Kwanini siku hizi vijana wadogo wana kiwango kikubwa cha stress na depression?

Zamani asilimia kubwa ya familia zilijipatia chakula kwa kulima,siku hizi hata wanaoishia vijijini wengne hawalimi,kijana anaanza kuwaza kwanza msosi nitatoa wapi,akifatia hela ya nguo(siku hizi kila mtu anataka kupendeza Kama mastaa),.. then demu mkali bila kujua atahonga Nini na hapo hana kazi Wala kibarua na bado anachagua hii kazi nafanya hii itanichoresha,...wasipate depression hapo!!..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umetishaaah lol
 
Sababu zipo nyingi za binafsi na ujumla.
1. Ukiisha uwewe.
Ukiishi ndani ya kusudio lako kamwe haya mengine ni ya ziada, msononeko wake ni mdogo sio kama aliye nje ya kusudi. Ndio sababu wengi wetu tunafanya vitu kwa sababu ya wazazi wamekulazimisha, ulishindwa kuendelea na masomo kwa namna moja au nyingine.

2.Mitaala ya shule inapaswa kufumuliwa na kuundwa upya ila kumjengea mtu uwezo wa kujitegemea kimawazo kuliko kutegemea zaidi serikali. Hapa vijana wengi hata tukipewa 10 million kama mtaji kati ya 10 ni mmoja au asiwepo atakayeweza kuuendeleza sio kosa lake ni maandalio aliyoandaliwa toka utotoni. Sheria, sanaa, tech. Hivi vitu vianze kufunzwa kutoka shule za msingi mpaka chuo kikuu.
3. Hofu ni adui mkubwa wa maendeleo ya mtu ni ugonjwa ulao ndani zaidi ya nje. Ndio sababu mtu huyu aliyemaliza chuo hauwezi kumfanyisha biashara ya mtaji usiomkubwa sababu ya hofu jamii itanionaje, mimi mwanadegree hii sio hadhi ya kazi yangu.

4.MFUMO WA NCHI: KIBIASHARA & ELIMU.

5.Ni jambo gumu sana kuliapply ila hivi ndivyo inapasa kua kulijua kusudi lako na wakati wako na kuliishi hilo kusudi lako. Hapa utaona mtu anafanya kitu kijamii ni cheap ila kinampa maendeleo. Mf. Unakuta mtu ni boda boda au dobi amejenga na anasomesha (nina ushahidi wa watu wa hivi) wakat huo kuna mtu anapokea 1M per month maendeleo yke ni kiwanja na furniture za bei ndani.

Tujipambanue huku tukimuomba MUNGU. Maana hata interview za siku hizi ni kama bongo movie tu.
 
Juzi nime screenshot tweet ya Fatma Karume, nikaiupdate kwenye status yangu ya whatsApp. Tweet ilikuwa inamkandia jiwe.

Aiseee palepale nimepokea sms kutoka kwa baadhi ndugu na marafiki, wananiambia niifute haraka. Aliyetisha zaidi ni mzee wangu akaniambia "wewe mtoto futa ujinga wako huo haraka kabla hujapata matatizo, hizi sio nyakati za kupost chochote". Ni halali watu kuwa na stress.
 
Wanamuendekeza tu.

Hivi nusu ya nchi nzima ikiamua ku post hivyo, hao polisi watamkamata nani na wamuache nani?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].. Shikamoo Uncle
Kama Mimi Hadi nimezeeka kabisa.....watu wazima wananiambia shkamoo bro na ukicheki mtu amekukata 10yrs
 
Social media imechangia kwa kiasi kikubwa kuliko tunavyo fikiria.. Sanasana kuona kama kila MTU anafuraha wakati wewe huna n.k

Kingine ni kitendo cha wazazi kuwa busy na maisha kiasi ambacho wanashindwa kuwa karibu na watoto.. Hili pia limekuwa tatizo kubwa kwa watoto millennial generation/generation Y hili ni tatizo kwa dunia nzima sio kwetu tu, ila kwetu bado halijapamba moto kama kwa wenzetu.
 
U

Umeponaje sasa? Weka wazi mbinu ulizotumia ili uwaokoe na wengine wanaopitia maumivu kama yako
Asante sana kwa swali zuri. Ila hapo hukuna mbinu zaidi ya kuchukua maamuzi
 
Wacheni kutupiana swala muhimu na kuzikimbia sababu kuntu.
1 Ni serikali
2.wazazi.
3.walimu
Ndo vyanzo vya matatizo yote.
 
mdhalendo
Nitaongea Mambo 3.

1. Umasikini, ukosefu wa pesa za kukidhi mahitaji muhimu zinaweza kumfanya mtu kuwa na mawazo, hatari zaidi mtu huyo akikosa msaada inaweza kupeleka kukata tamaa na kuona wengine wanapendelewa hp duniani...

2. Matatizo, yapo matatizo ambayo mtu anaweza kujitakia kwa ubishi tu au utashi wake na yapo ambayo yanatokea kwa bahati mbaya Kama ajari au kifo... Mara nyingi tatizo likitokea linampa mtu wakati mgumu wa kufikiri kulitatua, kuishi nalo Kama athari zake zinaendelea...

3. Ubepari, hapa ni kwamba maisha ya tz miaka 15 iliyopita na Sasa ni tofauti. Siku hizi undugu unapotea Kila mtu kivyake, pesa ndio Kila kitu mtu akikosa pesa lazima atakuwa na mawazo...
 
Wanawaza Vyura tu.. maji ya kuwafuga hao vyura hawana. Mbaya zaidi akili hazijakaa kujiongeza namna ya kupata hayo maji.. ila akili zinawaza zaidi jinsi ya kushuka vyura tu.
Mzee umenipa idea hapa. Huu wimbo utapata kuiskia siku za mbeleni km wewe ni muumini wa rap/hiphop.

[emoji1542]Siku hizi sura haina bei, gharama ni mchina/
Akili zimetuama kutazama milima./
Wanatamani vyura ila hawana visima/
Wenye visu wanakula, minyama wanaifinya./
Itaendelea...
Thank you[emoji1477][emoji1477]
 
Yote yana leta maana lakini kwenye mapenzi ni ujinga tu, mtu mwenye nia na maendeleo yake hawezi kufikiria kuhusu mapenzi, Bora umasturbate ili mambo yaende lakini mapenzi ya kufanya upoteze focus, na stress zisizo na maana,

Pia watu hawajui wanataka nini duniani au lengo kuu la maisha hawana, hasa afrika tunaishi ili tusife hapo napo ni tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…