Kwanini Shule za Serikali za vipaji maalum hazifanyi vizuri mitihani ya kidato cha nne (CSEE) tofauti na ile ya kidato cha sita(ACSEE)

Kwanini Shule za Serikali za vipaji maalum hazifanyi vizuri mitihani ya kidato cha nne (CSEE) tofauti na ile ya kidato cha sita(ACSEE)

Kamba certification ya kuwa special school inatolewa moja.
Enrollment kwa olevel na a level ni tofauti

Ile ni shule ya kata ,wakaanza wakanzisha a level pale wakawa wanachukua one kali kali tu kwa a level toka shule za mikoa mbali mbali

But huku o level wanachukua wa pale pale arusha sasa sijui kama wamebadilika ,ila ndio ilikuwa hivyo tangu zamani

Ndio matokeo ya o level na a level hayashabihani hata kidogo nadhani umenipata
 
Unaenda kusaka data au unaenda kuisaka mood kwanza haha
Aaaaah hata huo mda ninao, huko special school nilipita advance,
Mateso tupu, juhudi binafsi za mwanafunzi ndo zinazobeba shule wala sio kitu kingine.
 
Enrollment kwa olevel na a level ni tofauti

Ile ni shule ya kata ,wakaanza wakanzisha a level pale wakawa wanachukua one kali kali tu kwa a level toka shule za mikoa mbali mbali

But huku o level wanachukua wa pale pale arusha sasa sijui kama wamebadilika ,ila ndio ilikuwa hivyo tangu zamani

Ndio matokeo ya o level na a level hayashabihani hata kidogo nadhani umenipata
Yap hapo sawa Kisimiri kwa o level wanachukua katani na hayo ni makubaliano na yule muzungu ila hapo katani sio tu wanajichukulia wanachukua Cream yani.
 
Shule za serikali - Hapa Kazi tu

Private - kazi na ziendelee
 
Angalia Idadi ya wanafunzi mfano Mdogo tuu Ilboru - Div I - 103 sasa unalinganishaje na shule yenye darasa la watu 20 -. 30
 
Vimemo vimemo,
Watoto wengine wanaenda na vimemo ndo wanafanya matokeo yasiwe mazuri.
Ila all in all, hizi shule nzuri sana zinawasaidia sana vijana kuwa wapiganaji tofauti ni hizi za Ada ya milioni 10+
 
Kisimiri kwa upande wa o level n sekondari ya kata inachukua watoto wa palepale TU

Kwa advance ndio WAMEIFANYA KUWA YA VIPAJI MAALUMU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kisimiri kwa upande wa o level n sekondari ya kata inachukua watoto wa palepale TU

Kwa advance ndio WAMEIFANYA KUWA YA VIPAJI MAALUMU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hakuna shule ya Special ya hivyo we jamaa....Kisimiri kwa makubaliano ya Prof na Serikali ni Kwamba O level wachukuliwe wakazi wa pale ila cream kama wanavyofanya vipaji afu Advance wachukue all over kama zingine......serikali ilitaka kufanya kote jamaa akadai ile shule alijenga kama zawadi kwa wana kisimiri maana wazazi wake waliishi pale....Kisimiri bila average ya YA A pale huendi
 
walimu wa shule za gvt wanadili na mambo yao binafsi na cyo wanafunzi

unakuta mwl hajaingia darasan zaidi ya miez 6 na hakuna wa kumuuliza

nina mtoto alichaguliwa special sch lkn mpk now najuta kwa nn nilimruhusu aende huko
 
hata hizo advance za government zinazofanya vzr, mara nyingi huchukua hizo cream zinazotoka st. Francis, KEMEBOS na Feza.

msingi ndo kila kitu. O'level kama mzazi anauwezo ampeleke mtoto shule nzr ya binafsi kama st. Francis na Feza. Advnce ndo wakasome gvnt.
 
