Kwanini Taifa la Marekani limebarikiwa sana kiuchumi na kiteknolojia? Sababu hii hapa

Kujitoa kwa ajili ya wengine – Wakristo wa Marekani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kibinadamu kwa mataifa mengine, wakihamasishwa na mafundisho ya Yesu kuhusu upendo na huruma kwa jirani yako.
 
Kanuni ya "One Nation Under God" – Maneno haya yaliyopo kwenye Kiapo cha Uaminifu (Pledge of Allegiance) yanaonyesha jinsi Marekani inavyotambua mamlaka ya Mungu juu ya taifa hilo, jambo linalosisitiza maadili ya Kikristo katika jamii.
 
MTOA MADA ACHA UONGO NA HUJUI PRINCIPLE ZA KIUCHUMI.dini ni adui wa maendeleo duniani labda uitumie kujinufaisha kihuni kama wakina mwamposa.marekani alitoboa sana kiuchumi alipojiweka pembeni kwenye vita ya kwanza ya dunia akiwa anauza silaha huku mataifa mengine ya ulaya yakiangamia kiuchumi, baada ya vita yeye ndio akawa msaada mkubwa kiuchumi duniani
 
Athari chanya za maadili ya Kikristo kwa Jamii ya Marekani – Uwepo wa maadili ya Kikristo nchini Marekani umechangia kupunguza viwango vya uhalifu, kujenga jamii zenye mshikamano, na kusaidia ustawi wa familia, jambo linaloleta utulivu wa kijamii na maendeleo endelevu.
 
Marekani - Kituo cha Uchapishaji wa Biblia – Marekani ni nchi mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa Biblia duniani; inachapisha na kusambaza Maandiko Matakatifu kwa mamilioni ya watu katika lugha mbalimbali. Mafundisho yaliyomo katika Biblia yamewafanya watu wengi kuacha wizi, ufisadi, udanganyifu kazini, na matendo mengine maovu. Hali hii imechangia maendeleo ya kiuchumi ya Taifa hilo.
 
Ushirikiano imara kati ya Serikali na Taasisi za Kikristo – Serikali ya Marekani inatambua jinsi makanisa na mashirika ya Kikristo yanavyotoa mchango mkubwa katika jamii kwa kusaidia wasiojiweza, kutoa elimu, na kutoa huduma za afya. Hali hii inadumisha ustawi wa nchi hiyo.
 

Kwenye maisha ya kawaida, waweza tajirika kwa dhulma, halafu baadaye unatoa sadaka kwenye nyumba za ibada, huku ukisifiwa kuwa umebarikiwa. Inasikitisha sana.

Mifumo ya ya kiuchumi ya kibeberu, iliyojaa dhulma ndio inaitajirisha USA. Hakuna mambo ya baraka hapo.
 
Jumapili ni siku ya Ibada na mapumziko – Utamaduni wa Marekani unaheshimu siku ya Jumapili kama siku ya ibada na mapumziko, jambo linaloonyesha mizizi ya Kikristo katika taifa hilo.
 
Marekani ni Kituo cha Matamasha ya Injili – Marekani ni Taifa lenye wasanii wengi wa muziki wa Injili, ambao kupitia nyimbo zao, wamehamasisha mamilioni ya watu duniani kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Maisha yasiyo na ufisadi yanachangia kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Taifa hilo.
 
Vyombo vikubwa vya Habari vinavyosaidia kuenea kwa Ukristo Marekani – Mbali na redio na televisheni za Kikristo, kuna magazeti, tovuti, na majukwaa ya kidijitali yanayosambaza mafundisho ya Kikristo kwa mamilioni ya watu duniani kote. Vyombo hivi vinachangia sana kuleta ustawi wa kijamii katika Taifa hilo.
 
Marekani ni nchi inayopeleka misaada kwa mataifa yanayoteseka – Kupitia mashirika kama Red Cross, Samaritan’s Purse na World Vision, wamarekani wengi wanaongozwa na maadili ya Kikristo katika kusaidia watu wenye shida.
 
Na China ambayo inakwenda kuipita Marekani soon imebarikiwa kwa sababu ya Ukristo au Ubudha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…