Kwanini sisi Waafrika ni Masikini?

Kwanini sisi Waafrika ni Masikini?

Mkuu kwenye suala la uzalendo naliunga mkono moja kwa moja.Uzalendo ungeanzia ngazi ya maofisi yetu mpaka kwa viongozi wetu tusingeona mikataba ya hovyo kwenye rasilimali zetu,matumizi mabaya ya mapato ya nchi.Uzalendo ungekuwepo kwa viongozi wetu kila mwananchi angependa kulipa kodi maana angeamini kodi ingetumika ipasavyo kwenye kuendesha nchi na wala si vikao na maadhimisho yasiyo na tija kwa Taifa.Leo hii nchi inapoteza kodi kubwa kutokana na watu kukosa uzalendo na nchi yao.Bila makusanyo mazuri ya kodi nchi itakuwa hovyo hovyo tu.
 
Lebabu 111 umeongea kitu cha msingi sana maana hata tulichonacho hatuwezi kuvilinda. Lazima tuwajibike kulinda maliasili zetu.
 
Umaskini wa akili pamoja na umaskini wa Kukosa huduma muhimu kama maji,afya,barabara. Ukosefu wa akili inayoweza kufikiri pamoja na kutenda vizuri ndiyo mambo ninayoongelea. Na huo ndo umaskini.
 
Sasa ndo imekuwa too much hata uongozi wanapeana kifamilia mfano mtoto wa jakaya
 
Kwasababu tumetawaliwa hatujielewi na viongozi wa Africa wanajali masilahi yao binafsi si ya nchi au ya wananchi wao.
 
Kwanini Afrika isiwe nchi moja?


Afrika kuwa moja hata Nyerere alishasema haiwezekani sababu ya tofauti nyingi Nyerere alitoa hoja kuwa afrika inaweza kuungana kwa makundi yanayofanana mfano Tanzania Kenya na Uganda zikawa nchi moja, Malawi, Zambia na Zimbabwe zikawa nchi moja, Congo Kinshasa, Congo Brazaville na Gabon zikawa nchi moja, Ethiopia, Somalia, Djibout na Eriteria zikawa nchi moja, Misri, Algeria, Tunisia, Libya na Morocco zikawa nchi moja. South Africa, Lethoto, Swaziland na Namibia zikawa nchi moja.

Orodha ni ndefu kiini cha kusema haya Nyerere alinena kuwa kuna tofauti kubwa tano ya Kwanza weupe wa kaskazini yaani waarabu dhidi ya weusi wa kusini weupe wale watataka wao ndio wawe watawala, sababu ya pili kuna nchi za kuzungumza kiingereza na nchi za kuzungumza kifaransa kila kundi litataka kushika madaraka, sababu ya tatu kuna wa kaskazini wengi ni waislamu na wa kusini wengi ni wakristo, sababu ya nne wakati huo kulikuwa na nchi za kibepari na kijamaa na sababu ya tano kulikuwa na nchi zinazotawaliwa kijeshi na zile zinatawaliwa na serikali za kiraia hizi sababu mbili kwa sasa si tatizo ila zile tatu za mwanzo bado zinasimama na ni kikwazo kikubwa tunachoweza kufanya ni kuungana kwa makundi na kuwa na nchi saba au nane Afrika zenye sauti badala ya 51 za sasa.
 
Ooyooo hii stori naona kama ile ya kitabu cha alif ulela ulela au baadala ya kuhisabu naazi unahisabu makumbi ya naazi
 
Naona ungesema sisi ni wajinga ingefaa. Mungu katuwekea kila kitu almasi dhahabu madini yoote duniani asali na maziwa...lakini kale ka degree ka ujinga akatuongezea kidogo tofauti na mataifa engine. Ndo maana tunaaprofesa na mawaziri madokta ndo wanatuongoza
 
Ukweli ni kwamba sisi nisehemu ya mfumo wa kimataifa wa kiuchumi uitwao sasa utanndawazi,lakini ungemfufua profesa chachaghe seithy chachaghe angekuambia huo ni ubeberu ambaoo ni ubepari uliokomaa ukachukua sura ya ukimataifa, kwa bahati mbaya sisi ni wazalishaji wa rasilimali kwa mfumo huo na wao wanazipeleka viwandani huko kwao.wachina wameiba magogo yetu wanatengenezea fanicha kwao na lile vumbi wanatengeneza zinaziwaka waka wanatuuzia sisi wenyewe-mfumo ule umetufanya mazuzu.