Tatizo hapa nchini viongozi wengi wao ni feki,, kwa hiyo kila kitu kitakuwa ovyo tu
 
Hizi shule zinachukua wanafunzi wa wastani wa juu kabisa, yani wanafunzi waliofanya vizuri darasa la saba kwa kifupi wanachukua Cream tupu, Hapa naongelea shule kama Kibaha, Mzumbe, Kisimiri, Msalato, Tabora Boys n Girls , Kilakala na Ilboru .Shule hizi upande wa Olevel hazifanyi vizuri sana unakuta mpaka 0 za kutosha unabaki unajiuliza hii kweli ilikua Cream au samri? wakati mtoto alitoka shule ya msingi akiwa na Ufauru wa kutisha A zote anaenda kipaji maalumu kipaji kinayeyuka anazungusha yai.

Kwa Advance shule hizi kiukweli zinajitahidi na hapa tuangalie ulinganyifu wa ufaulu wa baadhi ya hizi shule kati ya Olevel(CSEE) na Advance (ACSEE) kwa miaka ya nyuma na sasa 2021

2️⃣0️⃣1️⃣6️⃣

1. MZUMBE (O LEVEL KITAIFA YA 27 ikiwa na div 4-1, na 3-12. ADVANCE KITAIFA YA 8)

2.ILBORU ( O LEVEL KITAIFA YA 42 ikiwa
na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 9)

3.KIBAHA( O LEVEL KITAIFA YA 1️6️ ikiwa na div 4-1. ADVANCE KITAIFA YA 7)

4.KISIMIRI (O LEVEL KITAIFA YA 592 ikiwa na div 0-22, 4-95, 3- 25. ADVANCE KITAIFA YA 1)

2️⃣0️⃣1️⃣8️⃣

1.KILAKALA (O LEVEL KITAIFA YA 76 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 14)

2.MSALATO ( O LEVEL KITAIFA YA 102 ikiwa na div 4-12. ADAVANCE KITAIFA YA 17)

3.TABORA GIRLS ( O LEVEL KITAIFA YA 90 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 11)

4.TABORA BOYS ( O LEVEL KITAIFA YA 67 ikiwa na div 4-1.ADVANCE KITAIFA YA 15)

2️⃣0️⃣2️⃣1️⃣

kISIMIRI ( O LEVEL KITAIFA YA 404 ikiwa na div 4-60. ADVANCE KITAIFA YA 1)

KILAKALA ( O LEVEL KITAIFA YA 30. ADVANCE KITAIFA 56).

ILBORU (O LEVEL KITAIFA YA 23. ADVANCE KITAIFA .18)

MZUMBE ( O LEVEL KITAIFA YA 10. ADVANCE KITAIFA 10)

Baaada ya kuangalia viwango hivyo vya miaka ya nyuma mpaka karibuni utaona kabisa pamoja na kwamba shule za serikali zinachukua cream lakini wanashindwa kuzirutubisha ziendelee kubaki cream ambapo wengine hubadirika kutoka Cream kwenda maziwa mgando.kutoka kuingia na wastani wa A shule ya kipaji na kuchomoka na Div 4 au 0 ni hatari mno.

Ona shule kama Kisimiri unaweza kudhani wao labda wamejikita zaidi Advance na kuwaacha wale wa o level wapambane na hali zao shule Advance inakua ya 1 lakini O level 0 za kutosha na 4 wakati utaratibu kwa level zote ni ule ule kuchukua Cream.

Shida ipo wapi wazee wangu? Huku government hususani o level ni kwamba serikali inashindwa kuvilea vipaji vyenye umri wa balehe na kuweka mkazo zaidi kwa wanaojitambua maana Advance kidogo mtu akili inaelewa na kupambanua majambo.

