Kwanini Serikali haipigi marufuku uingizaji wa mitumba?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hakuna nchi inayoweza kuendelea bila kulinda na kuendeleza viwanda vya ndani. Na njia kuu ya kulinda viwanda vya ndani ni kuzuia bidhaa cheap kutoka nje ya nchi.

Ndiyo maana China waliikataa Google, facebook nk. Ndiyo maana US waliipiga pini Huawei. Hili jambo mataifa karibu yote ya Afrika wanalichukulia poa, na ndiyo maana karibu bara lote masikini.

Viwanda vyetu vya mavazi haviwezi kuendelea iwapo tunapata nguo na viatu vya bei rahisi vya mitumba kutoka nje.

Ni sekta nyingi inatakiwa kudhibiti cheap imports, nimezungumzia mavazi sababu ndiyo huwa vitu vya kwanza kwa nchi inayoanza kuwa ya viwanda.

Kwanini Serikali haizuii mavazi ya mitumba ili tuanze kupiga hatua za maendeleo?
 
Sababu zilizosababisha nchi ikaruhusu mitumba bado ziko pale pale na inwezekana nyingine zimekuwa kubwa zaidi;
Hivi tuna viwanda vingapi vya viatu?
 
Una viwanda vya nguo wewe

Ova
 
Watu wavae nn
Hapo wazalishaji wa kushona watapata kazi na ajira kibao zitatengenezwa. Viwanda vya kuzalisha vitavyoshindana na mpya kutoka nje vitaanzishwa. Leo hii kiwanda cha nguo au viatu hakiwezi shindana na mavazi ya mtumba sokoni.
 
Halafu mitumba ya bei rahisi unavaa ww na hao mafala wenzio...
kuna mtumba quality na bei juu hujawahi fikiri
Unataka kusema huo mtumba unaizidi bei hiyo nguo ikiwa mpya? Mitumba yote ni cheap.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…