Kwanini Serikali Ikope Kuendesha Miradi, Wakati inaweza Kutengeneza Pesa ?

Kwanini Serikali Ikope Kuendesha Miradi, Wakati inaweza Kutengeneza Pesa ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kabla hatujaitana vichaa, kwanza kabisa tukubaliane kwamba ndicho kinachotokea sasa hivi duniani (creating money from thin Air) ingawa ni Benki ndio zinafanya hivyo...

Pesa inavyotengezwa na kuongezwa kwenye Mzunguko na Benki
  • Wewe ukienda kuomba mkopo Benki unapewa pesa ambayo Benki haina wala haipo ukizungusha huko kitaa unakiwarudishia unakuwa umeongeza pesa kwenye mzunguko kwa kurudisha kile ulichopewa na interest (faida) ya benki.

Serikali Inavyopata Pesa za Matumizi / Miradi
  • Tofauti na ile ya kukopa moja kwa moja kama sisi wadau wa mtaani ambayo Riba yake inaweza kuwa kubwa Serikali karibia zote ulimwenguni huwa zinatengeneza Government Bonds (Hati Fungani) na kuziuza na kupewa hizo pesa za kufanyia mambo yao, hapo wakopeshaji ni walionunua hizo Bonds.., kwahio Serikali inavyokusanya hizo pesa na kuwarudishia hao walionunua bonds (wakopeshaji) au mabenki binafsi na ya kidunia huo mradi unakuwa umegharimu pesa iliyokopwa kujumlisha na RIBA.
  • Vilevile kwa kutembeza bakuli na so called mikopo yenye RIBA nafuu kutoka IMF n.k. (Ila unafuu huo bado unakuwa una RIBA) ambayo vinginevyo isingekuwepo.

Kwanini Serikali isiprint moja kwa moja kufanya inavyotaka
  • Tukiachia Serikali ifyatue pesa inavyotaka inaweza ikaziprint bila kujali hivyo kupelekea pesa kuwa nyingi kuliko bidhaa na pesa kushuka thamani na watu kutokuamini pesa hio.

Kwanini Miradi ya Serikali na Vitu vinavyofanyika nchini Serikali Ikope au kutumia Mabenki na Isiongeze Pesa Moja kwa Moja ili Kuepuka Riba na Gharama
  • Kuepuka ufujaji tunahitaji Uwazi (Transparency) yaani kila senti inaonekani imefanya nini na ipo wapi, na matumizi yawe tu kutoka kwenye Bajeti na sio mtu kujiamulia kufanya matumizi hayo.
  • Kwa miradi ambayo inaweza kufanyika ndani ifanyike ndani kwa wakandarasi wa ndani (sababu wadau hawa watalipwa kwa pesa ya ndani, na bidhaa zote zitatumia pesa ya ndani kununuliwa) hivyo kuna umuhimu wa self reliance (yaani uwezo wa kupata bidhaa za ndani bila kuhitaji pesa ya nje kufanya manunuzi); Sio kuhitaji kununua Dollar ili kumlipa anayemwaga zege wakati anayemwaga hio zege angeweza kulipwa kwa Tshs.
Hitimisho:
Kwa Mtiririko huo hakuna sababu ya kukopa Pesa nje ili kufanya miradi alafu baadae wananchi wenyewe ndio waje walipe pesa hizo na Riba, badala yake wakopwe wananchi kwenye bajeti (deficit) ili mradi ufanyike na baadae wanalipa kutokana na makusanyo au chochote kile (tofauti ya kufanya hivyo ni kwamba hapa gharama inakuwa ndogo hakuna RIBA)

Angalizo; Kwa kufanikisha hili inabidi tuache / tupunguze utegemezi kwa Pesa za Kigeni, Miradi mingi itumie / iweze kufanyika kwa manunuzi yanayoweza kutumia Pesa za ndani, sisi sio kama USA ambayo inaweza ikatoa Hati Fungani ambazo ni dunia nzima ndio zinaguarantee wao kufanya matumizi wanavyotaka.
 
Kama sisi ndio tunalipa na TUNALIPA NA RIBA, kwanini sisi ndio tusiwakopeshe ili tulipa kwa nguvu kazi na mwisho wa siku lile deni lisiwe na hii Riba ?
 
Back
Top Bottom