Kwanini taarifa nyingi za miaka elfu iliyopita ni za kubuni au hazijulikani kiuhalisia? Je, kuna kizazi kilipotea?

Kwanini taarifa nyingi za miaka elfu iliyopita ni za kubuni au hazijulikani kiuhalisia? Je, kuna kizazi kilipotea?

Uwepo wa wewe na mimi ni ushahidi tosha kuwa dunia imekaliwa na binadam kwa MUDA WOTE tokea alipoumbwa binadam wa kwanza.

Kama dunia imekuwa na watu muda wote maana yake watu hao walikuwa wakisimuliana habari za matukio yaliyokuwa yanatokea wkt wao wakiwepo na habari hizi waliwapasia vizazi vyao ikaendeleea ivyo hata kwa vizazi vya leo hii.

Sasa mbona leo hii habari nyingi za matukio ya miaka elfu uko nyuma ni kama za kubuni au za watu kuhisi? Mfano mzuri ni maandiko ya vitabu vitakatifu. bado kuna mengi tu ya humo yanabishaniwa hata leo hii juu ya usahihi wake.

Inakuwaje bado kuna habari zisizo hakika wkt tunajua mwanadam amekuwepo wakati wote? Je, inawezekana kuna yamebuniwa tu na kundi au watu fulani tu kwa faida yao? Au wakuu nyinyi mnaonaje?

Tia neno hapa.
Kwanza kabisa, elewa kuwa kitabu kitakatifu hata kimoja kilicholindwa isipokuwa Qur'an pekee.

Hakuna zaidi ya hicho kilichohifadhiwa mioyoni mwa watu wengi duniani, kinachosaomwa sana bila hata ya kukifunguwa na mpaka leo kipo kama kilivyoteremshwa.
 
Sisi wamatumbi weusi tunapuuzia historia yetu ingawa ipo, tusiposituka na kuiandika kama huyu babu wa Lindi tumekwisha :

Kwa undani :

Toka maktaba:

Simulizi za Mjukuu wa Mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga wa maeneo ya Wamachinga Pwani ya
Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini
Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Mfano Ni stori za mazimwi ambazo tumesimuliwa Kama hadithi lkn zinaukweli wake. Watoto wa 2000 watadhani Ni za kubuni
 
Wamatumbi, wabembe n.k tuandike na kuhifadhi historia yetu kama jamii zingine zinazosimulia pia maandiko ya zaidi ya milenia tatu :

22 September 2023
UN HQ, New York

Hotuba mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA : Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu 2023.


View: https://m.youtube.com/watch?v=kNH85jgzJ0Y

Asante Mheshimiwa Rais!(Wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa)

Mabibi na mabwana, zaidi ya milenia tatu zilizopita, kiongozi wetu mkuu Musa, alihutubia watu wa Israeli walipokuwa karibu kuingia katika nchi ya ahadi. Alisema wangekuta milima yao miwili ikitazamana. Mlima Gerizimu, mahali ambapo baraka kubwa ingetangazwa, na Mlima Ebali, mahali pa laana kuu.


Musa alisema kwamba hatima ya watu ingeamuliwa na uchaguzi waliofanya kati ya baraka na laana. Chaguo lile la enzi ya Musa, limekuwa likijirudia enzi na enzi, si kwa watu wa Israeli pekee. Lakini kwa wanadamu wote. Tunakabiliwa na chaguo kama hilo leo. Chaguo letu litaamua ikiwa tunafurahia baraka za amani ya kihistoria, ya mafanikio na matumaini yasiyo na mipaka, au tutapata laana ya vita vya kutisha vya ugaidi na kukata tamaa.

Nilipozungumza mara ya mwisho kwenye jukwaa hili hili la UNGA miaka mitano iliyopita, nilionya kuhusu madhalimu wa Tehran. Wamekuwa ni laana, laana kwa watu wao wenyewe, kwa eneo letu, kwa ulimwengu mzima. Lakini wakati huo, nilizungumza pia kuhusu baraka kubwa ambayo ningeweza kuona kwenye upeo wa macho.

