Kwanini siku 100 za Rais Samia zitimie leo tarehe 27 badala ya 29/06/2021?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Nimesikia katika vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kuwa Rais Samia Suluhu ametimiza siku 100 madarakani leo 27/06/2021.

Nachokumbuka huyu Rais Samia alikula kiapo cha kuwa Rais wa JMT tarehe 19/03/2021 na hivyo siku 100 ni keshokutwa 29/06/2021.

Inakumbukwa Rais John Magufuli alifariki tarehe 17/06/2021 na kwa muda huo haikuwa rasmi kuwa tayari nchi imekuwa chini ya Makamu wa Rais isipokuwa tu pale alipokula kiapo rasmi tarehe 19/03/2021.

Ikumbukwe pia hapo tu baada ya Kifo cha Hayati Magufuli kulikuwa na kukuruka nyingi za nani awe Rais na ndiyo maana tulimaliza takriban siku mbili bila kuwa na Rais rasmi wa JMT japo katiba ilikuwa wazi kabisa.

Niondoeni tongotongo kwani atimize siku 100 leo.

Asanteni.
 
Mkuu March, May zina siku 31 kwahiyo zimeongeza siku 2 kwenye mwezi kwahiyo Ukipiga miezi mitatu ya siku 30 = 30x3 =90 Ukiplus 10 kutimia tarehe 29 unapata 100 ila kuna siku 2 zimezidi za March 31 na May 31 ,ni sahihi leo ni iku ya 100.
 
Mkuu March,May zina siku 31 kwahiyo zimeongeza siku 2 kwenye mwezi kwahiyo Ukipiga miezi mitatu ya siku 30 = 30x3 =90 Ukiplus 10 kutimia tarehe 29 unapata 100 ila kuna siku 2 zimezidi za March 31 na May 31 ,ni sahihi leo ni iku ya 100.
Sikuwaza juu ya hili, nlitumia tarehe na nadhani ndiyo sahihikabisa bila hayo ya miezi ya March na May kuwa miezi mirefu.
 
Nimesikia ktk vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kuwa Rais Samia Suluhu ametimiza siku 100 madarakani leo 27/06/2021.

Nachokumbuka huyu Rais Samia alikula kiapo Cha kuwa Rais wa JMT tarehe 19/03/2021 na hivyo siku 100 ni keshokutwa 29/06/2021.

Inakumbukwa Rais John Magufuli alifariki tarehe 17/06/2021 na kwa muda huo haikuwa rasmi kuwa tayari nchi imekuwa chini ya Makamu wa Rais isipokuwa tu pale alipokula kiapo rasmi tarehe 19/03/2021.

Ikumbukwe pia hapo tu baada ya Kifo cha Hayati Magufuli kulikuwa na kukuruka nyingi za nani awe Rais na ndiyo maana tulimaliza takriban siku mbili bila kuwa na Rais rasmi wa JMT japo katiba ilikuwa wazi kabisa.

Niondoeni tongotongo kwani atimize siku 100 leo.

Asanteni.
Hizo kukuruka za nani awe Rais zilikua ndani ya moyo wako au maana kila kitu kilikua wazi kua Samia ndio Rais mpya kwa Mujibu wa katiba.
 
Nimesikia ktk vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kuwa Rais Samia Suluhu ametimiza siku 100 madarakani leo 27/06/2021.

Nachokumbuka huyu Rais Samia alikula kiapo Cha kuwa Rais wa JMT tarehe 19/03/2021 na hivyo siku 100 ni keshokutwa 29/06/2021.

Inakumbukwa Rais John Magufuli alifariki tarehe 17/06/2021 na kwa muda huo haikuwa rasmi kuwa tayari nchi imekuwa chini ya Makamu wa Rais isipokuwa tu pale alipokula kiapo rasmi tarehe 19/03/2021.

Ikumbukwe pia hapo tu baada ya Kifo cha Hayati Magufuli kulikuwa na kukuruka nyingi za nani awe Rais na ndiyo maana tulimaliza takriban siku mbili bila kuwa na Rais rasmi wa JMT japo katiba ilikuwa wazi kabisa.

Niondoeni tongotongo kwani atimize siku 100 leo.

Asanteni.
Hapana. Kwanza Magufuli alitangazwa kufariki dunia 17/03/2021 siyo mwezi wa sits. Ile siku ya kutangazwa kifo ndio siku ambaye Samia alikuwa Rais wa JMT kwa mujibu wa Katiba yetu. Hawa waliokuwa wakikukuruka walikuwa na yao nje ya Katiba. Kilichobaki ilikuwa ni kuapishwa tu lakini alikuwa Rais tangu siku ya kufariki kwa Mwendazake, a.k.a Hamnazo
 
Naanza kukupata kwa mbali. Lakini alianza rasimi Urais baada ya kiapo
 
Siku ya Kiapo ni uthibitisho tu wa kukabidhiwa mamlaka. Ndiyo maana mtu anawaeza kuapishwa leo lakini barua ya uteuzi wake ikasema uteuzi huu ni wa kuanzia tarehe 25 Juni 2021. Yaani tarehe ya nyuma kabisa. Wengine watasema kuna miezi inasiku 28, 30, 31. Lakini ukweli ni kwamba ukizaliwa tarehe 1/7/2021 mwaka mmoja utatimia tarehe kama hiyo ya mwaka unaofuata bila kujali tofauti ya mrefu wa mwezi mmoja mmoja.
 
Kwanini siku 100 za Rais Samia zitimie leo tarehe 27 badala ya 29/06/2021?

Toka aapishwe tarehe 19/3/2021, siku mia za Rais Samia Suluhu Hassan kulingana na hesabu zangu (kumbuka mimi ni mwana hesabu) zilitimia tarehe 27/6/2021...

Machi....12
Aprili.....30
Mei........31
June......27

Jumla...100

Kama hesabu hazipandi, ruhusa kutumia vidole!
 
Siku aliyokufa huyo shetani dhalimu haina umuhimu wowote kwetu wengine labda kwa waumini wake.
Hata siku ya kufa mama yako mzazi unafikiri watu wote tutaona/tuliona umuhimu? Huyo Baba wa taifa Mwalimu Nyerere tu kuna watu wanamlaani ndio itakuwa huyo Magufuli?
 
Back
Top Bottom