Kwanini serikali isiwachukue hawa vichaa wanaozagaa mitaani na kuwaweka kwenye makempu kwa ajili ya kuwahudumia na kuwatibia

Una hoja mkuu usipuuzwe.
Itawasaidia sana wenye matatizo.
Itatoa ajira kwa wahudumu na kukuza uchumi.
 
Umeongea vyema mkuu makundi haya ni madogo kwa idadi hasa hawa vichaa na machizi, wangetenga bajeti ya kuwasaidia hawa watu kwa kuweka vituo vya huduma ya chakula na dawa wangesaidika sana

Nimetoa mfano wa kituo cha wagonjwa wa akili kule lutindi wilayani lushoto hakika vituo kama vile vingekuwepo vya serikali kila mkoa vituo kadhaa vingesaidia sana kupunguza au kuondoa hawa vichaa mtaani

Kichaa hana mtetezi, ndugu wakishamtelekeza au kushindwa matibabu anachongoja ni kifo hamna kingine naandika haya machozi yakinitoka Mungu awasaidie hawa watu hakika wanateseka sana
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Miaka ya nyuma kulikuwa na wodi ya vichaa katika kila hospitali ya wilaya na mkoa, siku hizi hatuoni vichaa mahospitalini
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…wote tuko mtaani kila mtu anachanganyikiwa kivyake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…