Hivi ndivyo nilivyosema. Nanukuu: "Tishio la kawaida la Iran limeifanya Israeli na nchi nyingi za Kiarabu kuwa karibu zaidi kuliko hapo awali katika urafiki ambao sijawahi kuuona maishani mwangu."

Nilisema: “Siku ingefika hivi karibuni ambapo Israeli ingeweza kupanua amani nje ya Misri na Jordan hadi kwa majirani wengine Waarabu.” Mwisho wa kunukuu.

Sasa, katika mikutano isiyohesabika na viongozi wa dunia, nilitoa hoja kwamba Israeli na mataifa ya Kiarabu yalishiriki maslahi mengi ya pamoja, na kwamba niliamini kwamba maslahi haya mengi ya pamoja yangeweza kuwezesha mafanikio ya amani pana katika eneo letu la Mashariki ya Kati

Makofi

Asante (kwa makofi) . Naam, mnanipongeza sasa kwa makofi . Lakini wakati ule, wengi walipuuzia matumaini yangu kudhani kuwa ni ndoto za kufikirika. Kukata tamaa kwenu kulitokana na robo karne ya nia ya kuwepo kupatika amani , na lakini ikashindikana. Na kwanini amani ilifeli? Kwani kulikuwepo nia njema? Kwanini siku zote walikutana na kushindwa? Kwa sababu yaliegemezwa kwenye wazo moja la kwamba tusipohitimisha kwanza makubaliano ya amani na Wapalestina, hakuna nchi nyingine ya Kiarabu ambayo ingerekebisha uhusiano wake na Israeli.



Kwa muda mrefu nimetafuta kufanya amani na Wapalestina. Lakini pia ninaamini kwamba hatupaswi kuwapa Wapalestina kura ya turufu ya veto juu ya mikataba mipya ya amani na mataifa ya Kiarabu. Wapalestina wanaweza kufaidika sana na amani pana zaidi. Wanapaswa kuwa sehemu ya mchakato huo, lakini hawapaswi kuwa na kura ya turufu ya veto juu ya mchakato huo.


Na pia ninaamini kwamba kufanya amani na mataifa mengi ya Kiarabu kungeongeza matarajio ya kufanya amani kati ya Israeli na Wapalestina. Tazama, Wapalestina ni 2% tu ya ulimwengu wa Kiarabu. Maadamu wanaamini kwamba 90% nyingine itabaki katika hali ya vita na Israeli, umati huo mkubwa, ulimwengu huo mkubwa wa Kiarabu unaweza hatimaye kutumika kuharibu taifa la Wayahudi.

Kwa hiyo Wapalestina watakapoona kwamba sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiarabu imejipatanisha na dola ya Kiyahudi, wao pia, watakuwa na uwezekano mkubwa wa kuachana na dhana ya kuiangamiza Israel, na hatimaye kuikumbatia njia ya amani ya kweli.



Sasa, kwa miaka mingi, mtazamo wangu wa amani ulikataliwa na wale walioitwa wataalamu wabobezi. Naam, walikuwa na makosa. Chini ya mtazamo wao, hatukuunda mkataba mmoja wa amani kwa robo karne. Walakini, mnamo 2020, chini ya njia ambayo nilitetea, tulijaribu kitu tofauti. Na kwa muda mfupi, tulipata mafanikio ya kushangaza. Tuliafiki mikataba minne ya amani - tukifanya kazi na Marekani, Israel ilitengeneza mikataba minne ya amani, katika muda wa miezi minne, na nchi nne za Kiarabu - Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco.

Makubaliano ya Abraham Accord yalikuwa msingi wa historia. Na leo, sote tunaona baraka za mapatano hayo. Biashara na uwekezaji na washirika wetu wapya wa amani inashamiri. Mataifa yetu yanashirikiana katika nyanja za biashara, nishati, maji, kilimo, madawa, mabadiliko ya hali hewa, na nyanja zingine nyingi. Takriban Waisraeli milioni moja wametembelea Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kila siku, Waisraeli wanaokoa muda na pesa kwa kufanya jambo ambalo hawakuweza kufanya kwa miaka 70 - wanaruka juu ya Rasi ya Arabia bila vikwazo hadi maeneo ya Ghuba, India, Mashariki ya Mbali na Australia.

