Kwanini serikali isiwachukue hawa vichaa wanaozagaa mitaani na kuwaweka kwenye makempu kwa ajili ya kuwahudumia na kuwatibia

Kwanini serikali isiwachukue hawa vichaa wanaozagaa mitaani na kuwaweka kwenye makempu kwa ajili ya kuwahudumia na kuwatibia

Una hoja mkuu usipuuzwe.
Itawasaidia sana wenye matatizo.
Itatoa ajira kwa wahudumu na kukuza uchumi.
 
Sijui Wizara ya Jinsia na Mandeleo ya Jamii inafanyaga kazi gani?
Maana hili lilipaswa kuwa moja ya majukumu yake. Hakukupaswa kuwa na wagonjwa wa akili mtaani, wala wazee, wala ombaomba wala watoto wa mtaani.
Wote wanapaswa kukusanywa na kuwekwa mahali pa kuishi.
Wale ambao wanaweza kufanya kazi, wafanye huku wakiwa hapo hapo kambini kama wakiamua kuwaweka kambini
Umeongea vyema mkuu makundi haya ni madogo kwa idadi hasa hawa vichaa na machizi, wangetenga bajeti ya kuwasaidia hawa watu kwa kuweka vituo vya huduma ya chakula na dawa wangesaidika sana

Nimetoa mfano wa kituo cha wagonjwa wa akili kule lutindi wilayani lushoto hakika vituo kama vile vingekuwepo vya serikali kila mkoa vituo kadhaa vingesaidia sana kupunguza au kuondoa hawa vichaa mtaani

Kichaa hana mtetezi, ndugu wakishamtelekeza au kushindwa matibabu anachongoja ni kifo hamna kingine naandika haya machozi yakinitoka Mungu awasaidie hawa watu hakika wanateseka sana
 
Hujambo? Heri ya Mwaka mpya.

Watu wengi bado wanazichanganya Wizara mbalimbali na Makundi yake maalumu. Haya maoni mazuri humu mngewasilisha moja kwa moja kwenye Wizara mahsusi ya kundi la watu wenye ulemavu ambayo inaitwa, Wizara ya Kazi Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu, Iko ofisi ya Waziri Mkuu. Hivyo, maoni haya mazuri yangejumuishwa kwenye mikakati rasmi ya masuala ya wenye ulemavu kwenye Wizara hii mahsusi tafadhali.

Ahsante Sana
🙏🙏🙏
 
Miaka ya nyuma kulikuwa na wodi ya vichaa katika kila hospitali ya wilaya na mkoa, siku hizi hatuoni vichaa mahospitalini
😅😅😅wote tuko mtaani kila mtu anachanganyikiwa kivyake
 
Back
Top Bottom