Kwanini serikali imebariki magari ya viongozi wa serikali kuwa namba feki? Mwanzo nilizani ni uhuni wa madereva kumbe wanapewa wabandike feki

Huo utaratibu umeanza lini? Na ndiyo mmepanga muwe mnazibadilishabadilisha kadri mtakavyo? Huo ni uhuni wa kufichia maovu.
 
Huo ni utaratibu huko kwenu tu TZ na umeanza lini? Wengine wazazi wetu walikuwa serikalini na hayo magari ndiyo yalikuwa yakitupeleka na kuturudisha mashuleni kila siku lakini hayakuwahi kuwa na numbers mbilimbili huu utaratibu mliouanzisha ni kwa malengo gani? Au ndiyo kutengeneza loopholes za watekaji na wauaji?
 
Huu wanaodai ndiyo utaratibu umeanza lini? Ni mambo wanayojifania kwa kuficha uovu wanaoufanya.
 
Sijamaanisha kutetea ndiyo maana nimekuuliza ungekuwa mshauri wa masuala ya usalama kwa viongozi wa nchi hasa wa kitaifa ungeruhusu jambo hili ama ungekataa?
Kwa upande mwingine, issue ya magari ya serikali kutumika na viongozi kwa masuala binafsi hilo lipo sanaa tuu. Inategemea na wadhifa alionao, ulishawahi kusikia Rais yupo likizo? Je ulishawahi kumuona akitumia magari yake binafsi aliyonunua kwa fedha zake? Je baadhi ya wastaafu pia huwa wanatumia magari binafsi?
Shida ipo kwa asiyestahili kuwa nalo baada ya muda wa kazi akakutwa nalo. Hapo ndiyo kuna shida kiongozi.
 
Ninachofahamu gari mfano yenye namba W EL huwa ina namba zake STL au STK ambazo zinatumika boss asipojuwepo kwenye gari. Hii ya namba za kawaida BCD au EFG ndio nasikia leo.
Kwahio hizi LC300 zenye namba T...ABF au T...BGA ziliingia nchini lini?
 
Ninachofahamu gari mfano yenye namba W EL huwa ina namba zake STL au STK ambazo zinatumika boss asipojuwepo kwenye gari. Hii ya namba za kawaida BCD au EFG ndio nasikia leo.
Kwahio hizi LC300 zenye namba T...ABF au T...BGA ziliingia nchini lini?
Inawezekana kabisa unachosema Kiongozi ni sahihi, lakini pia tukumbuke mambo hubadilika hayabaki hivyo hivyo.
 
Jaribu kutofautisha kupanda gari inayombeba baba/ukiwa kama abiria kwenda kazini na kupanda gari kama mtumishi
 
Ukija kujua gari hilohilo linawekwa bendera ya chama na kumsafirisha kiongozi wa chama si utalia 😅
 
Reactions: Lax
Naungana na wewe kwa asilimia mia. Unajua hawa jamaa wanatoa majibu yao uchwara humu wanafikiri huko serikalini wanafanya kazi wenyewe na hakuna watu wengine wenye uelewa zaidi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…