Mikataba ya Abraham Accord ilileta badiliko jingine kubwa. Iliwaleta Waarabu na Wayahudi karibu zaidi. Tunaiona katika harusi za mara kwa mara za Kiyahudi huko Dubai, katika kuwekwa wakfu kwa shule ya Torati katika sinagogi huko Bahran. Katika wageni wakimiminika kwenye Jumba la Makumbusho la Uyahudi wa Morocco na Casablanca. Tunaiona katika masomo ambayo yanatolewa kwa wanafunzi wa Kiarabu kuhusu historia ya Maangamizi makubwa ya holocaust yaliyofanywa wakati wa Ujerumani ya Hitler katika mitaala ya shule za UAE.


Hakuna shaka. Makubaliano ya Abraham Accord yalitangaza mapambazuko ya enzi mpya ya amani.

Lakini ninaamini kwamba tuko kwenye kilele cha mafanikio makubwa zaidi - amani ya kihistoria kati ya Israel na Saudi Arabia. Amani kama hiyo itasaidia sana kumaliza mzozo wa Waarabu wa Israeli. Itahimiza mataifa mengine ya Kiarabu kurekebisha uhusiano wao na Israeli. Itaongeza matarajio ya amani na Wapalestina. Itahimiza mapatano mapana kati ya Uyahudi na Uislamu, kati ya Jerusalemu na Makka, kati ya uzao wa Isaka na uzao wa Ishmaeli. Hizi zote ni baraka kubwa sana.

Wiki mbili zilizopita, tuliona baraka nyingine zikiibuka. Katika mkutano wa G20, Rais Biden Waziri Mkuu Modi na viongozi wa Ulaya na Waarabu walitangaza mipango ya ukanda maalum wa ushoroba ambao utaunganisha rasi (Peninsula) ya Arabia na Israeli. Itaunganisha India na Ulaya na njia za meli baharini, mitandao ya reli, mabomba ya nishati, nyaya za mawasiliano fiber optic.


Ushoroba maalum (corridor) katika ukanda huu utawezesha kuondoa vituo vya ukaguzi vya baharini, barabarani, ktk reli na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya bidhaa, mawasiliano na nishati kwa zaidi ya watu bilioni 2.

Ni mabadiliko gani ya kihistoria zaidi ya haya kwa nchi yangu. Unaona, ardhi ya Israeli iko katika njia panda kati ya Afrika, Asia na Ulaya. Na kwa karne nyingi, nchi yangu ilivamiwa mara kwa mara na falme geni za mbali katika kampeni zao za uporaji na kutawala nchi za mbali. Lakini leo, tunapobomoa kuta za uadui, Israeli inaweza kuwa daraja la amani na ustawi wa kiuchumi na biashara kati ya mabara haya.


Amani kati ya Israel na Saudi Arabia itaunda Mashariki ya Kati mpya.

Ili kuelewa ukubwa wa mageuzi ambayo tunatafuta kuendeleza, ngoja nikuonyeshe ramani ya Mashariki ya Kati mnamo 1948, mwaka ambao Israeli ilianzishwa. Hapa kuna Israeli mnamo 1948. Ni kanchi kadogo, kilichotengwa, iliyozungukwa na ulimwengu wa Kiarabu wenye uadui.

Katika miaka yetu saba ya kwanza, tulifanya amani na Misri na Jordan. Na kisha mnamo 2020, tulifanya mapatano ya Abraham Accord - amani na nchi zingine nne za Kiarabu. Sasa angalia nini kinatokea tunapofanya amani kati ya Saudi Arabia na Israel. Mashariki ya Kati nzima inabadilika. Tunabomoa kuta za uadui. Tunaleta uwezekano wa ustawi na amani katika eneo hili lote. Lakini pia tunafanya jambo lingine.


