Kwanini shule za kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa?

Kwanini shule za kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa?

1.Shule za kiislam na maeneo yenye waislam wengi hua wanafeli sana form 4 au 6,......Kama pale Zanzibar,ila uchumi wa Zanzibar ni mara 10 ya uchumk WA Kilimanjaro ama Zanzibar penye wakristo wengi😃😁😆😆
2.Samia Suluhu Rais wa Tanzania,alipata division zero form six😁😁,ila anawatawala vipanga wakina Mwigulu na professor Kabudi
3.ukienda mijini,kariakoo pale,utakutana na wauza maduka wengi waislam wameajiari wanapiga mishe zao,huku wakuja wakiahangaika na bahasha kuomba ajira
Life is the Game
Kwa hoja yako hii basi Pemba na Unguja yangekuwa ni maeneo yenye GDP kubwa zaidi Tanzania. Ila uko kuna wilaya zinaingia top 5 ya wilaya zisizo na vyoo Tanzania, wanaongoza kwa kunya vichakani.
 
Anna tibaijuka anayo majibu ya kutosha juu ya swali lako. Fuatilia ili ujue wale wanaoteuliwa kusahihisha mitihani, pamoja na maagizo wanayopewa
Ingawa itakuwa NI ngumu kumeza, lkn kuna kitu utaking'amua
Hayo majibu Ana Tibaijuka hana. Hakuna mahala popote amehusisha ufaulu wa mwanafunzi na dini yake.
 
Tofautisha Uisilamu na Bakwata, Shule ambazo hazifanyi vizuri ni za waisilamu ama ni za Bakwata?

Ukitoa Shule za Bakwata una data zozote kuonesha Shule za Kiisilamu hazifanyi Vizuri?

Kuanzia Feza, Aga Khan, Good Samaritan, Burhan, Istiqama na nyengine kibao zinafanya vizuri tu.
Mkuu ninachojua Feza sio shule ya Kiislamu hata kama inamilikiwa na Waturuki ambao almost wote ni Waislamu. Ni sawa na useme Tusiime au Kaizilege ni za Wakristu kisa dini za wamiliki.

Aga Khan ni taasisi ya Kiislamu ya kimataifa hivyo katika kujibu changamoto yetu bado haiwi mfano mzuri.
Hizo nyingine naamini ndio za kwetu wabongo wenyewe.

Hapa nchini tuna Al Muntazir ni International School ya Kiislamu, sijajua kama kuna International School ya Kikristo.

Shule za BAKWATA nazo ni za Waislamu, hakuna sister wa kanisa au padre anaziongoza. BAKWATA sio Walutheri wala walokole.
 
Nina experience na shule moja ya kiislam maarufu sana mkoa niliopo, kuna siku kulikuwa na tamasha la wanafunzi ambapo sisi tulikuwa wadhamini. Ilikuwepo na shule ya Baptist na shule zingine. Aisee wale wasichana wa shule ya kiislam pamoja na kuvaa hijabu lakini walikuwa hawana hofu ya kufanya vitu vya ajabu mbele ya wazazi. Wamezoeana na walimu kupita kawaida, wanakumbatiana na walimu mpaka tukabaki kushangaa. Muziki ukipigwa wanakatika mpaka wanalala chini kama wacheza shoo. Wale wa baptist walikuwa completely opposite. Hata kama walificha makucha lakini utofauti ulikuwa mkubwa sana. Kwa kile nilichokuona, division four is inevitable 😭😭😭
 
Anna tibaijuka anayo majibu ya kutosha juu ya swali lako. Fuatilia ili ujue wale wanaoteuliwa kusahihisha mitihani, pamoja na maagizo wanayopewa
Ingawa itakuwa NI ngumu kumeza, lkn kuna kitu utaking'amua
Hakuna unachofahamu kuhusu usahihishaji wa mitihani. Hakuna kisicho haki kitatendeka baada ya mtihani. Kwa jii post yako inaonyesha haupo kwenyw mfumo wa elimu kwa sasa hauna unachofahamu. Ficha ujinga wako.
 
Ukifa ndio utaongea vizuri, hiyo elimu yako ya dunia itakua haina nafasi wala maana baada ya kufa kwako
Umelishwa matango pori ukayameza mazima mazima, ukifa ndiyo imetoka hiyo.
Eti ukifa ndiyo utaongea vizuri, maiti haiongei ustaadh, ingekuwa kuna mtu ameshawahi kwenda huko unakokuita ahera na akarudi na ushahidi usiotia shaka hapo ingeeleweka lakini si hizi hadithi hizi za Pwagu na Pwaguzi zilizoletwa na Waarabu/Wazungu kwa ajili ya kupumbaza watu ili wafanikishe mambo yao bila vikwazo.
 
