Kwanini Serikali haipigi marufuku uingizaji wa mitumba?

Ulaya wanavaa mitumba lakini hawaimport. Kuna tofauti kubwa. Na kiuchumi, licha ya Bangladesh kuwa nchi ndogo sana kwa eneo na rasilimali, imetuacha mbali sana kiuchumi.
Kweli Mkuu na wapo wengi pia 168m population yao
Ila sisi ni uvivu na kutokujituma labda
Najua watasema mbona tunafanya kazi sana

Nafikiri tatizo ni uaminifu unachangia pia
Wao wanapata tenda nyingi kutoka mataifa ya Ulaya kuwashonea nguo kwa mshahara wa huko kwao

Kama tukiweza kuwa waadilifu na kujituma na kutokuwa wahujumu katika Taifa letu huenda just huenda tukafika mahali
 
vitatoka wapi na kuna cheap imports za mitumba? mbona hoja ndiyo inazungumza suala hilo!!?
Mkuu wangu hii issue inahitaji commitment isiyokuwa ya kawaida kama nchi kisera. Ili tufanikiwe tunatakiwa tuanze na mapinduzi kwenye kilimo kwanza ndipo zinapotoka material, tupate umeme wa uhakika ndio sasa tufungue viwanda. Marufuku ya uingizwaji wa mitumba, hautasaidia kama hayo juu hayajafanyika. Zaidi sana utasababisha uhaba wa nguo tutaanza kuzinunua kwa foleni kama enzi za mwalimu.

Tukirudi kwenye mapinduzi ya kilimo, Je unajua kuwa kuna kiwanda mahali fulani kimesitisha uzalishaji sababu waliwawezesha wakulima walime wao wanunue na wakulima hawajapata mavuno ya kutosha kupelekea kiwanda kisitishe uzalishaji kwa muda hadi msimu ujao.
 
Ukichuguza kwa makini, mitumba imesaidia sana hasa watu wa kipato cha chini. Ukinunua shati jipya la kibongo, siku chake limepauka na kuzeeka. Mtumba upo ngangari.
 
Kweli Mkuu na wapo wengi pia 168m population yao
Ila sisi ni uvivu na kutokujituma labda
Najua watasema mbona tunafanya kazi sana

Nafikiri tatizo ni uaminifu unachangia pia
Wao wanapata tenda nyingi kutoka mataifa ya Ulaya kuwashonea nguo kwa mshahara wa huko kwao

Kama tukiweza kuwa waadilifu na kujituma na kutokuwa wahujumu katika Taifa letu huenda just huenda tukafika mahali
Wanaexport sana. Bahati mbaya ukuaji huo hadi uweze kuexport ni lazima viwanda vya ndani vikue. Na kukuza viwanda vya ndani ni lazima serikali ivilinde dhidi ya cheap imports. Au tunaweza tengeneza EPZs(Export processing zones) kwaajili ya hizo bidhaa na kuziwezesha kwa misamaha ya kodi nk. Hilo nalo linaweza kusaidia sana
 
Nauza mitumba grade one...mtumba wa nguo za mashuka. Pure cotton, King-size....yanakua mashuka mawili na foronya 4. Mashuka ni makubwa sana afu mazito. BEI kwà kila pair nauza 70,000.

Belo lake linauzwa 960,000/= , ni la kilo 45. Ndani zinakaa 25 pieces.

Ni mashuka ambayo hayajalaliwa. I mean....ni yale ambayo yanabaki huko kwa wazungu....then yanafungwa kama mtumba bila hata yavkutumiwa.
Wanaita old stock. Wakiwa wanaingiza mali mpya kwenye stores au magodown wanazitoa za zamani.
 
Futuhi, ubora ndio jambo la mwisho kwetu, Pamba tunayo, ngozi tunazo n.k n.k

Ila viatu/sendo tunazotengeneza achilia tuu finishing mbaya tuu! unakuta kiatu/sendo inanuka uvundo wa njama kabisa, Kuna siku nimevua zile sendo za kimasai asubuh nakuta mbwa anapambana nayo..

Nguo ndio Bure kabisa labda tuvae kanga, mchawi maji,
T-shirt Ukiifua tuu kesho yake unavaa Joho.
 
Kunanguo za kuzuia hasa za ndani.
Halafu wale vijana pale karume na masoko mengine yote tz utawaajiri wewe?
Ukileta wazo la kuua kitu njoo na wazo mbadala pia. Usikurupuke
 
Mkuu wangu hii issue inahitaji commitment isiyokuwa ya kawaida kama nchi kisera. Ili tufanikiwe tunatakiwa tuanze na mapinduzi kwenye kilimo kwanza ndipo zinapotoka material, tupate umeme wa uhakika ndio sasa tufungue viwanda. Marufuku ya uingizwaji wa mitumba, hautasaidia kama hayo juu hayajafanyika. Zaidi sana utasababisha uhaba wa nguo tutaanza kuzinunua kwa foleni kama enzi za mwalimu.