Unajua, miaka michache iliyopita, nilisimama hapa na kalamu kuweka alama nyekundu katika ukanda wa Mashariki ya Kati kuonyesha laana, laana kuu, laana ya Iran ya nyuklia. Lakini leo, sasa, ninaleta alama hii kuonyesha baraka kuu, baraka ya Mashariki ya Kati mpya, kati ya Israeli, Saudi Arabia na majirani zetu wengine.

Hatutaondoa tu vikwazo kati ya Israel na majirani zetu, tutajenga ukanda mpya wa amani na ustawi unaounganisha Asia, kupitia UAE, Saudi Arabia, Jordan, Israel, hadi Ulaya. Haya ni mabadiliko ya chanya, mabadiliko makubwa. Alama nyingine ya historia.


Sasa, wakati ukanda wa amani Mashariki ya Kati upanuka, ninaamini kwamba njia ya kweli kuelekea amani ya kweli na majirani zetu wa Palestina inaweza hatimaye kupatikana. Lakini kuna tahadhari izingatiwe. Inapaswa kusemwa hapa, kwa uwazi na nguvu. Amani inaweza kupatikana tu ikiwa umebebwa na ukweli. Haiwezi kutegemea propaganda za uwongo. Haiwezi kuegemezwa kwenye chuki za kusambaza kashfa zisizo na mwisho kwa watu wa Kiyahudi.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas lazima akome kueneza propaganda na njama za kutisha dhidi ya Wayahudi katika Taifa la Kiyahudi. Narudia, nasisitiza , hivi karibuni Mahmoud Abbas alisema kwamba mtawala imla Hitler wa Ujerumani hakuwa anachuki za kuwasakama wayahudi (antisemite) - huwezi kufanya kampeni hizi . Lakini alifanya hivyo. Alisema hivyo.


Na Utawala wa Palestina lazima uache kuwatukuza magaidi, waache sera yake ya kihuni ya kuwafadhili kwa kulipa pesa kwa magaidi wa Kipalestina, kwa ajili ya mauaji ya Wayahudi. Haya yote ni ya kuchukiza, lazima njama hizi zikome ili amani itawale

Na chuki na propaganda hasi dhidi ya Wayahudi lazima zikataliwe popote zinapoonekana, iwe upande wa kushoto au wa kulia, iwe katika kumbi za vyuo vikuu au katika kumbi za Umoja wa Mataifa. Ili Amani idumu, Wapalestina lazima waache kutema chuki kwa Wayahudi, hatimaye wajipatanishe na taifa la Kiyahudi. Kwa hilo simaanishi tu kuwepo kwa taifa la Kiyahudi, bali kwa haki ya watu wa Kiyahudi kuwa na haki ya kiasili kuwepo katika nchi yao ya kihistoria - ardhi ya Israeli.


Na niwaambie, watu wa Israeli wanatamani amani kama hii. Natamani amani kama hii. Wakati nikiwa mwanajeshi kijana, zaidi ya nusu karne iliyopita, askari wenzangu na mimi katika vikosi maalum vya Israeli tulikabili hatari za kufa katika nyakati nyingi kwenye medani nyingi za vita, kutoka kwenye maji ya uvuguvugu ya Mfereji wa Suez, hadi miteremko iliyoganda theluji ya Mlima Hermoni, kutoka nyuma ya Mlima Hermoni. Mto Jordan hadi lami za njia za kuruka ndege uwanja wa ndege wa Beirut Lebanon.

Uzoefu niliopata nikiwa askari mstari wa mbele vitani na mambo mengine njliyoyaona kwa macho yalinifundisha gharama ya vita. Askari mwenzangu aliuawa mita chache karibu yangu na mwingine alikufa mikononi mwangu. Nilimzika kaka yangu mkubwa. Wale wenzangu ambao binafsi wamewahi teseka katika laana ya vita wanaweza kuthamini vyema baraka za amani.


Sasa, kuna vikwazo vingi kwenye njia ya amani. Kuna vikwazo vingi, kwa njia ya makubaliano ya Abraham Accord ya amani ambayo nimeeleza hivi punde. Lakini nimejitolea kufanya kila niwezalo ili kushinda vikwazo hivi, kutengeneza mustakabali bora wa Israeli, na watu wetu wote, watu wote katika eneo letu.