Elimu ya duniani tupo nyuma na ndio muhimu kwa maisha ya kawaida ya duniani
ٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا لَعِبٌۭ وَلَهْوٌۭ وَزِينَةٌۭ وَتَفَاخُرٌۢ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌۭ فِى ٱلْأَمْوَٰلِ وَٱلْأَوْلَـٰدِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ ٱلْكُفَّارَ نَبَاتُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصْفَرًّۭا ثُمَّ يَكُونُ حُطَـٰمًۭا ۖ وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌۭ شَدِيدٌۭ وَمَغْفِرَةٌۭ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنٌۭ ۚ وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا مَتَـٰعُ ٱلْغُرُورِ ٢٠
 
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2024 yanaonesha tena kwamba shule za Kanisa Katoliki zimeendelea kuongoza kwa viwango vya juu vya ufaulu. Kwa mfano, kati ya watahiniwa 19,182 waliotoka kwenye shule za Kanisa, asilimia 97.72 walipata daraja la kwanza hadi la tatu, huku asilimia 0.04 pekee wakipata daraja la sifuri.

Kwa upande mwingine, shule za Kiislamu hazijajitokeza kwa wingi katika nafasi za juu za ufaulu. Hali hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi, na inazua maswali: Kwa nini shule za Kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa? Je, tatizo ni mfumo wa elimu, usimamizi, au kuna mambo mengine yanayochangia hali hii?

TATIZO LIKO WAPI?

Uchambuzi wa hali ya shule za Kiislamu unaonesha changamoto mbalimbali zinazoweza kuwa sababu ya matokeo yasiyoridhisha.

1. Changamoto ya Usimamizi

Shule nyingi za Kiislamu huanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya kidini pamoja na elimu ya kawaida. Hata hivyo, usimamizi wa shule hizi mara nyingi haupo kwenye mfumo thabiti kama ule wa shule za Kanisa, ambazo zinakuwa chini ya taasisi zilizo na uzoefu wa miaka mingi katika uendeshaji wa taasisi za elimu.

Shule nyingi za Kanisa zinamilikiwa na majimbo ya Kanisa Katoliki, ambayo yana mtandao mpana wa usimamizi, huku bodi za shule zikiwa na utaratibu wa kufuatilia mwenendo wa kila taasisi. Kwa upande wa shule za Kiislamu, mara nyingi usimamizi wake hutegemea watu binafsi au taasisi zisizo na mfumo madhubuti wa ufuatiliaji wa maendeleo ya shule na walimu.

2. Mchanganyiko wa Mtaala

Shule za Kiislamu zina jukumu la kufundisha masomo ya dini pamoja na masomo ya mtaala wa serikali. Wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye masomo ya dini, jambo ambalo linaweza kupunguza muda wao wa kujifunza masomo ya kawaida.

Kwa mfano, shule za Kanisa zinazingatia mfumo wa mtaala wa serikali kwa ukamilifu, huku masomo ya dini yakiwa sehemu ya malezi badala ya kuwa sehemu kubwa ya ratiba ya shule. Kwa upande wa shule za Kiislamu, mgawanyo wa muda kati ya masomo ya dini na masomo ya kawaida unaweza kuathiri maandalizi ya wanafunzi kwa mitihani ya taifa.

3. Ukosefu wa Walimu Bora

Moja ya sababu kubwa zinazochangia ufaulu wa shule za Kanisa ni uwekezaji mkubwa katika walimu wenye sifa na uzoefu. Shule hizi huwalipa walimu vizuri, huwapa mafunzo ya mara kwa mara, na kuhakikisha mazingira mazuri ya kufundisha.

Kwa upande wa shule nyingi za Kiislamu, changamoto ya bajeti inasababisha walimu wengi wasilipwe vizuri au kutokuwa na mafunzo ya mara kwa mara ya kuongeza ufanisi wa ufundishaji. Hii inapelekea shule kukosa walimu wenye weledi wa kutosha kuandaa wanafunzi kwa ushindani wa kitaifa.

4. Miundombinu Duni

Shule za Kanisa zinahakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na maabara bora, maktaba za kisasa, na vifaa vya kujifunzia vya kutosha. Kwa upande wa shule nyingi za Kiislamu, ukosefu wa rasilimali hizi ni changamoto kubwa, jambo ambalo linaweza kuathiri viwango vya ufaulu.

5. Motisha kwa Wanafunzi

Katika shule za Kanisa, kuna utamaduni wa kushindanisha wanafunzi na kuwatia motisha kupitia zawadi na mfumo wa kutambua juhudi zao. Wanafunzi wanahamasishwa kushiriki katika mashindano ya kitaaluma na kupewa mwongozo wa karibu na walimu wao.

Kwa upande wa shule za Kiislamu, motisha kama hizi hazionekani kupewa kipaumbele kwa kiwango kikubwa. Hali hii inawafanya wanafunzi wengi wasikazane katika masomo ya kawaida kwa bidii ile ile inayoshuhudiwa katika shule za Kanisa.

NINI KIFANYIKE KUBORESHA UFAULU WA SHULE ZA KIISLAMU?

