Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Wakati Serikali ikitangaza kuwepo kwa mpango wa kuwatambua waandishi wa habari wakongwe ambao hawakusomea uandishi wa habari kwa ngazi ya stashahada, swali linalogonga vichwa ni kwa nini Serikali ndiyo iwe mwamuzi wa nani awe mwandishi wa habari na nani asiwe?
Hivi karibuni, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuandaa mpango maalumu utakaolenga kuwawezesha waandishi wa habari wakongwe ambao, kwa sababu moja au nyingine, wamekosa sifa za kuwa na ithibati ya kuwa waandishi wa habari.
Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Sheria yetu ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sura namba 229.
"Hiyo ni moja ya programu ambazo tunakusudia kuzifanya katika mwaka 2025, 2026, na 2027. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri, Paul Christian Makonda, alisema katika uwasilishaji wa bajeti, Bodi ya Ithibati inakamilisha mwongozo ambao tunatarajia uanze kutumika mwezi Julai mwaka huu,” alisema.
Soma zaidi: Serikali inaandaa mpango wa kuwarejesha kazini waandishi wakongwe waliokosa vigezo vya ithibati. Kwanini baada ya Uchaguzi?
Akizungumzia suala hilo, mhariri wa The Chanzo, Khalifa Said anasema hatua hiyo inadhihirisha upungufu uliomo kwenye Sheria ya Huduma za Habari ya 2016.
“Serikali inaazisha Sheria ya Huduma za Habari haikufanya utafiti wa kutosha kujua kwamba inakwenda kutatua shida gani. Hiyo shida au kasoro ndiyo inafanyiwa utafiti wa kisayansi. Wao waliona tu waandishi wa habari wasio na stashahada ya uandishi ndio wanakiuka maadili, sasa leo wanakuja tena wanasema kuna waandishi wakongwe, huko ni kukiuka sharia waliyoitengeneza wenyewe,” amesema.
Kuhusu mwongozo unaoandaliwa, Khalifa anasema unapaswa kuendana na sharia, vinginevyo utakuwa ni mkanganyiko wa kisheria.
“Kwenye sharia kuna ngazi nne, kwanza kuna Katiba, halafu sharia halafu kanuni kisha mwongozo, hivyo huo mwongozi unapaswa kufuate huo mtiririko, vinginevyo utakuwa mkanganyikao. Halafu huo mwongozo utaweka kigezo gani cha mwandishi mkongwe? Amefanya miaka mingapi? Amefanya kazi nchi ngapi? Nini sifa ya kuwa mkongwe?”
Kwa mujibu wa Khalifa, sharia hiyo ni mwendelezo wa ukandamizaji wa Serikali ili kukwepa ukosoaji kutoka kwa wananchi.
“Sio waandishi wa habari tu, kuna vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini. Lakini kwa nini Serikali ndiyo ituamulie kwamba nani ndiye mwandishi wa habari na nani asiwe? Kwa nini Serikali haiamui nani ni mhandisi au mwanasheria au mfamasia? Ni kwa sababu wana bodi zao za kitaaluma zenye mamlaka hayo.
“Ilitakiwa tuwe na Sheria ya Baraza la Habari la Tanzania na hiyo itaweka vigezo vya nani ni mwandishi, sio hii sharia inayoipa mamlaka Serikali kutuamulia,” amesema.
Hata hivyo, mwandishi mkongwe, Manyerere Jackton anasema kuna namna Sheria ya Huduma za Habari na kanuni zake vinatambua waandishi wakongwe ambao hawakupata elimu ya uandishi kwa ngazi ya stashahada.
“Nadhani hiki sio kitu kipya, kuna namna sharia hii inawatambua waandishi wa habari wakongwe, lakini sio kwa kuwaita tu na kuwapa ithibati, nadhani watashirikiana na Wizara ya Elimu kutoa mafunzo hata ya miezi mitatu, ndiyo wapewe ithibati,” anasema.
Manyerere anakiri kuwepo kwa ukandamizwaji wa vyombo vya habari, akisema ndio kawaida ya Serikali nyingi duniani.
“Ukiangalia kila sharia inatoa uhuru huku, lakini inauondoa tena upande mwingine. Tunasikia pia waandishi wa habari waliokosa ithibati waliondolewa muda mfupi kabla ya uchaguzi na sasa uchaguzi umeisha ndiyo wanafikiria kuwarudisha, hiyo inawezekana nakubaliana kwamba kuna mambo ya kisiasa tu,” anasema.