Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Hakuna wanasiasa waliwekeza pesa nyingi chadema Kama Lowasa na Sumaye.Sumaye kajenga Hadi makao.makuu ya Kanda Ofisi nzuri kuliko ya makao makuu.Lakini chadema hawana shukrani naye.Lowasa kaingiza wabunge wengi na madiwani Leo hi Lowasa anaonekana si lolote si chochote Chadema

Chadema shukrani hawana
Hiyo shukrani unayotaka wafanyiwe ENL na FTS ukiitazama kwa makini utagundua kuwa ni rushwa
 
Mzee Fredrick T. Sumaye na Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe waligombea Uenyekiti wa Kanda zao za Mashariki na Kusini. Kule Kanda ya Mashariki, Mzee Sumaye akiwa mgombea pekee wa Uenyekiti, alipata kura nyingi za HAPANA na hivyo kushindwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Kanda ya Mashariki.

Mbunge Mwambe naye aligombea Uenyekiti wa Kanda ya Kusini. Akazidiwa kura na Ndugu Mathew katika nafasi hiyo na hivyo kupoteza nafasi yake ya Uenyekiti wa Kanda ya Kusini aliyokuwa akiitetea. Mwambe yeye alizidiwa kura na Mathew kwenye boksi kwakuwa Kanda ya Kusini ilikuwa na mgombea zaidi ya mmoja wa Uenyekiti.

Mzee Sumaye na Mwambe wote walihamia CHADEMA wakitokea CCM. Wote waligombea Uenyekiti wa Kanda zao na ule wa Taifa wa CHADEMA mwaka huu (kabla ya leo Mzee Sumaye kujiweka pembeni kwenye uchaguzi huo na hata CHADEMA kwa ujumla wake). Kwanini waligombea nafasi mbili: kwenye Kanda zao na ile ya kitaifa?

Kwenye siasa kuna kushinda na kushindwa. Kwenye siasa kuna kuzidiana nguvu kiushawishi (wakati mwingine bila hujuma wala vitisho vyovyote). Wao walitaka vyote na sasa wanakosa vyote. Kwa jinsi mambo yalivyo, ni dhahiri Mwambe anakwenda kuzidiwa kura na Mbowe kwenye Uenyekiti CHADEMA Taifa. Naye sijui atakuja na kauli zipi na uamuzi gani.

Muda utatueleza.

Atajiondoa CDM na povu kibao kwamba kahujumiwa au kukoswakoswa kwa sumu!
 
Na huku kanuni zinakataza ilo..Maana kanuni zinasema lazma fomu ijazwe mtu akiwa nchini na kuwasilisha kwa mkono.


2020 Wanaccm tuchukue fomu kugombea uwenyekiti Taifa

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza!
 
Back
Top Bottom