kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nilibebwa kwa kupokezana kutosha shule ya Msingi hadi nyumbani kwetu kilomita 5 nikiwa darasa la nne. Wanafunzi wa kutoka mtaani kwetu walinibeba kama shukurani na pongezi kwa kumpiga jiwe la usoni mwanafunzi mgomvi sana na mwenye nguvu wa darasa la saba B aitwae Mathayo hadi akazirai.
Huyu alikuwa ni mwanafunzi ambae kila siku tukitoka shuleni alikuwa anatusubiri njiani kutupiga bila sababu ya maana. Alikuwa akitunyang'anya kila kitu chetu hadi ikalazimika wazazi wetu kutufuata shuleni kuturudisha nyumbani kwa usalama wetu. Tangu siku hiyo mathayo akaacha tabia yake ile.
Simba waliingia uwanjani kupigana na Mathayo wao (Yanga). Waliingia kama wanyonge na walioapizwa kuhakikisha kuwa mathayo anakufa kwa njia yoyote ile maana wamechoka kuonewa na Yanga.
Simba kuifunga yanga haiondoi ukweli kwamba Yanga ni bora kuliko Simba, ni kama vile walifunga kwa bahati mbaya kwa kutumia jiwe (goli la mapema lililotokana na adhabu ambayo haikuwa adhabu) na kuzirai moja kwa moja. Ukweli huu mtauona siku yanga ikikutana na Simba tena kwenye mashindano ya FA. lilikuwa jiwe tu sio ngumi wala teke.
Wachambuzi wetu wamepata pa kushikia baada ya kuinamishwa vichwa vyao kwa muda mrefu sana na yanga. Ni heri mkaendelea kusema Simba ni mbovu badala ya kuijaza kichwa kwa kuifunga yanga ki mchongo ili iendelee kukiboresha kikosi chake.