Kwanini serikali ya Tanzania inalazimisha lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe Kiswahili?

Kwanini serikali ya Tanzania inalazimisha lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe Kiswahili?

Nadhani wanafanya hivyo kwasababu kuepuka kuonekana sio wazalendo na lugha yao "hapo ndipo wanazidi kupeleka taifa katika shimo.
 
Tunafahamu kwamba mnalazimisha watu wasome Kwa kiswahili ili muendelee na biashara zenu za shule za private English medium school.

Huko hakuna mtaji mnaotegemea zaidi ya kingereza Kwa masomo yote.
Kuweka lugha ya English kwenye shule za kayumba ndy utakuwa mwisho wa shule zenu.

Shame on you..
-Mnalazimisha watu wasome Kwa kiswahili wakati Sheria zote za inchi zipo Kwa English.
 
Nchi zote zizoliwahi kutawaliwa na mwingereza zinafundisha kingereza katika mashule yao kwanzia msingi.wakimaliza shule wanakuwa na wigo mpana wa kuajiriwa katika makampuni ya kigeni kuliko sisi.Aidha nchi hizo zinaonyesha ufanisi katika michezo hasa mpira wa miguu kwa sababu wanapoajiri kocha wa kigeni mawasiliano yanakuwa mepesi.Lakini vilele kiuchumi mikataba ya biashara na madini haiwalalii sana kwa kutokujua lugha kama kwetu.Naweza kusema kutokuweka kipaumbere katika kufundisha lugha ya kiingereza hapa kwetu ni janga katika utandawazi wa sasa,
 
Hili swali Huwa najiuliza sana alafu sipati majibu
Hivi ni kweli hawa viongozi wa serikali hawajui magumu wanayopitia watoto pale wanapoingia kidato Cha kwanza na kukuta lugha imebadirika ghafla?

Hivi ni kweli hawa viongozi wa serikali hawajui umuhimu wa lugha ya kingereza ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu ?

Hivi ni kweli hawaoni tofauti kati ya mtoto aliyetumia lugha ya kiswahili darasa la kwanza Hadi darasa la saba na mtoto aliyesoma English medium pale watoto hawa wanapokutana kidato Cha kwanza?

Kwani mawaziri. Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wakurugenzi mbali mbali wanawasomesha watoto wao EM badala ya Kayamba wakati wao ndio waliotunga na kuisimamia sera ya kuwa kiswahili ndio iwe lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi ?

Hapa Kuna Siri iliyokificha nyuma ya pazia watanzania amkeni

Kwa sababu nakumbuka kipindi hakuna EM za private serikali walikuwa na za kwao Kwa hapa Dar ni Olympiyo na Bunge na kipindi hicho asilimia 90 ya waliosoma hizi shule walikuwa ni watoto wa mawaziri na viongizi wengine

Kwahiyo sio kama hawajui umuhimu wa lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe kingereza ila tu wanawapumbaza watanzania walio wenge kuwa eti watoto wao kutumia kiswahili shule za awali na msingi ndio kudumisha uzalendo
Haitaki wafanane na watoto wao, wanatengeneza tabaka tawaliwa
 
Una hoja kubwa.
USIPUUZWE.
 
Jiulize wachina wanatima kichina warisi kirusi wajerumani warussia usiwe mtumwa wa lugha ya kikoloni
Dawa
Maelekezo barabarani
Kompyuta
Magari
Mamlaka za kodi
Mashine na mitambo mbalimbali
Viwandani
Kote kunatumika lugha gani?
Kuendana na dunia siyo ukoloni na ushamba.
Huna uwezo wa kutengeneza mfumo hata mmoja halafu unasema unajiweza? Hii ni kuzalisha wajinga wengi usikute na ww ni zao la wajinga waliozalishwa ili utwana usiishe.
 
Naunga mkono hoja kiiingereza kifundishwe kama lugha ila masomo mengine yote yawe kwa kiswahili hakuna haja ya kuhangaika ku kariri mavitu yasiyo na manufaa baadaye asian tigers wameendelea sana hakuna hata mmoja nayeabudu viingereza
 
Kinge kinamata aisee japo s'ytms ni ngumu kumwelezea mtu akakuelewa ila kinamata sana aisee tena hata ktk maisha ya kawaida tu.
 
