Nyingi ya hypothesis ulizotaja sioni zikiwaandama sana kundi la vijana uliowataja... yaani wanafunzi!!
Kinyume chake, naona zina nafasi kubwa kwa vijana ambao tayari wameanza maisha... labda mtu kamaliza chuo na sasa yupo mtaani, au hata kaishia elimu ile ambayo kutokana na sababu moja au nyingine, haimwezeshi kwa muda huo kuendelea zaidi, na badala yake, anatakiwa kuanza maisha!
Sasa hebu turudi kwa vijana waliomaliza vyuo! Siku hizi nasikia mwamba ambae umetumia picha yake kama avatar yako amegoma kabisa kuajiri!
Kwamba, kuna Walimu na Madaktari kibao na watu wa fani zingine wame-graduate tangia 2015 lakini bado wapo tu mtaani!
Sasa hivi watu kama hao utashangaa wakiwa na depression hasa ukizingatia wengi wanatoka familia maskini?!
Najua wapo watakaosema kwanini wasijiajiri... yeyote atayesema hivyo ni stupid kwa sababu kwa maisha haya hakuna mwenye resources za kujiajiri halafu akaacha kujiajiri!
Haya turudi wale walio vyuoni! Wakati nipo Mwaka wa II chuo, alikuja chuo mshikaji mmoja ambae alikuwa ame-graduate chini ya mwaka mmoja tu uliopita!
Jamaa alikuja pale akiwa kama mwajiriwa wa NHIF, na alikuwa kanona kweli kweli! Akawa anatupatia story za washikaji zake wengine waliokuwa wameajiriwa hapa na pale! Ile kwetu sie ilitupa moyo sana na kuona kumbe hata sisi, it's a matter of time kabla hatujalamba ajira!
What about wanafunzi wa vyuoni hivi sasa?! Wale waliowatangulia ndo kwanza wanakutana nao mitaani wakiwa choka mbaya, huku wengine wakisukuma maisha kwa ku-bet!!!
Hivi utashangaa wanafunzi nao wakiwa katika hali ya kukosa utulivu kama tuliyokuwa nayo sie?! Yaani mshikaji na AA zake zote zile anaishia ku-bet?!!
Hao wanaondesha maisha kwa ku-bet sasa!!! Trust me, maisha yako hayawezi kutegemea kamali halafu usiwe na msongo wa mawazo!!