Kwanini sekta ya Bodaboda isifutwe? Ni kimbilio la waliofeli, wanajazana mochwari na wazalishaji wa wajane mtaani

Inasikitisha zaidi ukizunguka vijiweni unakuta jitu zima, lina miaka 39 au 40 na ushee, lina mvi hadi kwenye kidevu, lakini bado limekalia chuma linasubiri abiria wa buku jero! Jitu limeshakuwa zito barabarani, limechoka, lina wepesi sifuri wa kukwepa hatari, badala ya kufanya mambo ya maana au kurudi kijijini kulima, linaishia kushindana na vijana wa miaka 18 barabarani na kusubiri kufia kwenye lami.
 
acha dhihaka ndugu, Mungu hadhihakiwi.
 
Kimbilio la walio feli how! waliofaulu ni wapi ! #nonsense
 
Mtawapeleka wapi na hamna viwanda,bidhaa zotezinatoka china.
 
Hili povu itakua bodaboda kakuchapia mkeo na kumtia mimba juu,pole sana.
 
Bahati mbaya ata Uzi uwe viral vp hakuna malipo, kulikua na mtu alikua anachana walimu sana na nyuzi zake ila badae alichoka mwenyewe, ata we utachoka 4 the mean time changamsha genge
 
Mungu awabariki vijana wote wa bodaboda wanaotufanyia kazi kwa Uaminifu mkubwa,

Awakinge na ajali na mauti,. wapate riziki zao kama wengine wanavyopata

Ameen
 
Mkuu sasa unatuthkana katika jitihada zetu za kupata mkate wa kila siku....mnataka tukaine sasa au?
Kwanza muwa boda raha mzeya mbunye nje nje
 
Ingawa mtoa mada katumia lugha kali lakini kiukweli kuna kitu inabidi kifanyike kuhusu hawa bodaboda. Wapo careless sana na kazi yao ni kifo au ulemavu nje nje. Vilevile ndio vinara wa kutia mimba mabinti wa sekondari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…