Ili shule za Kiislamu zifanye vizuri zaidi katika mitihani ya taifa na kushindana na shule za Kanisa, yafuatayo yanapaswa kufanyiwa kazi:

1. Kuimarisha Usimamizi
Shule za Kiislamu zinahitaji kuwa na mfumo thabiti wa usimamizi, kwa mfano, kuanzisha bodi za uendeshaji zitakazowajibika kufuatilia maendeleo ya shule na kuhakikisha viwango bora vya elimu vinazingatiwa.


2. Kuboreshwa kwa Mtaala
Badala ya kugawanya muda kati ya masomo ya dini na masomo ya kawaida kwa namna inayoweza kuathiri ufaulu, shule zinapaswa kuhakikisha kuwa ratiba ya masomo inatilia mkazo maandalizi ya mitihani ya taifa huku masomo ya dini yakipangwa kwa namna isiyozuia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.


3. Uwekezaji Katika Walimu
Shule za Kiislamu zinapaswa kuweka kipaumbele katika kuajiri na kuwahifadhi walimu wenye sifa bora kwa kuhakikisha wanapewa mishahara mizuri na mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha mbinu zao za ufundishaji.


4. Kuboresha Miundombinu
Kama ambavyo shule za Kanisa zinawekeza katika maabara, maktaba na vifaa vya kujifunzia, shule za Kiislamu zinapaswa kufanya vivyo hivyo ili kuwapa wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia.


5. Motisha kwa Wanafunzi
Ni muhimu kwa shule za Kiislamu kuanzisha utaratibu wa kuwatia moyo wanafunzi kupitia tuzo kwa wale wanaofanya vizuri, programu za mashindano ya kitaaluma, na kuweka mifumo ya kuhamasisha bidii darasani.

HITIMISHO

Matokeo ya mwaka 2024 yanaendelea kuonyesha kuwa shule za Kanisa zinafanya vizuri zaidi katika mitihani ya taifa kwa sababu ya mifumo yao imara ya usimamizi, uwekezaji katika walimu, miundombinu bora, na mtazamo wa elimu kama sehemu ya maendeleo ya jamii.

Kwa upande wa shule za Kiislamu, kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili kufanikisha matokeo bora. Ikiwa usimamizi utaimarishwa, walimu bora wataajiriwa, miundombinu itaboreshwa, na wanafunzi watapewa motisha ya kutosha, kuna uwezekano mkubwa wa kuona shule hizi zikifanya vizuri na kushindana kwa karibu na shule zinazoongoza nchini.
Buku haramu
 
Mkuu ninachojua Feza sio shule ya Kiislamu hata kama inamilikiwa na Waturuki ambao almost wote ni Waislamu. Ni sawa na useme Tusiime au Kaizilege ni za Wakristu kisa dini za wamiliki.

Aga Khan ni taasisi ya Kiislamu ya kimataifa hivyo katika kujibu changamoto yetu bado haiwi mfano mzuri.
Hizo nyingine naamini ndio za kwetu wabongo wenyewe.

Hapa nchini tuna Al Muntazir ni International School ya Kiislamu, sijajua kama kuna International School ya Kikristo.

Shule za BAKWATA nazo ni za Waislamu, hakuna sister wa kanisa au padre anaziongoza. BAKWATA sio Walutheri wala walokole.
Feza ni shule za kiisilamu, mwanzilishi wake Fethullah Gulen ni neo-Ottomanist na ana bifu sana na Erdogan ndio maana wakati wa Magu Uturuki walikua wanaforce sana zifungwe. Unaweza Google huyo mhusika kwa maelezo zaidi

Stage set for battle over Feza Schools

Kwani Shule za Wakatoliki ama Taasisi nyengine za Wakristo sio za Kimataifa?

Na tatizo hapa ni Bakwata, ingekua ni waisilamu basi taasisi zote zingefanya vibaya, why iwe ni wao tu?
 
Anna tibaijuka anayo majibu ya kutosha juu ya swali lako. Fuatilia ili ujue wale wanaoteuliwa kusahihisha mitihani, pamoja na maagizo wanayopewa
Ingawa itakuwa NI ngumu kumeza, lkn kuna kitu utaking'amua
Ana Tibaijuka ndiyo anayewateua? Na hili tatizo halipo Tanzania peke yake for your information, angalia nchi zote za Sub Saharan Africa kwanza angalia zenye majority ya Waislamu au jamii za Kiislamu katika nchi ambazo wamechanganyikana Waislamu na Wakristu. It's the shit, historically Waarabu(walioleta Uislamu) na Wazungu(walioleta Ukristu) wanatofauti sana jinsi wanavyozingatia elimu na ndiyo root ya yote haya.
 
Halafu kesho na keshokutwa, wagalatia wakijaa vyuo vikuu, wakiajiriwa zaidi, wakijaa serikalini na kwenye nafasi nyeti anatokea kima kadhaa wa kijahidina na kuropoka nchi hii ni mfumo kristo!
Ukiona vinaelea ujue vimeundwa.
 
Back
Top Bottom