Na GENTAMYCINE naomba Kumjua huyu Mtu ( Watu ) ambao walikubaliana kuwa 'Watufiche' Watanzania Kuugua Kwake Hayati Rais Dkt. Magufuli.
Kwani Watanzania tokea tu Kuanza Kuugua Kwake tungetangaziwa Kungeharibika nini hadi tukafichwa Kiasi kile?
Nina uhakika kwa Watanzania jinsi tulivyobarikiwa kuwa ni Watu wa Imani za Kimaombi kwa Mwenyezi Mungu huku na Sisi wengine akina GENTAMYCINE tukiwa ni Watu wa kuamini Mizimu yangu ya Kizanaki, Kisimbiti, Kimakuwa na Kiyao kwa pamoja tungemuombea na angepona ili aendelee Kupiga Kazi na kutuongozea vyema Tanzania yetu iliyokuwa inaanza kwenda vyema tofauti na inavyoanza kurudi nyuma tena sasa.
Tukielekea Kumaliza huu Mwaka wa 2021 GENTAMYCINE sitaki kuwa Mnafiki na kukaa nalo Moyoni hili na leo bila Uwoga nasema Hayati Rais Dkt. Magufuli hakuondoka Mwenyewe bali Kalazimishwa kuondoka, ila naamini ipo Siku tu isiyo na Jina ukweli utajulikana.
Namalizia huu Uzi wangu kwa Kuuliza mara nyingine tena ni kwanini Watanzania tulifichwa Kuugua kwa Rais Hayati Dkt. Magufuli? Na lengo Kuu la Kutuficha lilikuwa ni nini? Kwani tungetangaziwa mapema kuhusu Kuugua Kwake tungeharibu Mpango gani uliokuwa Gizani dhidi yake hili Jembe la uhakika?
Nayasubiri tu majibu yenu ya uhakika!!!
Gentamicin is an antibiotic au ? Then hii mada ilitakiwa iende Intelligence ni mada nzito sana.
Pamoja na yote, but JPM alikuwa anawakilisha hisia za Watanzania wengi sana and he was smart kwenye uongozi. Jamaa alikuwa ni RAIS wa maono na misimamo.
Waliokatisha uhai wa JPM ni wahuni. Ndani ya TISS kulikuwa na TISS ambayo ilijinasibisha loyal kwa JPM .humo humo wahuni wakatembea na kupitia viongozi wa karibu wa JPM .
Kumbuka kuna watu ndani ya TISS hadi leo hawamkubali diwani, na kuna watu ndani ya Jeshi hawamkubali Mabeyo. Hizi zote ni team JPM zisizokubalika ndani ya vitengo
Ni chain iliyozunguka ndani kwa ndani na ikafanikiwa. Wahuni hao walipokamilisha wakaanza kuua legacy ya JPM kwa kumtumia Kichere, wahuni walishindwa kutangaza hata kifo cha Rais kiheshima.
Wahuni hao hao wakasambaza hadi video za marehemu .
Worst enough, wahuni ambao wengine walikuwa kwenye highest position Kwenye utawala wake publicly anaongea kabjsa kuwa utawala uliopita ndio ulikuwa mmbaya, sio utawala wa awamu ya 6 ; ni aibu and it’s shame kwa manufaa ya nchi.
Kosa kubwa la JPM ni kuwekeza kwenye ulinzi wa gun badala ulinzi wa kisayansi na asilimia kubwa alikuwa amezungukwa na wanafiki.
Naamaanisha hadi VP wake wa kipindi hicho alikuwa ni snitch kwake na alipenyeza mambo mengi sana kwa wahuni ikiwa ni pamoja na weakness point za JPM.
Na ndio maana leo hii anajisahau na kumkana waziwazi na kuuponda utawala ambao yeye ndiyo alikuwa mshauri wake wa karibu sana . Usnitch ni dhambi mbaya na haijawahi kumuacha mtu salama.
Hawa ndio watu waliofanikisha matukio makubwa. Yaani JPM alitakiwa awamu ya pili atoe takataka zote.
Wahuni wameingia madarakani wakaona jamaa alikuwa na Project kubwa nchini na zote zilikuwa zinaenda, wapi alikuwa anapata fedha; hawakuwa na majibu , njia pekee ni tozo na takataka nyingi.
Na miradi ya barabara na mwendokasi inasua sua huku wahuni wanakula pipa na jopo lao , ukipiga cost inakwenda zaid ya B kila trip .
Tunahitaji JPM mwingine , huyu jamaa atakumbukwa tu , miaka 6 but alama ni kubwa za Maendeleo.
Ni suala la Muda , karma is bitch , they will never be happy !