Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Pandikizi lilikuwa linasubiri muda wa ku strike lakini likagonga mwamba sasa linarejea kwenda kubanana
Kuna tetesi kuwa wale wote waliohamia ccm kutoka upinzani watapigwa chini katika uchaguzi mkuu ujao kitu ambacho ni burudani tosha.
 
Petro E. Mselewa,
Nawashangaa sana hawa jamaa. Mbowe mwenyewe anatoka kanda ya kaskazini, hakugombea kule kwenye kanda, aliwaachia wengine. Sasa hawa wanaotaka kila mahali wawe viongozi sijui lengo lao ni nini. Ni muda tu, Mwambe ataondoka Chadema baada ya kubwagwa kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Taifa. Hata ningekuwa mimi mpiga kura singefanya majaribio ya kumpa mwana CCM aitwaye Mwambe. Upinzani siyo lelemama. Walizoea vya bure CCM. Angalia Sumaye anavyolilia mashamba yake aliyonyang'anywa na serikali baada ya kwenda Chadema.
 
Tundu Lisu anagombea umakamu mwenyekiti wakati anaishi Ulaya, fomu amejaza online, CHADEMA kuna vituko!
Kwani kujaza form online ni kosa? Waulize wanafunzi wa elimu ya juu wanajazaje form. Mambo ya hard copy ni ya kishamba siku hizi ndugu yangu.
 
Pandikizi lilikuwa linasubiri muda wa ku strike lakini likagonga mwamba sasa linarejea kwenda kubanana
Kuna tetesi kuwa wale wote waliohamia ccm kutoka upinzani watapigwa chini katika uchaguzi mkuu ujao kitu ambacho ni burudani tosha.
Sasa analalamika kukosa uenyekiti wa Chadema Taifa, Kwani uchaguzi tayari? Mbona bado? Si angesubiri aone kama hachaguliwi?
 
Tundu Lisu anagombea umakamu mwenyekiti wakati anaishi Ulaya, fomu amejaza online, CHADEMA kuna vituko!
We vipi kipi kituko mbona bili yangu ya maji nalipa online je kumbe tunalipa kwa vituko ama kweli akili ni nywele nawe una nywele zako
 
JokaKuu,
Nilichoelewa ni kuwa Sumaye ni mwanasiasa mwenye upeo mdogo sana kisiasa, hajui anachokifanya na wala hawezi kuficha kile alichopanga kwa siri kwenda kukifanya. Ni rahisi sana kujua hata anachokwenda kukiwaza.
 
Mtakapo mpa mwana ccm mwingine 2020 kupeperusha bendera baada ya uchaguzi mtakuja kumnanga tena. Mbona Nyarandu mmepa uongozi katoka ccm juzijuzi tu. Na huyu ama Membe ndo atapeperusha bendera yenu kama mgombea, mtapiga mbiu na vigelele kisha baada ya uchaguzi atapiga chini na mtakuja tena hivi hivi. what a shame.
 
Sumaye alitaka ATEULIWE kuwa mwenyekiti kanda ya pwani CHADEMA pia ATEULIWE kuwa mwenyekiti CHADEMA taifa.

Hakutaka kugombea, maana waliobaki mgombea pekee hakujushughulisha akijua atapita bila kupingwa, alipopigiwa kura na kuongoza kwa HAPANA, akakimbia akajiona satoshi, na akawa na conclusion ya matokeo ya uwenyekiti taifa.

Lakini cha kushangaza bado, anatamani kuwa mshauri wa CHADEMA hata baada ya kujitoa mwenyewe.
 
Kwa nini usiwalalamikie waliotunga kanuni za uchaguzi ndani ya CHADEMA?

Yaani Kanuni za uchaguzi zinawaruhusu kufanya hivyo halafu wakifanya unaanza kuwalalamikia?

Huoni wenye tatizo ni wale waliotunga Kanuni za Uchaguzi ndani ya CHADEMA ndio maana baadhi ya watu ndani ya CHADEMA wamejirundikia vyeo kama vile hakuna wanachama wengine wa kushika nafasi hizo!

Nashukuru umejikita kwenye udhaifu wa katiba, huenda unawazodoa cdm bila kujua katiba ya nchi ndio uchafu mtupu. Ni cheo gani ndani ya nchi hii kiongozi wake hateuliwi na rais? Ni kweli madaraka ya rais kuchagua viongozi karibu wote wa nchi ni sahihi na sio wendawazimu, hasa unapopata rais anayetumia nguvu kuliko akili na busara? Kuna tofauti na mtu kuwa mbunge na wakati huo Huo kuwa waziri?
 
MsemajiUkweli,
Mkuu chama ni imani na mara nyingi kanuni pamoja na kuwa zipo lakini pia kuna utamaduni wa chama.

Huo utamaduni ndio ukiuvunja wengine wanakuwa na mashaka kama wewe una nia njema kweli?

In kama CCM, hakuna kanuni ambayo Membe amevunja kukusudia kuchukua fomu kugombea nafasi ya kupeperusha bendera ya chama na kumtoa Magufuli.

Ukitazama hajavunja kanuni yeyote ya CCM hata ya TANU au ASP. Lakini kuna utamaduni umevunjwa, ndio maana kuna wasiwasi jee nia no njema?

Sumaye na Mwambe wametoka CCM ndani ya miaka 5 halafu ghafla wanakuja kuchukua fomu kwenye nafasi zao za zamani pia taifa. Na hapo hapo kuna fikra za hujuma za kutaka kuvuruga uchaguzi wa mwenyekiti Taifa kwa sababu CCM haimtaki Mbowe, jee hao watoka CCM juzi kwa nini wasitiliwe mashaka?
Hesabu zao in badly calculated na wameangukia pua.
 
Mimi najiuliza inamaana Fredrick Tuluwayi Sumaye hakujiandaa kushindwa? Maana ya uchaguzi ni Nini Sasa? Chadema hakuna kupita bila kupingwa! Labda arudi ccm
 
Hakuna wanasiasa waliwekeza pesa nyingi chadema Kama Lowasa na Sumaye.Sumaye kajenga Hadi makao.makuu ya Kanda Ofisi nzuri kuliko ya makao makuu.Lakini chadema hawana shukrani naye.Lowasa kaingiza wabunge wengi na madiwani Leo hi Lowasa anaonekana si lolote si chochote Chadema

Chadema shukrani hawana
 
Sumaye ameonyesha utoto mkubwa sana katika siasa.

Mbona alipokaribishwa CHADEMA alipewa nafasi akagombea alishinda bila kelele zozote.

Hata sasa hivi kachukua fomu karejesha na kapigiwa kura hazijatosha anaona siyo demokrasia ?

Huko alipotoka mbona hajawahi kutendewa haki katika uchaguzi wowote ule ?

..ni kweli walichomfanyia siyo kitu kizuri hata kidogo.

..lakini sumaye angejipa muda wa kutafakari kabla ya kuchukua uamuzi huu.

..hata ccm ambako aliondoka alifanyiwa mizengwe ktk chaguzi zaidi ya moja.
 
Back
Top Bottom