SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Zamani mashirika yalikuwa na timu za michezo karibu yote.
Ndiyo maana tulikuwa na timu kali za Pamba ya Mwanza, Reli ya Morogoro, Tumbaku ya Morogoro, RTC Kagera, RTC Kigoma, CDA Dodoma, Ndovu Arusha, Sigara, Bima, Kilitex Arusha, Urafiki Jazz, Bora Netball, Aluminium Africa Boxing team, Uhamiaji nk.
Hata hivyo baada ya ukaguzi wa hesabu za serikali ikaonekana wapigaji walitumia mwamvuli wa michezo na burudani kupiga hela za mashirika na taasisi za serikali.
Mawazo chanya kama mwamba mmoja wa kuitwa Infantry SoldierSwali ni kwanini wawe na timu za mpira?
Kwanini sio michezo mingine ambayo bado inachechemea?
Kila taasisi unataka iwe na timu? Mapenzi yako ya mpira yanafanya usione zaidi ya mpira.
Unatolea mfano ZA na UG, upo serious kweli mkuu? Soka la hizo nchi limefika wapi kwa mfano? Wachezaji wao wakubwa wanaota kuja kucheza bongo.
Hizo taasisi zijikite kulipa watu mafao kwa wakati na kutoa huduma bora. Sio lazima kila mtu aingine michezoni. Labda wajenge viwanda kama alivyoshauri mwendazake vitaajiri watu wengi zaidi na kukuza uchumi.