Kwanini speed ni 180 km/h?

Kwanini speed ni 180 km/h?

180km/h kwa barabara hizi.si utajikuta umetangulia mbele ya haki kabla ya kuchukuliwa na covid
IMG_4116.jpg
 
Magari ya kijapani nadhani limit mwisho ni 180,kmh

Ni sera za JDM gari zinazotengenezwa kwa matumizi ya soko la japan speed limit mwish

Kwahiyo tatizo ni kwamba 180km/h haifikiki au barabara ya kwenda Kibaha mbovu au gari imechakaa?

Maana tunaona mara kibao tu watu na IST/Runx/Premio wanafuta visahani.

Tatizo 180km/h kwa mazingira yetu na aina ya magari haifikiki .... Kidogo Premio, hizo nyingine kufika 180 km/h ni almost to impossible ama suicide.

Hebu 'tusimulie' tu huyo uliyemuona na IST/ Runx/ Premio kafuta visahani
 
Gari hazijatengenezwa kwa ajili yetu ndo maana tunaishia kununua mitumba ya mwaka 2000+, koo speed 180 or 240km/h utafikisha kulingana na barabara husika na uwezo wa dereva ku control gari ikiwa barabarani
 
IST anafuta kisahani? Nitashuka kabla ya kufika tuendako 😆 bora hata premio nitashika roho mkononi
Kuna mshikaji humu alitoa story. Walikua wanatoka Mwanza gari private na wana kadhaa. Ulikua usiku kwahiyo hamna trafick wala jam sana njiani. Kule mjini mjini ilikua poa wanacheka sana kwenye gari kufika maporini dere anafuta kisaani akipunguza sana 100 labda kuwe na tuta.

Aisee gari zima kimyaaa hamna mtu alielala wala anaeongea. Wale wengine wakawa wanachat. Wakakubaliana waombe wasimame kwaajili ya aja ndogo.

Dere anasimama nae anaenda jisaidia anarudi anakuta kwenye siti amekaa mwana mwingine. Kumbe wajamaa wameshakunaliana uyu fala anataka kutuua uyu. Akishuka tu agusi gari tena.

Walilala Dodoma. Wakati jamaa aliwaambia asubuhi chai wanaenda kunywa Dar.
 
Wakuu

Baada ya kupata bahati ya kuwemo katika magari aina tofauti tofauti, makubwa na madogo lakini kubahatika kuendesha umbali mrefu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kitu kimoja nimekuwa nikijiuliza, ni kwa nini magari ''karibia'' yanaonesha uwezo wa kwenda kasi kufikia mwendo wa 180 km/h?

Nilichogundua, mwendo kasi wa 180 km/h ni mkubwa sana sana sana, haufikiki, ni hatari na sio halisi hasa kwa aina ya magari yetu mengi ambayo ni mtumba huku barabara zetu nazo zikiwa sio rafiki.

Kwa mfano, magari ya cc 900 mpaka 2000cc haya kuwekewa mwendo kasi wa 180 km/h ni sahihi? Kwanini wasingeweka tu mfano 140 km/h? Hebu tuangalie uhalisia, katika mazingira yoyote yenye cc chini ya 1500 inaweza kweli kufika mwendo kasi wa let say 160km/h? Binafsi sidhani. Kwa gari maalumu za kwenda kasi na safari ndefu, ama zenye cc zaidi ya 2500 uwezekano unaweza kuwepo lakini kwa hizi nyingine, nahisi watengenezaji wanatulipisha gharama kubwa kwa kitu ambacho hakipo ama kwa kifupi wanatuibia.

Nini mtazamo wako?
Bugatti inaenda zaidi ya 400km/hr.
 
Tatizo 180km/h kwa mazingira yetu na aina ya magari haifikiki .... Kidogo Premio, hizo nyingine kufika 180 km/h ni almost to impossible ama suicide.

Hebu 'tusimulie' tu huyo uliyemuona na IST/ Runx/ Premio kafuta visahani
Mimi na jirani yangu tulikuwa tunaenda Moshi na IST yake mwaka juzi. Alifuta kisahani japo ni very risky.
 
Back
Top Bottom