Tukirudi kwenye mapinduzi ya kilimo, Je unajua kuwa kuna kiwanda mahali fulani kimesitisha uzalishaji sababu waliwawezesha wakulima walime wao wanunue na wakulima hawajapata mavuno ya kutosha kupelekea kiwanda kisitishe uzalishaji kwa muda hadi msimu ujao.
Ni kweli, lakini naona kwa sasa watz ni industrious sana ukilinganisha na kipindi cha Nyerere. Wanaweza kuziba uhaba wowote kwa haraka kama walivyoziba ishu ya mifuko ya plastic.
 
Kunanguo za kuzuia hasa za ndani.
Halafu wale vijana pale karume na masoko mengine yote tz utawaajiri wewe?
Ukileta wazo la kuua kitu njoo na wazo mbadala pia. Usikurupuke
Utashangaa jinsi ajira za ushonaji nguo, waunda zipu, vifungo, washona viatu, wafanya tanning ya ngozi, watengeneza zip nk nk zitakavyozalishwa. Nyingi kuliko za hao wauza mitumba. Nao wengi waa hao wauza mitumba bado watauza hizo nguo na viatu vipya.
 
Futuhi, ubora ndio jambo la mwisho kwetu, Pamba tunayo, ngozi tunazo n.k n.k

Ila viatu/sendo tunazotengeneza achilia tuu finishing mbaya tuu! unakuta kiatu/sendo inanuka uvundo wa njama kabisa, Kuna siku nimevua zile sendo za kimasai asubuh nakuta mbwa anapambana nayo..

Nguo ndio Bure kabisa labda tuvae kanga, mchawi maji,
T-shirt Ukiifua tuu kesho yake unavaa Joho.
Polepole ubora huwa unakuja. Nchi nyingi zinafahamu kuwa mtumba ni cheap na unawavutia wananchi lakini walipiga marufuku. Wanajua athari zake kwa uchumi.
 
Hayawezi kujisort wala hawataweza kuzalisha nguo quality iwapo wanashindanishwa na mitumba cheap sokoni.
Wote wana afford nguo ya kushindia kwa elfu 15? We wish. Nchi yenyewe kila mtu anachumia tumbo lake, hadi hiyo ela ije ikufikie wewe wa kibondo uweze kununua nguo ya dukani mbona utakoma.. tatizo viwango vya nguo na bei haziendani
 
Ni sababu hakuna viwanda vya kutosha kushindana wao kwa wao. Ukitoa mtumba utaona viwanda vingi vikianzishwa. Vikijaribu kuzalisha vitu kwa fahion na quality ya mtumba.
 
Na kodi zetu hizi? Na TRA wamekukalia kooni? Wa kufungua viwanda labda makaburu. Watanzania tuna mioyo sana na biashara ila authorities ni kama zinashindana nani anaweza kukusanya kodi zaidi.

Naona tuiachie serikali ifungue viwanda vyake vya nguo maana wakifungua wananchi ni kama wamechokonoa milango ya kusumbuliwa na mamlaka za mapato. Figisu
Kama zote.

Mnataka mtuvalishe midosho yenu mifamba sare sare maua?
Kifupi ipo mitumba mironya na quality
 
Kwani kuna viwanda vingapi vya nguo mkuu?

Natamani ungesema hata vipo 20 ili iwe rahisi kuelewa hoja yako.
Watu wa Dar ndio uendekeza mitumba, ukienda mikoani watu wamepiga spesho zao wala hawana habari na mtumba, waulize akina mama washona vyeleani wanavyonufaika na kushona vitenge, lkn wa dar wao upunguza matambala ya mitumba
 
Kuna viwanda vya nguo vingapi ambayo mauzo yake yaneshuka Hadi ukaamua kuanzisha huu Uzi?
 
Na kodi zetu hizi? Na TRA wamekukalia kooni? Wa kufungua viwanda labda makaburu. Watanzania tuna mioyo sana na biashara ila authorities ni kama zinashindana nani anaweza kukusanya kodi zaidi.

Naona tuiachie serikali ifungue viwanda vyake vya nguo maana wakifungua wananchi ni kama wamechokonoa milango ya kusumbuliwa na mamlaka za mapato. Figisu
Kama zote.
Ndiyo hapo serikali inakuwa na mkakati wa kusaidia viwanda hivi. Kwa misamaha ya kodi na kuhakikisha vinakua. Ukipiga marufuku na usisaidie ukuaji wa ndani bado unakuwa hujafanya kitu cha maana sana.
 
Kuna viwanda vya nguo vingapi ambayo mauzo yake yaneshuka Hadi ukaamua kuanzisha huu Uzi?
Kwa jinsi mitumba inavyovaliwa, tushukuru hata hivyo viwili vitatu vilivyopo. Kulitakiwa visiwepo kabisa.
 
Back
Top Bottom