Kwanini Serikali ya Rais Samia inashambuliwa na Luhaga Mpina na Waziri wa kisekta, Msemaji na Katibu Mkuu wapo kimya?

TaiPei

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2022
Posts
572
Reaction score
608
Mbunge wa Jimbo la Kisesa CCM Mhe Luhaga Joelson Mpina kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akiishambulia vikali kwa hoja nzito nzito Serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan lakini mamlaka husika ziko kimya kabisa.

Tujaribu kufikiria kama Wananchi wataamua kuchukua hoja za Mhe Luhaga Mpina kama zilivyo basi CCM itakuwa imepoteza Ufuasi wa kiwango cha Juu sana kwenye medani za siasa hasa Ukanda wa maziwa maku ya Victoria na Tanganyika.

Huenda nikashindwa kuandika sawa sawa ila itoshe tu kusema Wateule msaidieni Rais kujibu hizi hoja nzito za Mhe Luhaga Mpina tena kwa wakati ukweli ni kwamba huku mtaani hali sio nzuri sana kwa Upande wetu hivyo hatuna haja ya kujiamini kiasi hiki cha kumpuuza mtu mwenye hadhi ya Ubunge tena toka Chama tawala.

Nashauri kila mmoja amjibu Mhe Luhaga Mpina Kwakuwa Uongo hauhitaji Itifaki kuukabili, Mpina ajibiwe na Balozi wa nyumba kumi, ajibiwe na diwani au Mbunge aijibiwe na kila mmoja mwenye majibu sahihi kwani kukaa kimya ni kumaanisha hoja za Mpina ni za kweli na ni ukweli tupu.

Pia soma
- Pre GE2025 - Luhaga Mpina: Baadhi ya Viongozi wa Serikali wanahusika kutorosha fedha

- Luhaga Mpina: Wanaomsifia Rais Samia ndio hao wanaoongoza kwa kumhujumu na kufanya uovu
 
 
Wewe unahisi LUHAGA MPINA ni kuwaita vyombo vya habari nakuongea uzushi?

Ingekua hivo basi wangekua wameshamjibu.

Kumjibu MPINA kama sio msomaji na mfatiliaji , ukaja kubwabwaja kama Akina Kibajaji utaonekana Fala tu.

Hivo hao watu wako pengine wanapitia Kila kitu alichokisema MPINA ndo wake wamjibu
 
Sasa ndio ujibu swali kwanini hajibiwi?
 
Niliona kafulila akimjibu kama sikosei
 
Kapuuzwa
 
Unajibuje vioja vya mtu aliyechanganyikiwa kwa mfano? Waangalie kina Medard Kalemani wametulia, yule mshamba wa kisukuma amewehuka baada ya kukosa uwaziri. Kwl ni jinga. Vile ni vioja hakuna hoja pale ndio maana amepuuzwa tu. Ht mahakamani wsmefuta vikesi vyake vile vyote. Anajiaibisha anafanya mambo ya kitoto
 
Tatizo Wananchi hawana akili kama hizi zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…