Ninakumbuka nilipokwenda form one nilipata shida sana.
wewe kama mimi aisee. tumetoka kayumba kufika seco na viswahili vyetu bana tumeķuta kuna maticha akìingia class ni full kinge mwanzo mwisho. tulikuwa tunatoka kapa. tuliishia kuwachukia sana wale walimu.
 
Serikali inawafuga mkuu, halafu hakuna walimu wa hicho kinge ndio maana watu wanapeleka kwenye ma bus ya njano. Kabla ya kutaka hao walimu wafundishe kizungu walitakiwa wawandae kwa kuwapa maarifa ya kufundisha hao wanafinzi anyetaka hicho kiswahili kiwe lugha ya kufundishia yeye wanae wanasoma kwingine na lugha ingine.
 
Ukifuatilia sana hapa ungundua aina ya walimu wanaofundisha hayo madarasa ndyo chanzo Cha matumizi ya kiswahili
 
Ninakumbuka nilipokwenda form one nilipata shida sana. anyway hapa mwalimu alikosea sana. Hii pia imesababisha kuwa na diaspora wachache sana ukilinganisha na nchi kama Kenya, Zimbabwe na ziginezo. Inakuwa ngumu sana tunapokuwa nje kuzungumza kiingereza fasha.
Na ndio maana walimu wa lugha ya kiswahili wanaofundisha nchi za Ulaya na Asia 90% ni wakenya

Wakati sisi watanzania ndio tunajua kiswahili fasaha ila tunaonekana hatuji hata lugha yetu wenyewe ya kiswahili Kwa sababu hatujui kingereza

Yani watanzania ni sawa wamefungwa mikono alafu wanaambiwa wapigane na ambao hawajafungwa mikono

Na mbaya zaidi waliotufunga hiyo mikono ni viongozi wetu Kwa makusudi kabisa
 
Kwanini ID yako unajiita Francis badala ya kichogo? au mbulumundu?
Kama kwl wewe hutaki utumwa Kwa watu weupe..
Kujifunza English ni muhimu Sn Kwa dunia ya Sasa.
Nimepewa hilo jina.., sio rahisi kulibadilisha. Ila lugha ni yetu, na tutaendelea kuifumisha..
 
Nakubaliana na wewe kingereza kitiliwe mkazo hili isiwe lugha ya maajabu kama ilivyo Sasa...

Leo hii ukipigiwa simu kwenye daladala halafu ukapokea kisha ukaanza kuongeza kingereza watu wanakushangaa sana, Sasa hii Hali tuifute.

Ila hapo unaposema eti hili tuendelee tunahitaji kingereza huko ni kujidanganya, maana hata Sasa hivi tumezungukwa na nchi ambazo kingereza ni lugha wanayotumia mara Kwa mara lakini Bado ni maskini zaidi yetu.. i.e Zambia na Uganda
 
Muzei Nyerere aliwahigi kusema "Umasikini wa Fikra" ndio Umasikini mukubwa.

Mwenye ana fikra za kutawaliwa na Lugha za mzungu ni "Masikini" wa fikra.

Ni Umasikini wa Fikra huu

#bigot
 
Nakubaliana na wewe kingereza kitiliwe mkazo hili isiwe lugha ya maajabu kama ilivyo Sasa...

Leo hii ukipigiwa simu kwenye daladala halafu ukapokea kisha ukaanza kuongeza kingereza watu wanakushangaa sana, Sasa hii Hali tuifute.

Ila hapo unaposema eti hili tuendelee tunahitaji kingereza huko ni kujidanganya, maana hata Sasa hivi tumezungukwa na nchi ambazo kingereza ni lugha wanayotumia mara Kwa mara lakini Bado ni maskini zaidi yetu.. i.e Zambia na Uganda
Hizo nchi zimeendekea kuliko sisi Tanzania kinachotubeba ni bandari tu

Kama ingekuwa inawezekana sisi watanzania na serikali yetu tungehamia Uganda alafu wao waganda na serikali yao wahamemie aridhi ya Tanzania amini usiamini wangetiacha mbali sana
 
Back
Top Bottom