Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Magari ya kijapani nadhani limit mwisho ni 180,kmh
Ni sera za JDM gari zinazotengenezwa kwa matumizi ya soko la japan speed limit mwish
Kwahiyo tatizo ni kwamba 180km/h haifikiki au barabara ya kwenda Kibaha mbovu au gari imechakaa?
Maana tunaona mara kibao tu watu na IST/Runx/Premio wanafuta visahani.
150 km/h inanitosha sana kwa gari za Japan,sijawahi kuendesha gari za Europe,ila za Japan nimeendesha nyingi ikishafika 120 km/h gari inakuwa nyepesi sana...
Asante sana.Speed ya 180 imewekwa pale Ili ku standardize components na kupunguza manufacturing costs .kimantiki sio kila gari linauwezo wa kufika speed hiyo .
Kwanini zisifike?Asante sana.
Hii ndio watu hawataki kusikia, uniambie TOYOTA CAMI/ PASSO zifike 180km/h - hapana aiseeeeee
Passo vitz cc1000 mwisho ni 140PASSO??? Aiseeee, nafikiri hata uipeleke pale JNIA Terminal 3 - haifiki 180km/h
Inaweza kufika 180 inategemea na mguu wako na barabara.Passo vitz cc1000 mwisho ni 140
Passo vitz cc1000 mwisho ni 140
Tatizo 180km/h kwa mazingira yetu na aina ya magari haifikiki .... Kidogo Premio, hizo nyingine kufika 180 km/h ni almost to impossible ama suicide.
Hebu 'tusimulie' tu huyo uliyemuona na IST/ Runx/ Premio kafuta visahani
Mkuu wapi CC!?180 km / hr inafika bila tatizo...
IST anafuta kisahani? Nitashuka kabla ya kufika tuendako 😆 bora hata premio nitashika roho mkononiKwahiyo tatizo ni kwamba 180km/h haifikiki au barabara ya kwenda Kibaha mbovu au gari imechakaa?
Maana tunaona mara kibao tu watu na IST/Runx/Premio wanafuta visahani.
Kipande cha kiboya hiki Ruvu-Chalinze!180km/h kwa barabara hizi.si utajikuta umetangulia mbele ya haki kabla ya kuchukuliwa na covidView attachment 1716134
Crown je? 😀 😀IST anafuta kisahani? Nitashuka kabla ya kufika tuendako 😆 bora hata premio nitashika roho mkononi
Kuna mshikaji humu alitoa story. Walikua wanatoka Mwanza gari private na wana kadhaa. Ulikua usiku kwahiyo hamna trafick wala jam sana njiani. Kule mjini mjini ilikua poa wanacheka sana kwenye gari kufika maporini dere anafuta kisaani akipunguza sana 100 labda kuwe na tuta.IST anafuta kisahani? Nitashuka kabla ya kufika tuendako 😆 bora hata premio nitashika roho mkononi
Bugatti inaenda zaidi ya 400km/hr.Wakuu
Baada ya kupata bahati ya kuwemo katika magari aina tofauti tofauti, makubwa na madogo lakini kubahatika kuendesha umbali mrefu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kitu kimoja nimekuwa nikijiuliza, ni kwa nini magari ''karibia'' yanaonesha uwezo wa kwenda kasi kufikia mwendo wa 180 km/h?
Nilichogundua, mwendo kasi wa 180 km/h ni mkubwa sana sana sana, haufikiki, ni hatari na sio halisi hasa kwa aina ya magari yetu mengi ambayo ni mtumba huku barabara zetu nazo zikiwa sio rafiki.
Kwa mfano, magari ya cc 900 mpaka 2000cc haya kuwekewa mwendo kasi wa 180 km/h ni sahihi? Kwanini wasingeweka tu mfano 140 km/h? Hebu tuangalie uhalisia, katika mazingira yoyote yenye cc chini ya 1500 inaweza kweli kufika mwendo kasi wa let say 160km/h? Binafsi sidhani. Kwa gari maalumu za kwenda kasi na safari ndefu, ama zenye cc zaidi ya 2500 uwezekano unaweza kuwepo lakini kwa hizi nyingine, nahisi watengenezaji wanatulipisha gharama kubwa kwa kitu ambacho hakipo ama kwa kifupi wanatuibia.
Nini mtazamo wako?
180 km / hr inafika bila tatizo...
Mimi na jirani yangu tulikuwa tunaenda Moshi na IST yake mwaka juzi. Alifuta kisahani japo ni very risky.Tatizo 180km/h kwa mazingira yetu na aina ya magari haifikiki .... Kidogo Premio, hizo nyingine kufika 180 km/h ni almost to impossible ama suicide.
Hebu 'tusimulie' tu huyo uliyemuona na IST/ Runx/ Premio kafuta visahani