TaiPei
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 572
- 608
Mbunge wa Jimbo la Kisesa CCM Mhe Luhaga Joelson Mpina kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akiishambulia vikali kwa hoja nzito nzito Serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan lakini mamlaka husika ziko kimya kabisa.
Tujaribu kufikiria kama Wananchi wataamua kuchukua hoja za Mhe Luhaga Mpina kama zilivyo basi CCM itakuwa imepoteza Ufuasi wa kiwango cha Juu sana kwenye medani za siasa hasa Ukanda wa maziwa maku ya Victoria na Tanganyika.
Huenda nikashindwa kuandika sawa sawa ila itoshe tu kusema Wateule msaidieni Rais kujibu hizi hoja nzito za Mhe Luhaga Mpina tena kwa wakati ukweli ni kwamba huku mtaani hali sio nzuri sana kwa Upande wetu hivyo hatuna haja ya kujiamini kiasi hiki cha kumpuuza mtu mwenye hadhi ya Ubunge tena toka Chama tawala.
Nashauri kila mmoja amjibu Mhe Luhaga Mpina Kwakuwa Uongo hauhitaji Itifaki kuukabili, Mpina ajibiwe na Balozi wa nyumba kumi, ajibiwe na diwani au Mbunge aijibiwe na kila mmoja mwenye majibu sahihi kwani kukaa kimya ni kumaanisha hoja za Mpina ni za kweli na ni ukweli tupu.
Pia soma
- Pre GE2025 - Luhaga Mpina: Baadhi ya Viongozi wa Serikali wanahusika kutorosha fedha
- Luhaga Mpina: Wanaomsifia Rais Samia ndio hao wanaoongoza kwa kumhujumu na kufanya uovu