Siku mbili zilizopita, nilijadili maono haya ya amani na Rais Joe Biden. Tunashiriki matumaini sawa kwa kile kinachoweza kupatikana. Na ninathamini sana kujitolea kwake kuchangamkia fursa hii ya kihistoria. Marekani ni mdau muhimu sana katika juhudi hizi. Na kama vile tulivyofanikisha Makubaliano ya Abraham, na uongozi wa Rais Trump, naamini tunaweza kupata amani na Saudi Arabia, na uongozi wa Rais Biden.

Kwa kufanya kazi pamoja na uongozi wa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa ufalme wa Saudia , tunaweza kuunda mustakabali wa baraka kubwa kwa watu wetu wote.


Sasa, mwajua, mabibi na mabwana, mwajua, kuna nzi katika mafuta haya safi. Kwa sababu uwe na uhakika, mahafidhina wakereketwa wanaotawala Iran watafanya kila wawezalo kuzuia amani hii ya kihistoria. Iran inaendelea kutumia mabilioni ya fedha kuwapa washirika wake wa ugaidi. Inaendelea kupanua hema zake za ugaidi katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Amerika Kusini, hata Amerika Kaskazini.

Walijaribu hata kumuua waziri wa mambo ya nje wa Amerika. Walijaribu hata kumuua mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani. Hii inakuambia yote unayohitaji kujua kuhusu nia ya mauaji ya Iran, na asili ya mauaji ya Iran.


Iran inaendelea kutishia njia za meli za kimataifa baharini , kuwashikilia raia wa kigeni kwa ajili ya kuwakomboa kwa dau la fedha na kujihusisha na kuficha mipango ya kuwa na silaha za nyuklia. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mgambo wake wauaji wameua mamia na kuwatia mbaroni maelfu ya raia jasiri wa Iran.


Ndege zisizo na rubani na programu za makombora za Iran zinatishia Israel na majirani zetu wa Kiarabu na ndege zisizo na rubani za Iran zimeleta na kuleta kifo na uharibifu kwa watu wasio na hatia nchini Ukraine.


Hata hivyo uchokozi wa utawala huo wa Iran kwa kiasi kikubwa unakabiliwa na hali ya kutojali katika jumuiya ya kimataifa. Miaka minane iliyopita, madola ya Magharibi yaliahidi kwamba iwapo Iran itakiuka makubaliano ya nyuklia, vikwazo hivyo virejeshwa. Kweli, Iran inakiuka makubaliano. Lakini vikwazo havijarejeshwa.


Kuzuia mipango kificho ya hatari ya nyuklia ya Iran. Sera hii ya kujifanya hamnazo ya mataifa na umoja wa mataifa lazima ibadilike . Vikwazo lazima virudishwe. Na zaidi ya yote, Iran lazima ikabiliane na tishio la kushughulikiwa .* Maadamu mimi ni Waziri Mkuu wa Israeli, nitafanya kila niwezalo kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia.


Vile vile, tunapaswa kuunga mkono wanawake na wanaume jasiri wa Iran wanajitokeza kupinga utawala Tehran, ambao wanatamani uhuru. Ambao wameamka kwa ujasiri kwenye vijia vya Tehran na miji mingine ya Irani na wanakabiliwa na kifo. Ni watu wa Iran tuwaunge mkono, sio wakandamizaji wao, maana wamejitolea kupiga ukandamizaji hivyo ni washirika wetu wa kweli kwa mustakabali bora.

Mabibi na mabwana, kama wakati wetu ujao utakuwa wa baraka au laana itategemea pia jinsi tunavyoshughulikia labda maendeleo muhimu zaidi ya wakati wetu. Kuongezeka kwa akili ya bandia AI - Artificial intelligence.

Mapinduzi ya AI yanaendelea kwa kasi kubwa ya kama spidi ya mwanga wa radi. Ilichukua karne nyingi kwa ubinadamu kufikia mapinduzi ya kilimo. Ilichukua miongo kadhaa kufikia mapinduzi ya viwanda. Tunaweza kuwa na miaka michache tu ya kukabiliana na mapinduzi ya AI.


