Kwanini Serikali inaendelea kutoa kauli zinazoacha tafsiri mchanganyiko kwa wananchi?

Kwanini Serikali inaendelea kutoa kauli zinazoacha tafsiri mchanganyiko kwa wananchi?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Mchana wa October 29, Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama vilitoa kauli kwamba ikifika saa 12 watu wawe ndani. Kauli ile kwanza haikutangazwa kwa juhudi za kutosha ili ziwafikie watu wengi. Pia kwa makusudi iliacha mapengo ya tafsiri yanayokuja baadae kuleta utata wa kisheria.

Mfano, hawakusema ikifika saa 12 ya jioni au ya muda gani. Hawakusema pia lile katazo lilikuwa linaenda hadi muda gani.

Matokeo yake, asubuhi, watu walidhani katazo limekwisha au wanatakiwa kurudi ndani ikifika jioni ya saa 12, kumbe hata ile asubuhi na mchana wa October 30 lile katazo lilikuwa bado valid. Watu wakatandikwa shaba kama kuku.

Leo tena nimetoka kuona taarifa ya serikali ikitolewa na Mwigulu. Taarifa hii inatumia lugha laini lakini ni kama katazo pia la watu kutoka nje. Kesho utashangaa watu wanapigwa shaba vile vile kwa kukaa tu vibarazani mwao au kwa kwenda kujitafutia riziki.

Kwa nini serikali imeamua kutoongea lugha ya moja kwa moja kwa wananchi wake? Hizi lugha za mafumbo kwa ajili ya kujiwekea kinga, mwisho wa siku ndiyo zinaleta sintofahamu maana wananchi hawapati maelekezo yaliyonyooka.
 
Mchana wa October 29, Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama vilitoa kauli kwamba ikifika saa 12 watu wawe ndani. Kauli ile kwanza haikutangazwa kwa juhudi za kutosha ili ziwafikie watu wengi. Pia kwa makusudi iliacha mapengo ya tafsiri yanayokuja baadae kuleta utata wa kisheria.
Mfano, hawakusema ikifika saa 12 ya jioni au ya muda gani. Hawakusema pia lile katazo lilikuwa linaenda hadi muda gani. Matokeo yake, asubuhi, watu walidhani katazo limekwisha au wanatakiwa kurudi ndani ikifika jioni ya saa 12, kumbe hata ile asubuhi na mchana wa October 30 lile katazo lilikuwa bado valid. Watu wakatandikwa shaba kama kuku.
Hii ilikuwa hatari sana, tarehe 30 mimi nilitoka naenda masjid nikijua saa 12 ishapita nafika road nakutana na risasi, ningerudisha namba siku ile huenda hata mwili usingerudi, iko haja hata kama ni kuendeshwa kihuni maelezo yawe yananyooka! vinginevyo tutaisha sana.
 
Hata askari wanatamani yaendeleee. Wanapiga sana hela.

Ulinzi binafsi kwenye ofisi za watu na posho za chungu kikuu.

Mimi mwenyewe natani maamdamano yaendelee, Nimependa ulinzi Serikali imeamua kutupatia tukiwa barabarani na matembezi

Huu ulinzi alikua anapewa Samuya pekee sasa na sisi walala hoi serikali imetulumbuka
 
Kumbe hawa askari walikuwa hawafanyi kazi. Hii nchi tunaweza kuishi bila ujambazi wala vibaka.

Hili zoezi liwe endelevu. Trafiki hawana maana barabarani. Maisha yanaenda tena kwa amani kbs
 
Hii ilikuwa hatari sana, tarehe 30 mimi nilitoka naenda masjid nikijua saa 12 ishapita nafika road nakutana na risasi, ningerudisha namba siku ile huenda hata mwili usingerudi, iko haja hata kama ni kuendeshwa kihuni maelezo yawe yananyooka! vinginevyo tutaisha sana.
Wanatoa taarifa zenye ukakasi kwa makusudi. Leo wanasema wanatoa ushauri watu wakae ndani lakini ni amri. Hawataki kuonekana wametoa amri ya watu kukaa ndani ila wanataka wapate faida za watu kukaa ndani.
 
Kwahiyo mnawalazimisha wafanya biashara wafunge biashara zao? Wenye viwanda wafunge viwanda vyao? Na madereva wa magari waache kazi zao za kujitafutia riziki?
Biashara gani tena au maduka mlioenda kuvunja?
Viwanda gani tena au vile mlivyoenda kuvamia kama kule mwanza mkaungua kama kuku wa kukaanga?
Magari gan tena ambayo mlichoma na kuharibu hadi na vituo vya mafuta?
 
Hii ilikuwa hatari sana, tarehe 30 mimi nilitoka naenda masjid nikijua saa 12 ishapita nafika road nakutana na risasi, ningerudisha namba siku ile huenda hata mwili usingerudi, iko haja hata kama ni kuendeshwa kihuni maelezo yawe yananyooka! vinginevyo tutaisha sana.
Kukaja kusikika hadi Ijumaa watu waswalie nyumbani, kuna wazee walidhani utani wanaenda msikitini ile ijumaa wakazuiwa na polisi ikabidi wakarudi nyumbani.
 
Umeongea kitu cha msingi Sana.
Ilibaki kidogo nisababishe family member wangu mmoja auwawe siku ya 30/10.
Nilimpigia simu jioni ya 29/10 kuwa kesho asubuhi awahi akaongeze stock ya mahitaji muhimu.
Bahati nzuri aliwasiliana na watu wengine wakamjulisha asithubutu kwenda central business area ya mtaani.
Na kweli, walipoenda kununua vitu siku hiyo asubuhi walipigwa shaba bila kuulizwa au kupewa onyo.
Jamaa waliua kikatili sana. Ni kwamba vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa ktk fighting mode kama kwenye war front line. Huku wananchi walikuwa wali relax, wapo at easy wakichukulia maandamano yameisha tarehe 29/10 hawana mpango tena wa kuandamana.
Nadhani kulikuwa na mawasiliano mabaya au hafifu miongoni mwa majeshi, usalama wa taifa na viongozi wa juu wa serikali. Kuna delay ya kutathimini situation on the ground na kipi kifanyike kupunguza civilian casualties.
Poor planning on military and intelligence services na executive leaders.
 
Umeongea kitu cha msingi Sana.
Ilibaki kidogo nisababishe family member wangu mmoja auwawe siku ya 30/10.
Nikimpigia simu jioni ya 29/10 kuwa kesho asubuhi awahi akaongeze stock ya mahitaji muhimu.
Bahati nzuri aliwasiliana na watu wengine wakamjulisha asithubutu kwenda central business area ya mtaani.
Na kweli, walipoenda kununua vitu siku hiyo asubuhi walipigwa shaba bila kuulizwa au kupewa onyo.
Jamaa waliua kikatili sana. Ni kwamba walikuwa ktk fighting mode kama kwenye war front line. Huku wananchi wakichukulia maandamano yameisha tarehe 29/10 hawana mpango Tena was kuandamana.
Nadhani kulikuwa na mawasiliano mabaya au hafifu miongoni mwa majeshi, usalama wa taifa na viongozi wa juu wa serikali. Kuna delay ya kutathimini situation on the ground na kipi kifanyike kupunguza civilian casualties.
Poor planning on military and intelligence services na executive leaders.
Walitoa taarifa ile kimkakati wakiwaza mbele ili siku moja wakifikishwa mahakamani waseme taarifa ya kukaa ndani ilitolewa kwenye vyombo vya habari na wale waliotoka nje walikaidi amri hiyo.
 
Back
Top Bottom