Kwanini serikali imebariki magari ya viongozi wa serikali kuwa namba feki? Mwanzo nilizani ni uhuni wa madereva kumbe wanapewa wabandike feki

Kwanini serikali imebariki magari ya viongozi wa serikali kuwa namba feki? Mwanzo nilizani ni uhuni wa madereva kumbe wanapewa wabandike feki

Dah .
Ngojeni niwaeleshe, Gari yoyote inayoingia nchini lazima isajiliwe kwa plate number za kawaida.. zile tunazozijua za T454 EGF(mfano).. alafu kisha ndiyo kama za serikali zinapewa Hizo namba zao za STM,. Kwahyo zile za serikali ubandikwa wakati tayari hizi gari zina plate no. Za kawaida za mfumo wa nchi..
Huo utaratibu umeanza lini? Na ndiyo mmepanga muwe mnazibadilishabadilisha kadri mtakavyo? Huo ni uhuni wa kufichia maovu.
 
Elimu elimu elimu

Shida ya wabongo huwa hawana tabia ya kuuliza vitu yeye akishashiba ugali wake,mpe kichwa cha habari tu story nzima ataimaliza yeye.

Gari zote za serikali huja na namba za kiraia kupitia wizara ya ujenzi kisha namba hizo husajiliwa tena kwenye taasisi/wizara husika kwa namba husika.

Swala la kubadili namba limeruhusiwa kisheria endapo mhusika/mwenye cheo mfano mkuu wa mkoa hayumo ndani ya hyo gari hivyo dereva hutakiwa kubadili namba na kuweka namba iliyokuja na gari ama namba inayotambulika na ofisi.

Na pindi mhusika anapopanda plate namba yenye cheo chake huwekwa kwenye gari husika kutambulisha ni gari ambayo imembeba fulani.

Japo mfumo huo ni tofauti kidogo na jeshi au polisi ambako wao huwa hawaweki namba za kiraia bali za jeshi then mhusika anapopanda huwekwa initial kama nyota nk ili kutambulisha kwenye gari kuna fulani
Huo ni utaratibu huko kwenu tu TZ na umeanza lini? Wengine wazazi wetu walikuwa serikalini na hayo magari ndiyo yalikuwa yakitupeleka na kuturudisha mashuleni kila siku lakini hayakuwahi kuwa na numbers mbilimbili huu utaratibu mliouanzisha ni kwa malengo gani? Au ndiyo kutengeneza loopholes za watekaji na wauaji?
 
Pokeeni ushauri,acheni kuona ninyi ni vichwa,panapohitaji mabadiriko fanyeni mabadiriko.

Kwani magari ya serikali yakipokelewa yakapewa namba za serikali moja kwa moja kuna shida gani?
kama issue ni kutaka kujua nchi imeingiza au ina magari mangapi ni kuchukua idadi ya yanayomilikiwa na serikali ukaongeza uliyoyasajiri kwa namba za kawaida.
Ila kama ni ule mfumo wa mbuzi kula kwa kamba yake hapo nitaelewa,lakini kusema hili lipo kwa manufaa ya nchi nakataa mpaka kesho.
Huu wanaodai ndiyo utaratibu umeanza lini? Ni mambo wanayojifania kwa kuficha uovu wanaoufanya.
 
unatetea matumiz ya gari za serikali kutumika kwa maswala yao binafsi ,plate namba inapaswa kuwa moja na gari inapaswa kutojificha maana tunaamin popote ilipo kuna dhima ya kiutumishi na inapaswa kutambulika ili isiingiliwe kwenye majukumu yake , la sivyo watauliwa sana kama Tegeta
Sijamaanisha kutetea ndiyo maana nimekuuliza ungekuwa mshauri wa masuala ya usalama kwa viongozi wa nchi hasa wa kitaifa ungeruhusu jambo hili ama ungekataa?
Kwa upande mwingine, issue ya magari ya serikali kutumika na viongozi kwa masuala binafsi hilo lipo sanaa tuu. Inategemea na wadhifa alionao, ulishawahi kusikia Rais yupo likizo? Je ulishawahi kumuona akitumia magari yake binafsi aliyonunua kwa fedha zake? Je baadhi ya wastaafu pia huwa wanatumia magari binafsi?
Shida ipo kwa asiyestahili kuwa nalo baada ya muda wa kazi akakutwa nalo. Hapo ndiyo kuna shida kiongozi.
 
