Kwanini Serikali haipigi marufuku uingizaji wa mitumba?

Kwanini Serikali haipigi marufuku uingizaji wa mitumba?

Nchi haiwezi kuendelea kwa mtazamo huo. Ni sawa uwaambie watoto nyumbani kuwa tubane matumizi tunataka kujenga nyumba halafu waanze, "Acha zako."
Tutavaa nini? Nguo za dukani nzuri ni gharama.
 
Sababu zilizosababisha nchi ikaruhusu mitumba bado ziko pale pale na inwezekana nyingine zimekuwa kubwa zaidi;
Hivi tuna viwanda vingapi vya viatu?
Hatuna viwanda vya nguo na viatu vya kutosha sababu ya uagizaji wa mitumba ya bei rahisi. Na si kuwa tunaagiza mitumba sababu hatuna viwanda vya mavazi.
 
Urafiki, mwatex, sungura tex, kiltex mutex, vyote vilikufa sasa nitajie, viwanda vya nguo tulivyonavyo Tanzania
Vipo vingi kama nida industries. Lakini bado viko chini sababu haviwezi shindana na mitumba.
 
Hakuna nchi inayoweza kuendelea bila kulinda na kuendeleza viwanda vya ndani. Na njia kuu ya kulinda viwanda vya ndani ni kuzuia bidhaa cheap kutoka nje ya nchi. Ndiyo maana China waliikataa Google, facebook nk. Ndiyo maana US waliipiga pini Huawei. Hili jambo mataifa karibu yote ya Africa wanalichukulia poa, na ndiyo maana karibu bara lote masikini.

Viwanda vyetu vya mavazi haviwezi kuendelea iwapo tunapata nguo na viatu vya bei rahisi vya mitumba kutoka nje. Ni sekta nyingi inatakiwa kudhibiti cheap imports, nimezungumzia mavazi sababu ndiyo huwa vitu vya kwanza kwa nchi inayoanza kuwa ya viwanda.

Kwa nini serikali haizuii mavazi ya mitumba ili tuanze kupiga hatua za maendeleo?
Viatu vyangu kwenye mikokoteni elf kumi tu, mashati elf nne ,surual Kuna sehemu elf mbili siku hizi siwaoni wako wa kaki kaki
 
Mijitu mingine ina roho mbaya ka nini yani...sasa Serikali ikipiga marufuku sisi wauza mitumba tutauza nini?

Kama huna kitu cha kupost...si uwege msomaji tu? Hili jamaa linajifanya lijuaji sana. Afu humu jf tushakuchoka na sera zako za ajabu ajabu!!!!
 
Hakuna nchi inayoweza kuendelea bila kulinda na kuendeleza viwanda vya ndani. Na njia kuu ya kulinda viwanda vya ndani ni kuzuia bidhaa cheap kutoka nje ya nchi.

Ndiyo maana China waliikataa Google, facebook nk. Ndiyo maana US waliipiga pini Huawei. Hili jambo mataifa karibu yote ya Afrika wanalichukulia poa, na ndiyo maana karibu bara lote masikini.

Viwanda vyetu vya mavazi haviwezi kuendelea iwapo tunapata nguo na viatu vya bei rahisi vya mitumba kutoka nje.

Ni sekta nyingi inatakiwa kudhibiti cheap imports, nimezungumzia mavazi sababu ndiyo huwa vitu vya kwanza kwa nchi inayoanza kuwa ya viwanda.

Kwanini Serikali haizuii mavazi ya mitumba ili tuanze kupiga hatua za maendeleo?
ivi mtumba grade one unaujua?
 
Vipo vingi kama nida industries. Lakini bado viko chini sababu haviwezi shindana na mitumba.
Vipo vingi halafu unataja halafu sizungumzii mafundi cherehani ila viwanda vya kuzalisha vitambaa hadi final product kuweza kuwavisha watanzania wote waitegemee mitumba
 
Hakuna nchi inayoweza kuendelea bila kulinda na kuendeleza viwanda vya ndani. Na njia kuu ya kulinda viwanda vya ndani ni kuzuia bidhaa cheap kutoka nje ya nchi.