Hii tofuati kabisa na shule za binafsi ambazo pia moja ya sababu za ufaulu wao mkubwa kuchukua cream inatajwa lakini mbona wenzetu wanawasha kote kote mfano Marian boys and girls, Feza Boys n Girls wakiwasha top 10 olevel unakuta na Advance wamo....Pia wenzetu wa Binafsi O level ambapo government inachechemea wao ndo wanawasha haswa si unaona Cream za KEMOBOS zote one , Cream za St Francis Zote one, Cream za Bright na waja zote one sasa kwa nini Cream zetu za O level ni ngumu kutoa one zote basi angalau muishie 3 kweli Cream mnailambisha 4 na 0 sijapenda aisee.

Eti wakuu mnaona sifa kuitwa wakuu wa shule special na kupewa kipaumbele cha kufanya selection? Wakati mikakati ya kumaintain vipaji vyetu ni 0 😱

Kwa nini yani Whyyyy jaman whhhhy ??
Shule gani ya vipaji imefanya vibaya, au unaangalia rank tu? Weka hapa matokeo ya Mzumbe, Tabora boys, Tabora girls etc
 
Hakuna shule ya Special ya hivyo we jamaa....Kisimiri kwa makubaliano ya Prof na Serikali ni Kwamba O level wachukuliwe wakazi wa pale ila cream kama wanavyofanya vipaji afu Advance wachukue all over kama zingine......serikali ilitaka kufanya kote jamaa akadai ile shule alijenga kama zawadi kwa wana kisimiri maana wazazi wake waliishi pale....Kisimiri bila average ya YA A pale huendi
Cream ya kata haifanyi shule kuwa special
Unajua hiyo kata ina shule za msingi ngapi?
 
Kisimiri ni special kwa advance tu, o level ni kama shule ya kata.
Sababu zipo nyingi
1.Kuna wanafunzi wa kawaida au vilaza wanajiunga na special schools kwa mlango wa nyuma aka janjajanja.
2.Janja janja kujiunga special school ni ngumu,wanaenda wenye sofa husika.

Swali la nyongeza
Nitajie shule za kanisa au mashirika ya kanisa katoliki zinazofanya vizuri kidato cha 6?
 
Sijasoma uzi wako ola nataka nikuambie hakuna shulw wanaiva mitihani kama private school. Enzo za ujana wangu niliwahi kuwa mwalimu wa taaluma private school fulani hivi; hivyo msinibishie
 
Nitaongelea kwa Personal experience

O 'level kwa shule za serikali ni mtihani, masomo ni mengi na unapaswa kuyafaulu yote ili matokeo ya jumla yawe vizuri. Hapa bado balehe ndio inachemka yaani watakaoweza kubalance mapenzi na shule au wajitenge nayo kabisa ndio wanafaulu, waliobakia wengi wanafeli, sio sababu hawana uwezo ila mihemko imezidi

A 'level, wengi mnakutana mmefaulu na mnachoendelea kujifunza ni kitu mtu umependa na pia ni muendelezo wa combination ulizozichagua mwanzoni. Wengine wanafika shule washakata topics zote za form 5 kwa hiyo sharing inakuwa na nguvu zaidi

Pia mihemko ya ujana ipo ila kuna kautulivu na maturity flani inakuwepo kwenye kuicontrol, unless ukutane na mtu katoka seminari au single sex schools ambazo zipo strict kwa hiyo akikutana na mixture anapagawa..
 
Kisimiri ni special kwa advance tu, o level ni kama shule ya kata.
Sababu zipo nyingi
1.Kuna wanafunzi wa kawaida au vilaza wanajiunga na special schools kwa mlango wa nyuma aka janjajanja.
2.Janja janja kujiunga special school ni ngumu,wanaenda wenye sofa husika.

Swali la nyongeza
Nitajie shule za kanisa au mashirika ya kanisa katoliki zinazofanya vizuri kidato cha 6?
Kisimiri ni special full afu kutaja kuna Marian, Cannosa, Mazinde Juu, Maria Gorreth aiseee tulia
 
Back
Top Bottom