Kwanini Serikali inaendelea kutoa kauli zinazoacha tafsiri mchanganyiko kwa wananchi?

Wewe umeelewaje?
Siyo suala la kuelewa ni suala la kauli iliyotamkwa na vile wao watakavyoitekeleza ni vitu viwili tofauti. Unapotoa ushauri, mtu ana uhuru wa kukataa au kukubali ushauri wako.

Serikali makini inajua tofauti ya Ushauri na Amri.
 
Yenyewe imechanganyikiwa
 
 
Halafu risasi zilivyokuwa zinapigwa hakuna kuulizwa dini wala kabila lako, ila kuna wapuuzi wanataka kugawa watu kidini. Au Shekh uliona risasi zilikuwa na msamaha kwa kundi maalumu?
 
Biashara gani tena au maduka mlioenda kuvunja?
Viwanda gani tena au vile mlivyoenda kuvamia kama kule mwanza mkaungua kama kuku wa kukaanga?
Magari gan tena ambayo mlichoma na kuharibu hadi na vituo vya mafuta?
Babu tulia kunywa maji :bila bi msumi kuondoka na kuiacha familia ya kikala, moto utafuka na Tanganyika huru na kumbwa tutaijenga tena.uhai wa binadamu unathamani kuliko mavitu
 
Ni kwamba kesho watu wote mnapaswa kukaa ndani majumbani kwenu, hakuna kutoka nje...
Ni wale tu wenye ulazima wa kufanya hivyo tena kwa kupangiwa na viongozi wao...
Kwa tamko hilo kiongozi gani wa kawaida anaweza kumpangia mfanyakazi wake aende kazini kesho wakati ni siku ya mapumziko... zaidi ya polisi, wanajeshi, Tanesco na madaktari...


Cc: Mahondaw
 
Kwa hiyo wenye haki ya kufanya kazi ni waajiriwa tu. Waliojiajiri je? Yale ya MO29 yamejirudia.

Unawaambia watu wafanyie kazi nyumbani utadhani wote shughuli zao zinaruhusu hivyo. Hapo hapo umekata mtandao. Hapo hapo mwenye duka, genge au anayeshona nyumbani kwake hawezi fanya kazi maana wateja wake wameambiwa wasitoke ndani na hata yeye akikaa kibarazani ashone anapigwa shaba.

Ingetosha kusema hiyo ni AMRI ya kutotoka ndani badala ya kusema ni USHAURI. Waepuke kutumia lugha za hadaa katika nyakati za hatari.
 
Technically mmefokewa hakuna kutoka nje...
 
Tarehe 30 October nimetoka nyumbani kuwahi boat ya kwanza nivuke niende Zanzibar, nafika Tegeta nakutana na barrier kali ya wanajeshi, kistaarabu Wakanimbia nirudi nyumbani, njiani nilikutana na maiti tatu. Wakati narudi nikawaza sana kama ningekutana na wale wavaa nguo za kaniki ingekuaje. Maana nilikuwa na bodaboda.

So ni heri wakasema tu kwa uwazi kesho hakuna mtu kutoka nje.
 
Walitoa taarifa ile kimkakati wakiwaza mbele ili siku moja wakifikishwa mahakamani waseme taarifa ya kukaa ndani ilitolewa kwenye vyombo vya habari na wale waliotoka nje walikaidi amri hiyo.
Bado adhabu ya kukiuka amri ile siyo capital punishment or death sentence.
Hawawezi kuchomoka.
Kwanini wasiwakamate au wasiwapige risasi za miguuni?
Watu walilengwa vichwa tena wakiwa hawana silaha wala Mwenge wa kuchoma vitu.
Wengine wakiwa kwenye geti au ndani ya nyumba au vibarazani.
Muda lilipo toka tangazo na kuanza utekelezaji ni mfupi.
Wengine walikuwa mbali na makazi yao na wengine safarini.
Kwa mfano mtu kapiga kura kapanda basi anaenda mbali. Tangazo limetolewa akiwa njiani akifika 12:30 jioni atafanyeje?
Hana pesa ya kukaa guesthouse na ya chakula kwa siku 3 angefanyeje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…