe kuh na nimeomba kwa jina la yesu mwokozi wa bodaboda muumba mbingu na barabara zote za ulimwengu wa pikipiki na bajaj.
 
Kasome vizuri uzi zangu, nilikuwa natafuta mganga kwa ajili gani, kasome vzr nilikuwa silipi simu kwa ajili gani unajua sahv natumia simu gani

Nashinda site hiyo boma ni ya 3
 
ule uzi wa kwanza nilifurahia kidogo baada ya kuona hiyo jinsia yenu mnasemwa kwasababu nyuzi nyingi humu zilikua zinatusema ke mpka tukakoswa pa kupumulia 😅😅

watu mnatunza mafaili loh😂😂😂 kwahiyo ulirudi maktaba kupitia document za nyuma?🤭
 
Umekusanya pointi nyingi muhimu ukaziweka pamoja ziwe kama kitu kimoja😁.
Ila umeeleweka japokuwa hujafanya tafiti, kuna walinzi wa kampuni za ulinzi na JKT, kuna waalimu, kuna askari polisi, ffu, kuna wafanyakazi zingine binafsi ambao wote baada ya kazi huingia mtaani kufanya bodaboda ili kujiongezea kipato "nawajua wengi", kuna bodaboda wenyewe ambao muda mwingi hii ndiyo kazi yao siku nzima, kuna waendesha pikipiki ambao hawafanyi biashara ya kupakia abiria, tunapozungumza tuwe tunasema tunawalenga wa aina ipi??

Kuhusu kusubiri abiria wa elfu moja kijiweni, ukumbuke hata ukifungua duka utakaa hapo kusubiria mteja anayekuja kununua sigara ya mia moja, au pipi ya hamsini, upande wa kusubiri mteja wa bei Gani? hiyo ni riziki ya mola, watu wengi mashuleni wamefundishwa kwamba plan A ikifeli ingia plan B unayoiweza

Kila mwenye chombo Cha moto unayemuona barabarani ujue yupo kisheria, na amekamilika na ameruhusiwa ndio maana kuna traffic wa kuzuia asiyestahili asitumie hivyo vyombo, wanakuwa wamesoma na Wana leseni pia

Kikubwa Kila mmoja ana Haki ya
kutumia barabara, kuheshimiana wawapo barabarani, tusijihesabie haki, tupendane. Wenye bodaboda wengi ndio wamenunua bajaji unazoziona wengine wamenunua Hadi hiace za kubeba abiria, Mtu yeyote anayekuwa barabarani anaweza kufa muda wowote kwa chochote anachotumia awapo barabarani. Ni hayo kidogo nimekukumbusha unapoendelea kuwashutumu hao ndugu zako
 
[emoji23]
 
Huyo mshamba kwa sababu amepata check no. kupitia Ajira Portal anapata hela ya kulipa kodi na IST ya mkopo anajiona kamaliza maisha😂! Boda boda nao ni binadamu kama sisi wana utashi na majukumu ndio yanawasukuma kuingia barabarani kubeba abiria. Kama anakerwa na boda boda wafanye swap tu yeye akae nyumbani amuachie ajira yake boda boda.
 
Au sio naona unachamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…