Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Kwanini Sumaye na Mwambe waligombea kwenye Kanda zao na tena wanagombea Uenyekiti Taifa?

Kwa nini usiwalalamikie waliotunga kanuni za uchaguzi ndani ya CHADEMA?

Yaani Kanuni za uchaguzi zinawaruhusu kufanya hivyo halafu wakifanya unaanza kuwalalamikia?

Huoni wenye tatizo ni wale waliotunga Kanuni za Uchaguzi ndani ya CHADEMA ndio maana baadhi ya watu ndani ya CHADEMA wamejirundikia vyeo kama vile hakuna wanachama wengine wa kushika nafasi hizo!
vipi waliotunga kanuni za s/mitaa
 
Ndani ya CDM ni shwari, wanaoondoka waende salama.
Mwambe alishakalibishwa na Boss wa Lumumba hiyo haina siri.
Mzee wangu Sumaye sijui anamfuata Edo tunaangalia.
Ndio maana tuna imani na Mbowe kuongoza CDM!!
 
Nawashangaa sana hawa jamaa. Mbowe mwenyewe anatoka kanda ya kaskazini, hakugombea kule kwenye kanda, aliwaachia wengine. Sasa hawa wanaotaka kila mahali wawe viongozi sijui lengo lao ni nini. Ni muda tu, Mwambe ataondoka Chadema baada ya kubwagwa kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Taifa. Hata ningekuwa mimi mpiga kura singefanya majaribio ya kumpa mwana CCM aitwaye Mwambe. Upinzani siyo lelemama. Walizoea vya bure CCM. Angalia Sumaye anavyolilia mashamba yake aliyonyang'anywa na serikali baada ya kwenda Chadema.
hawakumnyang'anya wamemhifadhia, ili akamilishe mpango mkakati aliokuwa amepewa warudishe. Bahadi mbaya karata alizokua nazo ameanza kucheza majokel na yememuishia kabla game halijaisha.
 
Petro E. Mselewa,
Mizani zinaweza kutumika kupima uzani wao kwa chadema. Nisichofahmu ni kama mapenzi yao ni kwa maslahi yao au vinginevyo.
 
Sumaye na Mwambe ni wahanga wa “safisha safisha”. Hata itakuwa hivo kwa Nyalandu. Waliorejea CCM wengi walikuwa ni wale waliokuwa CCM kwanza. Hili lisisahaulike!!

Chadema wameona kuwa walikosea kuwakaribisha wanachama wa CCM mwaka 2015. Wamekubali kujisahihisha hata kama maana yake ni kuwatendea watu mambo yasiyo ya haki.

Walipaswa kueleza kwanini wanagombea nafasi mbili, je ni tamaa ya madaraka??

Walikuwa wameandaliwa wasikose kote. Hata hao wanaccm walioshinda kama kina Nyalandu ni wa kuwakalia vizuri. Ifike mahali cdm waache okota okota hasa hao wanaccm na kuwapa nafasi. Inatakiwa waweke kifungu kabisa, kama hujakaa cdm ndani ya miaka mitano mfululizo hakuna kupewa nafasi ya kugombea, na kama umetokea ccm ndio inabidi chujio liwe kali kabisa.
 
Pandikizi lilikuwa linasubiri muda wa ku strike lakini likagonga mwamba sasa linarejea kwenda kubanana
Kuna tetesi kuwa wale wote waliohamia ccm kutoka upinzani watapigwa chini katika uchaguzi mkuu ujao kitu ambacho ni burudani tosha.
Hivyo ndivyo wananvyo waza viongozi wa chama kinachotaka kujiongezea wanachama wapya?
Wanachama wapya lazima wasiwe wametokea chama kingine?

Kuna mambo tuyachukulie kwa uzito mkubwa sana na sio kishabiki au kitoto.
Kisa cha Mzee Sumaye kinajega taswira mbaya sana kwa mustakabali wa upinzani Tanzania, ukizingatia upinzani wanaenda kugawana wanachama 2020 na chaguzi zingine.

CC: JokaKuu
 
..ni kweli walichomfanyia siyo kitu kizuri hata kidogo.

..lakini sumaye angejipa muda wa kutafakari kabla ya kuchukua uamuzi huu.

..hata ccm ambako aliondoka alifanyiwa mizengwe ktk chaguzi zaidi ya moja.

Kura zimepigwa wazi na katika huo uchaguzi hakukuwa na fujo wala kificho chochote, hatukuona box la kura likitolewa nje ya kituo na kwenda kupunguzwa kura zake, je hapo alitakaje? Mkuu unataka kutekwa na hizi propaganda mfu? Kama kuna watu walishawishiwa wasimpigie kura na kweli hawakupigiwa hiyo ndio siasa na ndio ushindani. Ingekuwa waliokuwa wampigie kura walishikiwa bastola ili wasimpigie hapo sawa. Huyo mzee alizoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.

Hivi Sumaye alikuwa anautaka uwenyekiti wa cdm, amefungua matawi mangapi ya cdm nchi hii? Ni mchango gani ametoa tukaona kweli alikuja kujenga demokrasia na kukuza chama? Hakuwa na mchango wowote wala mvuto wowote wa kisiasa wenye faida dhahiri kwa chama. Akichafue cdm apendavyo, ila alichotumwa kukifanya cdm kimedoda, aende ACT TLP, au arudi ccm ndio wanamuhitaji.
 
