Kwanini siku hizi vijana wadogo wana kiwango kikubwa cha stress na depression?

Kwanini siku hizi vijana wadogo wana kiwango kikubwa cha stress na depression?

We nchi rais anasema atawapiga mpaka shangazi wa wapinzani, na ataamua kumkata yeyote kwenye mbio za ubunge, kulingana na atakavyoamka.

Kwa nini watu wasiwe na stress?

Kama mtu anayewania ubunge anaweza kukatwa kwa rais atakavyoamka siku hiyo, huyu kijana wa mtaani si anaweza kuuawa kabisa?

Watu wanasoma wanahitimu, wanaingia mtaani miaka mitano hawana kazi.

Kwa nini wasiwe na stress?

Nchi hata kucheka tu unaweza kushikwa na Polisi.

Kwa nini watu wasiwe na stress?
 
Miaka ya 70 wazazi wetu hawakua na degree, magari, majumba ya kisasa(gharama) lakini walikua wanaishi maisha ya furaha, upendo na kuhurumiana.

Sasa hivi kijana anaweza kua na elimu nzuri, nyumba nzuri, kazi nzuri, usafiri, mke au mume mzuri lakini bado hana furaha, sonono inammaliza yote ni kutoridhika anatamani awe kama fulani, atembee na mke au mume wa fulani, amzidi kipato mtu fulani, awe na gari kama ya fulani.

Furaha zetu siku hizi tunazitafuta kwenye vitu na sio utu.
 
Kweli, walio wengi kundi lao ni hii sababu.
 
Ni kweli ....umekwaza watu sana humu..na ulipoambiwa una stress ndio ukazidi. . ..kumbe ilikuwa ....cha mirembe kinakuita.. Mungu aendelee kukuponya ...hongera kwa kuwa mkweli mkuu... .. maisha yana changamoto sana!
Stress zilifanya nikapigana ngumi nyingi sana, nikawa natukana hovyo humu JF thank Jah at least nimeanza kubadirika.
 
Binadamu sisi tupo tofauti sana lakini kwenye huo huo utofauti wetu pia kuna ufanano wetu

Nashangaa sana kijana mwenye zaidi ya miaka 24 au chini ya hapo eti anasema mapenzi ndiyo tatizo
 
Wadau wa JF.
Leo ningependa tujadili kidogo hali ya afya ya akili inayoendelea kuwatafuna vijana wetu mitaani bila jamii kuangazia.

Leo ni hali ya kawaida kukuta kijana teenager anayesoma sekondari au chuo kikuu akilalamika kuwa na msongo mkubwa wa mawazo au kitaalamu inaitwa Sonona (depression). Hali hiyo imepelekea baadhi yao kujizuru hadi kufikia hatua ya kujaribu kujiua.

Swali la kujiuliza: Nini kimepelekea ongezeko kubwa la vijana wadogo kuwa na depression: Je, ni kukosa malezi mazuri?, kushindwa kufikia ndoto na malengo yao? Je, mitandao ya kijamii imesababisha wao kutamani maisha ya kifahari wanayoyaona kwenye 'status' za wenzao? Je, ni hali ngumu za kiuchumi kwenye familia zao? Je, ni changamoto za kimapenzi?

Leo ningetamani nipate maoni yako, nini kinachangia ongezeko kubwa la sonona kwa vijana tofauti na ilivyokuwa miaka 15 na kurudi nyuma iliyopita Karibu tujadiliane pamoja

.View attachment 1488505
Solution hapo ni be your self
 
Miaka ya 70 wazazi wetu hawakua na degree, magari, majumba ya kisasa(gharama) lakini walikua wanaishi maisha ya furaha, upendo na kuhurumiana.

Sasa hivi kijana anaweza kua na elimu nzuri, nyumba nzuri, kazi nzuri, usafiri, mke au mume mzuri lakini bado hana furaha, sonono inammaliza yote ni kutoridhika anatamani awe kama fulani, atembee na mke au mume wa fulani, amzidi kipato mtu fulani, awe na gari kama ya fulani.

Furaha zetu siku hizi tunazitafuta kwenye vitu na sio utu.
[emoji817][emoji818]
 
We nchi rais anasema atawapiga mpaka shangazi wa wapinzani, na ataamua kumkata yeyote kwenye mbio za ubunge, kulingana na atakavyoamka.

Kwa nini watu wasiwe na stress?

Kama mtu anayewania ubunge anaweza kukatwa kwa rais atakavyoamka siku hiyo, huyu kijana wa mtaani si anaweza kuuawa kabisa?

Watu wanasoma wanahitimu, wanaingia mtaani miaka mitano hawana kazi.

Kwa nini wasiwe na stress?

Nchi hata kucheka tu unaweza kushikwa na Polisi.

Kwa nini watu wasiwe na stress?
[emoji817][emoji818]
 
High level of expectations
Vijana wengi tunajipimia pakubwa mno almost kwenye kila nyanja uchumi, mapenzi, masomo n.k
Na inapotokea hatujafika zile expectations tunazojiwekea ndipo stress zinapoanzia.
Na wengi haturidhiki ingawa kutokuridhika ni Tabia ya kibinadamu Ila tunasahau kuwa na subira sasa
Kutokua na subira plus kuwa na high level of expectations kukakutana na mazingira ya mitandao ya kijamii ambayo inawaonyesha watu wenye umri Kama kijana alionao na yuko mahali Fulani ndipo stress inazidi Mara nyingi.
Hatusikilizi ndani mwetu Nini tunataka tuwe na pale mazingira yanapotusukuma pasipo petu ndipo stress huongezeka maradufu.

Hakuna kazi kubwa sana Kama kuiongoza nafsi yako
 
ukosefu wa pesa, kutotimiza goals,kufeli kwny jambo fulani,pia pressure kutoka kwny jamii inayotuzunguka inasababisha streess . mfano soma hii ..

Ukishafikisha miaka 20 na kuendelea na bado unawategemea wazazi kwa asilimia 100, umekwisha
Yanii hii thread iko very negative ingawa angejaribu kuiweka vizuri ingefikisha ujumbe ambao ni positive

Pressure Kama hizi zinaua Sana Sana kwasabababu ukiangalia mtu 23-25 ndo umri wa kumaliza chuo kikuu akikutana na kitu Kama hiki na Hana ajira yuko nyumban unadhni Nini kitatokea???
 
Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa anawajenga vijana kuanzia shule za msingi, sekondari hadi chuo kikuu.
Hata watoto wake waliishi kama Watanzania wengine.
Aliwaambia watoto wake " magari ya Ikullu ni kwa ajili ya Rais na si watoto au mke"
Watoto wa Mwalimu tulipanda nao mabasi ya UDA na kusoma nao shule za kawaida.
Shuleni walienda kwa kupanda treni au mabasi ya kawaida na wala si ndege.
Kwa ujumla watoto wa wakubwa na matajiri tulichanganyika na kula chakula cha ina moja , kuvaa nguo za ina moja na kulala seheme za aina moja tulipokuwa shule na hata Jeshi la kujenga Taifa.
Watoto wa sasa hivi wa viongozi wakuu na matajiri wanaishi maisha ya anasa sana kiasi cha kusababisha wale wengine ambao hawana kitu na wamesoma kukata tama na kuwa omba omba.
Kwa maana ingine ni kwamba vijana wa sasa hivi wanaona pesa ndiyo msingi wa maendeleo wakati sisi tulifundishwa na kukubali kuwa pesa si msingi wa maendeleo bali ni matokeo yake.
 
Back
Top Bottom