Kwanini taifa la Nigeria limetawala sekta nyingi sana na kuwa na masupa star Wengi Sana na mabilionea?

nchi zote zenye population kubwa ni matajiri na wana kila aina ya kipaji....MF USA, China,India, Russia etc..Nigeria kwa population yake..jumlisha E.Africa na southern Africa yote ndo upate idadi ya wanaijeria
Kwahiyo idadi ya raia wa Rwanda ni sawa na China maana population ya Rwanda ni ndogo kulinganisha na Tanzania lakini kimaendeleo wapo mbali.. Muachage kula wali na sembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nigerians wapo karibia kila nchi katika hii Dunia.

Upande wa Intellectual pia wako njema sana, greatest Mathematicians wanao wakutosha..

Kuna mdau ameongelea suala la kutoathirika na Umagharibi, mpaka kesho hawajapoteza lafudhi yao.. Wengi wao akiongea maneno mawili unajua huyu mnigeria, akina sisi wengine mtu akienda UK au US ataStruggle kuongea kama Britons au Americans.. Kitu ambacho kinatupotezea identity yetu.

Halafu Kuna suala na majina, jamaa wanajua kuenzi majina yao ya asili, hawaoni hatari kuwa na jina refu kama 30cm ruler,

Kama idadi ya watu inawafanya kuwa hivi walivyo, inabidi tumuunge mkono namba 1, tufyatue watoto mazee..
 
Aisee ! Nigeria wao Wana mavazi yao yanaitwa 'mavazi ya ki Nigeria '
 
Mkuu umesahau na Uchawi... Wachawi wa Nigeria ni hatari, wanaongoza afrika nzima... Hata sumbawanga hapo wanachemsha

Makanisa (Mbeya haigusi moto wa Nigeria), Mapastor (TB Joshua and alike, wetu Gwaji Boy Hahahaaah), na Waimbaji wa nyimbo za Injili (Mercy Chinwo, balaa lake hata kina Shusho wawe 100 hawaoni ndani)

NB: Mifano ni ya kitz tu ili tuwaelewe vizuri hawa jamaa ila kama wapo nchi nyingine wanaowazidi naruhusiwa kukosolewa
 
Kwa wale mnaokimbilia uchawi nadhani ni uvivu wa kufanya utafiti. Katika bara la Africa nadhani Wanigeria wanaongoza kwa exposure, kwa wale waliobahatika kupita Ulaya au USA wanajua hilo. Hivyo kinachowasaidia zaidi ni exposure na sio uchawi kama watu wanavyofikiria.
Kingine kikubwa walichonacho ni DIASPORA, hawa ndio wateja wakubwa wa kazi zao epecially za kidigitally, kwa diaspora kulipa $1 kustream nyimbo 1 sio big deal au kununua movie kwa $5 au $10 pia sio issue, hivyo ukiwa na diaspora kama 1 million hilo ni soko kubwa sana. Mengine ni matunda ya kazi nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakuwaga na kaukabila kisiri siri ,mbona pia mna IQ ndogo hatusemi ,msukuma mwenye akili ni magufuli tuu
 
Unakuwaga na kaukabila kisiri siri ,mbona pia mna IQ ndogo hatusemi ,msukuma mwenye akili ni magufuli tuu
Kuhusu IQ ya JPM, nakubali kwasababu jamaa amefanya Ph.D ya kemia kwa miaka 3 ambapo hilo linawezekana kwa full time tuu lakini yeye ameifanya kwa part time miaka hiyo hiyo mitatu huku akiwa mbunge, na Waziri na bila kuchukua likizo. Yaani amekuwa enrolled fulltime course ya course wark and dissertation, huku akiwa Waziri fulltime na Mbunge fulltime.

Ingefanywa sensa ya makabila ya Ph.D holders, you'll be surprised!.
P
 
kweli mnaijeria hata azaliwe Los Angeles utakuta anaitwa Adegeyo Babatunde Okonukwo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hilo alipigwa tafu sana tu.
 
1.lugha ya kiingereza ni basic, sio anasa
2.population kubwa sana 200m+
3.vyuo vingi sana
4.makabilq zaidi ya 230 na culture zao wametunza

Tanzania na Nigeria Zina kubwa almost sawa Tanzania ikiwa juu kidogo

Tuko 50m, wako 209m

Ebu imagine rafiki.....ni survival la kufa mtu

Wanaenda nje ya nchi kutafuta maisha


Kwa wingi huo Bado wamekuwa unrest kwa sababu za Vita, uasi, na upinzani mkali......hizo kashikashi za ki nchi zinawanoa zaidi kupambana kiuchumi na viongozi wao kutobweteka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…