Hivyo ndivyo wananvyo waza viongozi wa chama kinachotaka kujiongezea wanachama wapya?
Wanachama wapya lazima wasiwe wametokea chama kingine?

Kuna mambo tuyachukulie kwa uzito mkubwa sana na sio kishabiki au kitoto.
Kisa cha Mzee Sumaye kinajega taswira mbaya sana kwa mustakabali wa upinzani Tanzania, ukizingatia upinzani wanaenda kugawana wanachama 2020 na chaguzi zingine.

CC: JokaKuu
Taswira mbaya utaiona wewe. Dr. Slaa alitoka upinzani baada ya kuona Lowasa na Sumaye wamekuja upinzani na kusena hawezi kukaa meza moja na MAFISADI, na akajihapiza kama Sumaye alivyojihapiza leo. Baadae akateuliwa, no i mean akaandaliwa press conference na watu wa TISS (huyu wa leo sijui amendaliwa na nani, ila barua ilisambaa ikiwa na nembo ya taifa), akapitia mlango wa uhani kuingia ndani, baadae Lowasa akarudi alipo Slaa, sijasikia akitata kutoka tena huko alipo. Ujagundua kitu au dhamira yoyote?


MWAMBA TUVUSHE
 
Hivyo ndivyo wananvyo waza viongozi wa chama kinachotaka kujiongezea wanachama wapya?
Wanachama wapya lazima wasiwe wametokea chama kingine?

Kuna mambo tuyachukulie kwa uzito mkubwa sana na sio kishabiki au kitoto.
Kisa cha Mzee Sumaye kinajega taswira mbaya sana kwa mustakabali wa upinzani Tanzania, ukizingatia upinzani wanaenda kugawana wanachama 2020 na chaguzi zingine.

CC: JokaKuu

Cdm tunahitaji wanachama wapya na sio kubembeleza wasaka vyeo. Huyo Sumaye ambaye unaona ni sehemu ya watu wanaoitia cdm doa, alifungua matawi mangapi ya cdm? Cdm ni chama cha wanachama na sio sehemu ya kugaia wazee vyeo. Kama inabidi Sumaye abembelezwe ili cdm ipate wanachama hao sio wanachama bali watakuwa wachumba. Aende ccm ndio inadekeza wanachama kwakuwa imechokwa na wananchi inategemea mbeleko ya vyombo vya dola.

Ni kipi Sumaye kakileta, au wanachama gani ama ni hamasa ipi kaileta toka amekuja cdm? Kama ni mikutano ya kisiasa imezuiwa akiwepo na hajafanya lolote, kama ni chaguzi zinanajisiwa wazi wazi na wala hatujamwona akifanya lolote la maana kuondoa hali hiyo. Hivi majuzi chaguzi za serikali za mitaa zimenajisiwa na wala hatujaona mchango wake wowote kubadili hali ile. Sasa mtu huyo anataka madaraka ili iwe nini kwa mfano. Kama hao wanachama unaosema ni wa aina ya Sumaye acha wasiwepo.
 
Mwaka 2017 tulikaa pale Rose garden tukawa tunabishana na mmbea mwenzangu nikamwambia mbowe hatumuwez mana kapita humu tunamopita sisi asaivi
 
Sijui ni demokrasia ipi aliotaka ionekane ndani ya CHADEMA iliomuonyesha kuwa demokrasia ni kuchaguliwa tu na kuto kuchaguliwa siyo demokrasia.
 
Tundu Lisu anagombea umakamu mwenyekiti wakati anaishi Ulaya, fomu amejaza online, CHADEMA kuna vituko!

Unachangia hapa ili uonekane ni mjanja au unaishambulia cdm, kumbe ni mshamba fulani. Siku hizi kila kitu ni online, kuanzia kulipa Ankara za maji, umeme, malipo karibia yote ya serikali, Brela nk. Hapa ndio dunia ilipo. Kama bado unaishi kwenye dunia ya analogia wenzako walishatoka miaka mingi sana.
 
Unachangia hapa ili uonekane ni mjanja au unaishambulia cdm, kumbe ni mshamba fulani. Siku hizi kila kitu ni online, kuanzia kulipa Ankara za maji, umeme, malipo karibia yote ya serikali, Brela nk. Hapa ndio dunia ilipo. Kama bado unaishi kwenye dunia ya analogia wenzako walishatoka miaka mingi sana.
Hemu ifike sehemu muwe mnanielewa basi,nilishasema hivi kule CCM Kuna mtambo wa kuchakata akili za watu na operater wa ule mtambo ni Goodluck Mlinga mbunge wa Ulanga....alipata dharula Mlinga mtambo unashikiliwa na Lusinde Mara moja moja. Hemu mwangalie pole pole( chakubanga) walivyomchakata akili,hemu mwangalie Dr Bashiru walivyomchakata akili sipati picha wake za hawa jamaa wawili wanajisikieaje tangu waume zao wachakatwe akili.
 
Back
Top Bottom