Na rais anayeonesha dalili za kututoa kiuchumi lazima atatengenezewa zengwe na kuondolewa hii ni kuanzia patrice lumumba,thomas sankara,muamar ghadaffi na hugo wa amerikani.

Laiti USSR isingesambaratika balance ingekuwepo na mifumo miwili ingeshindana socialist dominance na imperialism. Russia haiwezi tena maana imeshasaliti ujamaa.
 
Naomba nikusahihishe. Waafrika sio maskini. Maskini wapo India hawa hata ardhi hawana. Papua new Guinea, Vanuatu na baadhi ya mapori ya Amazon. We hujaona maskini? Shida ni kutofanya utafiti hata wa kugoogle tu. Unawaza una conclude. Mtu mwenye mawazo kama haya kushindwa maisha mbona tayari.
 
Mimi, kuna wakati huwa najiuliza. Hivi kwa nini sisi waafrica?

Ukiangalia Historia, mfano kwa habari ya utumwa kwa nini sisi hatukuwaza kwenda kuwatawala wenzetu mabara mengine? kwa nini wao wametutangulia tangu mwanzo? Hata utendaji kazi wao hawa jamaa weupe ni tofauti na wetu. Angalia nchi kama south africa ambapo wamekuwa katika uongozi kwa miaka mingi, hamna longo longo. Naamini kuna kitu ambacho wanacho ambacho sisi hatuna.

Hata timu zetu za mpira mfano Nigeria, Ghana, Ivory Coast, ni tofauti kabisa in terms of consistence. Uwezo tunao lakin unaona kabisa watu hawako serious. Na one of the reasons why wachezaji watu wa africa wakienda ulaya, hata wafanya kazi hufanya vizuri ni kwa sababu kule wanakuta watu wako serious and committed.

Kwanini sisi tulikuwa watumwa kwa mfano, wenzetu walipata wapi akili ya kututawala sisi akili zetu ziliwaza nini? Pamoja na elimu na mabo yote kwa nini bado tunatawaliwa?

Mi nadhani tatizo sio haya tuyaonayo sasa bali, tatizo ni la msingi (foundational problems). Hata tukikaa wenyewe hatupatani na hatufanyi vizuri. Mfano ktk nchi yetu, Mwl Nyerere aliwafukuza wakoloni, hali ya maisha imekuwa mbaya zaidi ya ile iliyokuwepo kabla, na kadiri miaka inavyosonga mbele ndivyo ilivyo ngumu kutoka. Tumeishia kuwaita wale wale tulio wafukuza waje tena kutusaidia.

Hatari sana!
 
Msome Rais Botha wa Sauzi.

We do not pretend like other Whites that we like Blacks. The fact that, Blacks look like human beings and act like human beings do not necessarily make them sensible human beings. Hedgehogs are not porcupines and lizards are not crocodiles simply because they look alike. If God wanted us to be equal to the Blacks, he would have created us all of a uniform colour and intellect.


But he created us differently: Whites, Blacks, Yellow, Rulers and the ruled. Intellectually, we are superior to the Blacks; that has been proven beyond any reasonable doubt over the years. I believe that the Afrikaner is an honest, God fearing person, who has demonstrated practically the right way of being.

Nevertheless, it is comforting to know that behind the scenes, Europe, America, Canada, Australia-and all others are behind us in spite of what they say. For diplomatic relations, we all know what language should be used and where. To prove my point, Comrades, does anyone of you know a White country without an investment or interest in South Africa? Who buys our gold? Who buys our diamonds? Who trades with us? Who is helping us develop other nuclear weapon? The very truth is that we are their people and they are our people. It's a big secret. The strength of our economy is backed by America, Britain, Germany. It is our strong conviction, therefore, that the Black is the raw material for the White man.

So Brothers and Sisters, let us join hands together to fight against this Black devil. I appeal to all Afrikaners to come out with any creative means of fighting this war. Surely God cannot forsake his own people whom we are.
[/B]
 
Nashukuru mkuu, japo inauma kuwa Chini ya other races! Nimepata majibu kwa nini south Africa iko vizuri kuliko nchi zote za Africa! Nadhani ili kuwa na naendeleo Kuna haja ya kuungana na Hawa wadau, kitu ambacho serikali zetu ndio zinafanya, kwa sababu ya inferiority, na ujinga tunakubali mikataba mibovu! Hatari sana!
 
Back
Top Bottom