Hatari ni kubwa, na ziko mbele yetu. Kuvurugwa kwa demokrasia, ubongo wetu kuchukuliwa na akili bandia , nafasi za kazi kupunguzwa, kuongezeka kwa uhalifu, na udukuzi wa mifumo yote inayowezesha maisha ya kisasa. Bado kinachosumbua zaidi, ni mlipuko unaowezekana wa vita vinavyoendeshwa na Akili Bandia -AI ambavyo vinaweza kufikia kiwango kisichoweza kufikiria.


Na nyuma ya hii labda kuna tishio kubwa zaidi, kilichokuwa simulizi za kusadikika ya mambo ya hadithi za kisayansi, kwamba mashine za kujifundisha zinaweza kudhibiti wanadamu, badala ya sisi watu kudhibiti mashine. Mataifa yanayoongoza duniani, hata yawe na ushindani, lazima yashughulikie hatari hizi. Ni lazima tufanye hivyo haraka. Na lazima tufanye hivyo pamoja. Lazima tuhakikishe kwamba zama za Akili Bandia ya AI utopia haigeuki kuwa tishio la AI.


Tuna mengi ya chanya ya kupata kupitia Akili Bandia . Hebu wazia baraka za hatimaye kubaini muundo wa kanuni za vinasaba chembe za urithi (gene), kurefusha maisha ya mwanadamu kwa miongo kadhaa, na kupunguza sana magonjwa ya uzee. Hebu fikiria huduma ya afya inayolengwa kulingana na muundo wa maumbile ya vinasaba vya kila mtu, na dawa ya kutabiri ambayo huzuia magonjwa muda mrefu kabla ya kutokea. Wazia roboti zinazosaidia kuwatunza wazee. Hebu fikiria mwisho wa msongamano wa magari, huku magari yanayojiendesha yakiwa ardhini, chini ya ardhi na angani. Hebu wazia elimu ya ziada kujifunza kibinafsi ambayo inakuza uwezo kamili wa kila mtu katika maisha yake yote.


Hebu fikiria ulimwengu wenye nishati safi isiyo na kikomo, na maliasili kwa mataifa yote. Hebu fikiria kilimo cha kisasa zaidi na viwanda vya kiotomatiki vinavyotoa chakula na bidhaa kwa wingi vinavyomaliza kabisa tatizo la njaa na upatikanaji chakula.


Najua huu maneno haya unayosikia ni kama mistari ya wimbo wa mwanamuziki nguli mtunzi John Lennon. Lakini yote yanaweza kutokea.


Hebu subiri kwa punde waza , fikiria kwamba tunaweza kufikia mwisho wa uhaba wa kila kitu!. Kitu ambacho kimeshindikana katika hali ya ubinadamu ndani ya historia yote. Haya Yote ni ndani ya uwezo wetu. Na hapa kuna kitu kingine ambacho tunaweza kufikia. Kwa matumizi sahihi ya Akili Bandia- AI, tunaweza kuchunguza mbingu za mbali kuliko hapo awali na kupanua tunachofahamu zaidi ya sayari yetu ya bluu.


Kwa uzuri au ubaya, maendeleo ya Akili Bandia - AI yataongozwa na mataifa machache, na nchi yangu Israeli tayari iko kati yao. Kama vile mapinduzi ya kiteknolojia ya Israeli yalivyoupa ulimwengu ubunifu wa kustaajabisha, nina imani kwamba Akili Bandia AI iliyotengenezwa na Israeli itasaidia tena wanadamu wote.


Natoa wito kwa viongozi wa dunia kuja pamoja ili kuchagiza mabadiliko makubwa yaliyo mbele yetu. Lakini kufanya hivyo kwa njia ya kuwajibika na ya kimaadili. Lengo letu lazima liwe zaidi kulinda kuwa Akili Bandia- AI inaleta uhuru na sio kiduchu, inazuia vita badala ya kuvianzisha na kuhakikisha kuwa watu wanaishi maisha marefu, yenye afya, yenye tija na amani. Ni ndani ya uwezo wetu.


