Kwanini taarifa za kifo cha Mpishi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais zimefichwa?

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
346
Reaction score
2,968
Ofisi ya Makamu wa Rais ilitangaza msiba wa mtumishi wake, Bi. Kulwa L. Ngusa, aliyekuwa akihudumu kama Mpishi katika Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kulwa alifariki dunia Agosti 21, 2026, majira ya saa 12:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na familia ya marehemu. Uongozi na wafanyakazi wa ofisi hiyo wametoa pole kwa familia, ndugu, na jamaa walioguswa na msiba huo.

Sasa, taarifa hiyo imenyofolewa kwenye kurasa za Mitandao ya Kijamii za Ofisi hiyo; ni kuwa amefufuka?

 
Kuinyofoa imenisikitisha.. Hii inamanisha kifo chake sio cha kawaida
 
Huenda marehemu kifo chake hakikua chake..
Naomba niishie hapo
 
Alishindwa/alikuwa kikwazo kuua mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…