Elimu elimu elimu

Shida ya wabongo huwa hawana tabia ya kuuliza vitu yeye akishashiba ugali wake,mpe kichwa cha habari tu story nzima ataimaliza yeye.

Gari zote za serikali huja na namba za kiraia kupitia wizara ya ujenzi kisha namba hizo husajiliwa tena kwenye taasisi/wizara husika kwa namba husika.

Swala la kubadili namba limeruhusiwa kisheria endapo mhusika/mwenye cheo mfano mkuu wa mkoa hayumo ndani ya hyo gari hivyo dereva hutakiwa kubadili namba na kuweka namba iliyokuja na gari ama namba inayotambulika na ofisi.

Na pindi mhusika anapopanda plate namba yenye cheo chake huwekwa kwenye gari husika kutambulisha ni gari ambayo imembeba fulani.

Japo mfumo huo ni tofauti kidogo na jeshi au polisi ambako wao huwa hawaweki namba za kiraia bali za jeshi then mhusika anapopanda huwekwa initial kama nyota nk ili kutambulisha kwenye gari kuna fulani
Ninachofahamu gari mfano yenye namba W EL huwa ina namba zake STL au STK ambazo zinatumika boss asipojuwepo kwenye gari. Hii ya namba za kawaida BCD au EFG ndio nasikia leo.
Kwahio hizi LC300 zenye namba T...ABF au T...BGA ziliingia nchini lini?
 
Inawezekana kabisa unachosema Kiongozi ni sahihi, lakini pia tukumbuke mambo hubadilika hayabaki hivyo hivyo.
 
Huo ni utaratibu huko kwenu tu TZ na umeanza lini? Wengine wazazi wetu walikuwa serikalini na hayo magari ndiyo yalikuwa yakitupeleka na kuturudisha mashuleni kila siku lakini hayakuwahi kuwa na numbers mbilimbili huu utaratibu mliouanzisha ni kwa malengo gani? Au ndiyo kutengeneza loopholes za watekaji na wauaji?
Jaribu kutofautisha kupanda gari inayombeba baba/ukiwa kama abiria kwenda kazini na kupanda gari kama mtumishi
 
Ukija kujua gari hilohilo linawekwa bendera ya chama na kumsafirisha kiongozi wa chama si utalia 😅
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hichi kitu sio sahihi, ni uongo kwa 100%.
Kila gari (haijarishi ya binafsi, jeshi, serikali) huwa na usajiri wa namba moja tu katika wakati mmoja, gari moja haiwezi na haipaswi kuwa na namba mbili za usajiri kwa wakati mmoja.

Kama gari ilikuwa ya serikali halafu umiliki ukahamia binafsi, ile namba ya awali ya usajiri ya serikali hufa ili kuzaliwa namba mpya ya binafsi, na haitafufuka tena. Vice versa ni sawa.

Kinachoweza kubadilika katika gari za serikali ni vibao vya utambulisho ili kuficha vibao vya namba husika. Kwa mfano gari yoyote ya serikali inaweza kutolewa kibao cha namba ya asili (mfano STH 892) ili kuwekwa kibao chenye utambulisho wa ufupisho kwa viongozi wa juu mfano waziri, naibu waziri, makamu wa rais, waziri mkuu nk. Na wahusika wakiwa hawajabebwa kwenye hayo magari na hayo magari kwenda kutumika kwa shughuli zingine vibao vya utambulisho wa viongozi hung'olewa na namba halisi (asili) za serikali (STK, STJ, STH) kwa gari husika hurejeshwa. Lakini kamwe hauruhusiwi gari ya serikali kuwekwa namba binafsi. Ni uhalifu. Ni mchezo mchafu umeanza kuzoeleka katika jamii yetu. Haipaswi.
Naungana na wewe kwa asilimia mia. Unajua hawa jamaa wanatoa majibu yao uchwara humu wanafikiri huko serikalini wanafanya kazi wenyewe na hakuna watu wengine wenye uelewa zaidi yao.
 
Back
Top Bottom