Na tunapotumia nguvu za Akili Bandia -AI, ngoja kwanza tukumbuke kila wakati thamani isiyoweza kubadilishwa ya ubinadamu na hekima ya mwanadamu. Hebu tuthamini na undani wa uwezo wa huruma, ambao hauwezi kuchukuliwa na nafsi ya Akili Bandia AI


Maelfu ya miaka, Musa aliwapa wana wa Israel chaguo lisilo na wakati na la ulimwengu wote. Angalieni, nimesema mbele yenu hivi leo, baraka na laana. Na tuchague kwa busara kati ya laana na baraka zinazosimama mbele yetu leo. Wacha tutumie azimio letu na ujasiri wetu kukomesha laana ya Iran ya nyuklia na kurudisha nyuma ushabiki na uchokozi wake.

Hebu tulete baraka za Mashariki ya Kati mpya ambayo itabadilisha ardhi ambayo iliwahi kuandikwa kwa migogoro na machafuko, kuwa uwanda wa ustawi na amani. Na tuepuke hatari za Akili Bandia - AI kwa kuchanganya utu, nguvu za akili ya binadamu na mashine, ili kuleta mustakabali mzuri wa ulimwengu wetu katika wakati wetu, na kwa siku zote za mbele. Asante.


*Source : FULL TEXT: Benjamin Netanyahu's 2023 UN General Assembly Speech
 
Uwepo wa wewe na mimi ni ushahidi tosha kuwa dunia imekaliwa na binadam kwa MUDA WOTE tokea alipoumbwa binadam wa kwanza.

Kama dunia imekuwa na watu muda wote maana yake watu hao walikuwa wakisimuliana habari za matukio yaliyokuwa yanatokea wkt wao wakiwepo na habari hizi waliwapasia vizazi vyao ikaendeleea ivyo hata kwa vizazi vya leo hii.

Sasa mbona leo hii habari nyingi za matukio ya miaka elfu uko nyuma ni kama za kubuni au za watu kuhisi? Mfano mzuri ni maandiko ya vitabu vitakatifu. bado kuna mengi tu ya humo yanabishaniwa hata leo hii juu ya usahihi wake.

Inakuwaje bado kuna habari zisizo hakika wkt tunajua mwanadam amekuwepo wakati wote? Je, inawezekana kuna yamebuniwa tu na kundi au watu fulani tu kwa faida yao? Au wakuu nyinyi mnaonaje?

Tia neno hapa.

Miaka 1,000 nyuma umeenda mbali sana. Leo nimemsikiliza Godbless Lema anaongea kuhusu chaguzi za serikali za mitaa.

The mighty Lema just finished on the wire. A press conference. Going on and on about local governments elections, with gratuitous Biblical references of course, and calls for religious leaders to get involved in politics.

But that's not what I am here for.

I am here for the innumeracy. We talk a lot about illiteracy, not nearly enough about innumeracy.

We are such innumerates as a people. Lema ana dispute participation figures, anasema "75% ya million 31 ni kama million 28 hivi".


Yani kashindwa kufanya mental math ya haraka ya 32 - (32÷4) kupata 75% ya 32 kuwa 24 na 75% ya 31 just under 24.

Zaidi, why get into the minutia of numeric exactitude, or even estimation, if your answer is this far off? Kwa nini mtu asiseme tu 75% ya million 31 bila kujidhalilisha kuwa hajui hesabu rahisi za kutafuta percent?

Nakumbuka siku ya kwanza nam blast Lema ilikuwa ni yeye kutumia hizi hesabu za kutungatunga. Alisema rate ya divorce US ni kama 90%. Nikamwambia you need to double check your figures.

Naona bado hajaacha.

Jana kuna mtu hapa JF kasema GDP ya Kenya ni mara mbili ya ya Tanzania. Wakati actually ni around mara 1.48. But do we care? Ukimbana mtu utaambiwa "Ndiyo hiyo hiyo, si umeelewa?"

I know we dont walk with calculators, and we are all not capable of mental math. But could we at least refrain from throwing around exact figures, or even estimations, when we do not do the least bit of thinking about being at least close to the truth?

