Kwanini sisi wengine (wengi) hatuna barabara nzuri za mitaani kama Mikocheni, na Upanga? Au hatustahili na hao ndio wananchi sana?

Barabara nzuri mitaani, taa za barabarani mitaani(street lights), mifumo ya kiulinzi(security camera networks), upatikanaji wa maji bila kukatika na mifumo mizuri ya kuifadhi mazingira.

Hivyo hapo juu ni vitu/huduma ambazo hazitakiwi kuwa exclusive hata kidogo kwamba eti ni watu wa hadhi/aina fulani tu ndio wawe navyo.

Hizo ni public services ambazo zinapaswa kuwepo kwanzia uswekeni huko Temeke mikoroshini,gongo la mboto,mburahati,tandale mpaka huko tunapopaita ushuani Masaki,Oysterbay,mikocheni mpaka Mbweni.

Ni jambo ambalo linawezekana kabisa ikiwa tu serikali kupitia idara zake zote za mipango miji hapa nchini itaamua kufanya kazi kwa waledi na kwa dhamira ya dhati, maana kufanya hayo yote hayahitaji gharama kubwa kama kujenga SGR.
 
Ni nchi Maskini tu kama Tanzania ambapo unakuta gharama za kupanga nyumba zinategemeana upatikanaji wa huduma ya maji pamoja na ubora wa barabara zilizopo hapo mtaani eti gari inafika au haifiki au kuna shida ya maji au yanapatikana muda wote.

Matokeo yake sasa unakuta unaoneshwa nyumba ya ajabu ajabu tu ila kodi yake ni kubwa kisa tu iko karibu na barabara na hakuna shida kubwa ya maji.

Na pia vile vile unaweza ukakutana na Nyumba nzuri ina mazingira mazuri ya kuishi ila haina soko sababu tu eti uwepo wa barabara mbovu na kukosekana kwa maji ya uhakika yaan vitu ambavyo havikutakiwa kuwa vya kibabaishaji.

Ni huzuni sana kuona quality ya Nyumba ni least determinant factor of housing price kwa hapa bongo.
 
Kama tabora hadi vichochoro vina lami.
Fika yombo na buza ujionee masaki wakasome
 
Mikocheni ipi labda sijaelewa๐Ÿค”
Watu wanakariri ujue. Mtu hata hajafika Mikocheni anajitajia tu sehemu.

Kuna siku nilikuwa likizo Dar. Nikawa natembea na mshua, akawa kaenda nyumba yake ya Oysterbay kuangalia mambo yake. Kukawa na tatizo la simu pale nyumbani.

TTCL ilikuwa wapo katikati pale Oysterbay Primary kona ya Karume Road na Haile Selassie. Basi ikawa tumeenda pale TTCL. Kufika tu nikawa naangalia ile barabara ilivyopigika, mashimo kibao.

Nikawa najiuliza hii ndiyo Oysterbay wanapokaa viongozi wa nchi na barabara ziko hivi. Huko kwingine si mahandaki?
 
Mwakilishi wa Mbezi Beach nikisaidiana na Pdidy nikiripoti kutoka pande za Mbezi Beach, fezea ndio kama hizi....

Usione hapo kukavu ukasema tunalialia, mvua ikinyesha ni balaaa, na sehemu nyingine kuna mashimo ka mahandaki, ila mama anotosha, kumi tena
 
Kuna sehemu wanaita BWENI huko ndio kuna lami katika kila mtaa ila kuna mitaa michache ndio bado lami haijafika.
 
Usisahau, hata mbinguni kuna class.
 
Kwanini iwe njini pekee? Sisi wengine mbuzi tunakaa zizini?๐Ÿ˜
Hizo ndio akili za maccm na viongozi wao, yaan wenyewe wanaamini barabara nzuri, mifumo mizuri ya kupitisha maji taka na taa za barabarani zinastahili kuwa mijini tu basi. Mawazo ya kipuuzi kabisa halafu eti ndio wanasema watalibadilisha hili taifa kimaendeleo.
 
Kuna sehemu wanaita BWENI huko ndio kuna lami katika kila mtaa ila kuna mitaa michache ndio bado lami haijafika.
Imagine sehemu kama Mbweni ambako kuna idadi ndogo sana ya watu wasiofika hata 2,000 ila kuna lami na taa za bara barani tena zile ambazo zimefungwa security cameras.

Halafu wakati huo Kimara ambako kuna wakazi zaidi ya milion moja, bara bara za mitaani ni mbovu mvua ikinyesha maji yanatwama bara barani.
 
Inasikitisha sana.
 
Sahv ile imepigwa mkeka
Alafu mleta uzi asidhani kila obay,masaki,mikocheni kuna lami
๐Ÿ˜„

Ova
 
Huko kimara nyumba zenyewe
Mjenga hakuna mitaaa
Hata goba huko na kwengineko
Lami labda zitapigwa bara zinazoo tokaa tu..ila ki mtaa msahau ๐Ÿ˜„

Ova
 
Sahv ile imepigwa mkeka
Alafu mleta uzi asidhani kila obay,masaki,mikocheni kuna lami
๐Ÿ˜„

Ova
Dah, sijarudi siku nyingi viwanja vyangu mitaa ya Haile Selassie huko.

Pale mwanangu Gotta Irie alikuwa na collection la reggae sijawahi kuona Tanzania nzima na hata nje utaona collections zile kwenye maduka ya muziki. Easily over 15,000 records and CDs. Miaka hiyo ya 1980s - 1990s.
 
Ila kwa suala la usafi bado hata hizo sehemu unazosema..

Mikocheni mitaro imejaa maji taka , maji machafu kweli....

Ni bora za zaidi hii mifumo ya kujenga mitaro wabadilishe, mitaro ifunikwe kuliko kama hivi inavyoachwa wazi inajaa maji machafu hadi yanatoa harufu mbaya sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