Kwanini taarifa nyingi za miaka elfu iliyopita ni za kubuni au hazijulikani kiuhalisia? Je, kuna kizazi kilipotea?

Kwasababu kuna muda binadamu hakuwa na utashi wakuacha history,ujuzi wakuandika hakua nao,hata lugha ilikuwa patashika ni ishara tu.
wakati huo mission zao hazikuwa kuwaza kukuachia wewe historia wakati tu maisha yalikuwa mvurugano,myda wowote unaweza kuvamiwa na wanyama wakuue mi nikae niandike history nitafunwe..?

nafikiri pia mwanadamu anaenda kwa evolution yani uwezo unazidi kukua siku baada ya siku, sasahivi maarifa ya kuhifadhi taarifa yameimarika maradufu kiasi chakushangaza!.
ukute hata binadamu wa awali wanajua asili yetu kabisa ambayo hivi sasa hatuijui isipokuwa sasa hawakuweza kuhifadhi hizo taarifa!, kuna muda kweli bado binadamu alikuwa kwenye ombwe la sintofahamu ni sawasawa na mtoto mchanga ubongo wake kuanza kuhifadhi kumbukumbu vyema huchukua muda fulani wa makuzi ila kula anajua,kupumua anajua,na haja nyengine nyengine!.

chanzo chetu bado kinautata sana!
 
Unauliza za miaka efu mbali huko wakati kwenye waaasisi wa CCM tu kuna ubishani,waliioshiriki mapinduzi ya zanzibar kuna ubishani.
Picha ya safari ya nyerere UN iliwahi kuzua ubishani
Umeenda mbali mno mpwa
 
Unauliza za miaka efu mbali huko wakati kwenye waaasisi wa CCM tu kuna ubishani,waliioshiriki mapinduzi ya zanzibar kuna ubishani.
Picha ya safari ya nyerere UN iliwahi kuzua ubishani
Umeenda mbali mno mpwa
Haahaa hizi zinajulikana sana tu tena kwa dokumaa kabisa sema ni mambo ya siasa ndo yametamalaki apo. mwanasisasa haaminiki kivile ndugu.
 
Hivi kusema hapo kale, elimu ya maandishi na utunzaji kumbukumbu ilikuwa finyu, nitakuwa nimekosea?

Kwa mfano sisi Afrika, hasa Afrika ya mashariki, iko wapi historia yetu kabla ya ujio wa wakoloni?

Maana kwetu sisi inaonekana kama dunia ilianza karne ya 16, kabla yake ni giza totoro hakuna anayeelewa kutuhusu ni kama hatukuwepo kabisa.
 
kusema hapo kale, elimu ya maandishi na utunzaji kumbukumbu ilikuwa finyu, nitakuwa nimekosea
upo sawa kiongozi. sisi tulitegemea zaidi masimulizi. historia zikitunzwa vichwani mwa watu na wakisimuliana kwa vizazi hata vizazi. shida sasa akifa huyo mwenye historia shughuli inaishia apo.
 
upo sawa kiongozi. sisi tulitegemea zaidi masimulizi. historia zikitunzwa vichwani mwa watu na wakisimuliana kwa vizazi hata vizazi. shida sasa akifa huyo mwenye historia shughuli inaishia apo.
Binadamu ameanza kutumia maandishi kwa kuchelewa sana, miaka 3400 kabla ya Kristo ndio inakadiriwa Binadamu walianza kutumia maandishi
 
Kuna watu wanasemaga kuwa dunia ina maisha yapo millions of years ago ila hawakupi reference yoyote
Reference ni fossil evidence na miamba.
Kila mwamba una muda wake maalumu wa kujiunda na unatoa mionzi ya radioactive kulingana na umri wake,
Hakikisha unapeleka watoto wako shule wajifunze haya mambo.
 
Tulichagua kuamini watu waliokataa habari za miaka 2000 iliyopita na kuamini habari zao za miaka Milion 60 iliyopita😂.

OBEY ( tricknology ) ipo kukuswaga Kama ng'ombe.
 
Usa wanapenda sana kitunza malikale,
Haat sio mbaya kama wanajua matumizi kama kufanyia matambiko,
 
Achana na taarifa za miaka buku ilopita,wewe binafsi ukiulizwa taarifa zako za miaka 10 ilopita utatoa mimacho tu.

Taarifa zisipotunzwa ktk maandishi/sauti ni rahisi kupotea.
 
Unauliza za miaka efu mbali huko wakati kwenye waaasisi wa CCM tu kuna ubishani,waliioshiriki mapinduzi ya zanzibar kuna ubishani.
Picha ya safari ya nyerere UN iliwahi kuzua ubishani
Umeenda mbali mno mpwa
Kwamba ile safari ni geresha TU 😂
 
Mfano ,mimi nikupe taarifa zangu na wewe umpe mwingine na mwingine na mwingine , je hizo taarifa zitakua sawa na mtu wa kwanza kuzipata?
Taarifa zako haziwi sahihi, lakini ukipewa taarifa ya Muumba wako na akiahidi atailinda basi itakuwa sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…