Especially at press conferences for all the world to see our innumeracy?

Do Tanzanians notice or even care about these things?

Sasa ukiongelea miaka 1,000 iliyooita, umeenda mbali sana.

Hatuna uadilifu wa taarifa hata za leo.
 
Kwamba ile safari ni geresha TU 😂
Kuna wakina mama walipiga nae picha wamevaa vilemba,Yeriko nyerere akasema ni masister wa kanisa katoliki,mohamed said akasema ni wakina mama wa pwani wa miaka ile
 
Reference ni fossil evidence na miamba.
Kila mwamba una muda wake maalumu wa kujiunda na unatoa mionzi ya radioactive kulingana na umri wake,
Hakikisha unapeleka watoto wako shule wajifunze haya mambo.
Nafikir wewe kwanza ulitakiwa kwenda shule vizuri maana hata swali hujajibu wala kulielewa umeruka ruka ukajieleza badala kujibu swali
 
Kuna wakina mama walipiga nae picha wamevaa vilemba,Yeriko nyerere akasema ni masister wa kanisa katoliki,mohamed said akasema ni wakina mama wa pwani wa miaka ile
Ndio maana jamaa ,aliamua serikali yake kuwa ya usiri sana, coz anayajua aliyoyafanya
 
Fasihi simulizi ni shida sana. Mnavyozidi kusimuliana maana inapotea.

Fasihi andishi imegubikwa na siri na kufichwa fichwa sana. Kuna siri nyingi za dunia zimekaliwa na baadhi ya mataifa.
 
Kwanza kabisa, elewa kuwa kitabu kitakatifu hata kimoja kilicholindwa isipokuwa Qur'an pekee.

Hakuna zaidi ya hicho kilichohifadhiwa mioyoni mwa watu wengi duniani, kinachosaomwa sana bila hata ya kukifunguwa na mpaka leo kipo kama kilivyoteremshwa.
kiongoz kama kuna any proof wa haya uliyoandika tuwekee hapa tujifunze km hutajali
 
Habari na elimu muhimu za zamani zimefichwa na watu wachache, wanazitumia kwa manufaa yao.

Mfano Library of Alexander (Egypt) ilichomwa moto na wakaficha baadhi ya vitabu.

Mfano mwingine ni stargate iliyokuwa imefichwa na sadam husein, USA walipo vamia direct walienda kuichukua na kuipeleka kwao kwa matumizi yao binafsi.
Mkuu,ebu nitoe tongotongo hapa.hiyo Stargate ni nini?
 
Mkuu,ebu nitoe tongotongo hapa.hiyo Stargate ni nini?
Stargate ni Portal au njia ya kuhama dimension moja kwenda nyingine.

Universe ina dimension tatu tofauti:-

•Angelic (Ulimwengu wa malaika)
•Demonic( Ulimwengu wa majin) na
Ulimwengu wa binadamu.
 
ushahidi mkubwa ni wa mtu kuona tukio live na kisha mtu uyo kusimulia uzao wake au jamii yake. nje ya hapo habari husika inakuwa ni ya kubumba tu.
Hata uzao wake unaweza usiamini ukweli wa muhusika,....yamenikuta hayo
 
Inawezekana kizazi kijacho kitakachozaliwa kuanzia mwaka 3000 kikawa na vichwa vitatu, na wao kujiona wakawaida tu.
kuna theory tuliwahi discuss na mwalimu wangu wa biology advance,...juu ya kuongezeka kwa race duniani,...kwa njia ya mutation na interracial marriage,....fikiria machotara wakianza kuzaliana wao kwa wao ndani miaka kadhaaa?🤔🤔
 
kuna theory tuliwahi discuss na mwalimu wangu wa biology advance,...juu ya kuongezeka kwa race duniani,...kwa njia ya mutation na interracial marriage,....fikiria machotara wakianza kuzaliana wao kwa wao ndani miaka kadhaaa?🤔🤔
Chotara wa kiarabu na chotara wa kihindi atatokea nini?
 
Back
Top Bottom