Ndiyo maana China waliikataa Google, facebook nk. Ndiyo maana US waliipiga pini Huawei. Hili jambo mataifa karibu yote ya Afrika wanalichukulia poa, na ndiyo maana karibu bara lote masikini.

Viwanda vyetu vya mavazi haviwezi kuendelea iwapo tunapata nguo na viatu vya bei rahisi vya mitumba kutoka nje.

Ni sekta nyingi inatakiwa kudhibiti cheap imports, nimezungumzia mavazi sababu ndiyo huwa vitu vya kwanza kwa nchi inayoanza kuwa ya viwanda.

Kwanini Serikali haizuii mavazi ya mitumba ili tuanze kupiga hatua za maendeleo?
Unataka wote tuvae vijora? Hivi umeona nguo zinazotengenezwa hapa tz? Ni huruma yani nguo ukikohoa imechanika. Sio kwa ubaya lakini tuongeze viwango. Na hizo nguo zinazotengenezwa na hawa mafundi wetu ni hela ya balo la mtumba. Mkuu acha tu mambo yatajisort tuhangaike na shida ya maji na umeme kwanza
 
ivi mtumba grade one unaujua?
Nauza mitumba grade one...mtumba wa nguo za mashuka. Pure cotton, King-size....yanakua mashuka mawili na foronya 4. Mashuka ni makubwa sana afu mazito. BEI kwà kila pair nauza 70,000.

Belo lake linauzwa 960,000/= , ni la kilo 45. Ndani zinakaa 25 pieces.

Ni mashuka ambayo hayajalaliwa. I mean....ni yale ambayo yanabaki huko kwa wazungu....then yanafungwa kama mtumba bila hata yavkutumiwa.
 
Mijitu mingine ina roho mbaya ka nini yani...sasa Serikali ikipiga marufuku sisi wauza mitumba tutauza nini?

Kama huna kitu cha kupost...si uwege msomaji tu? Hili jamaa linajifanya lijuaji sana. Afu humu jf tushakuchoka na sera zako za ajabu ajabu!!!!
Hiyo ndiyo njia pekee ya nchi ya kuendelea. Umasikini wetu hautokani na rushwa, ujinga wala viongozi wabovu. Unatokana na hapa tumeshinda tambua jinsi cheap imports zinavyoathiri uchumi wetu.
 
Vipo vingi halafu unataja halafu sizungumzii mafundi cherehani ila viwanda vya kuzalisha vitambaa hadi final product kuweza kuwavisha watanzania wote waitegemee mitumba
Kama unataka sana kuvijua vitafute. Na hakuna aliyesema vinatosha kuvisha watanzania wote, hivi umeelewa hata mada?
 
Unataka wote tuvae vijora? Hivi umeona nguo zinazotengenezwa hapa tz? Ni huruma yani nguo ukikohoa umechanika. Sio kwa ubaya lakini tuongeze viwango. Na hizo nguo zinazotengenezwa na hawa mafundi wetu ni hela ya balo la mtumba. Mkuu acha tu mambo yatajisort tuhangaike na shida ya maji na umeme kwanza
Hayawezi kujisort wala hawataweza kuzalisha nguo quality iwapo wanashindanishwa na mitumba cheap sokoni.
 
4620 ndio viwanda vya nguo vilivyopo Bangladesh lakini viraka vimejaa na umasikini wa kutupa

Hata Ulaya watu wanavaa mtumba
Na wanatengeneza nguo kwa pamba yetu
Huoni kuna haja ya kutumia akili hapo
Ulaya wanavaa mitumba lakini hawaimport. Kuna tofauti kubwa. Na kiuchumi, licha ya Bangladesh kuwa nchi ndogo sana kwa eneo na rasilimali, imetuacha mbali sana kiuchumi.
 
Back
Top Bottom