Kwanini taifa la Nigeria limetawala sekta nyingi sana na kuwa na masupa star Wengi Sana na mabilionea?

Kwanini taifa la Nigeria limetawala sekta nyingi sana na kuwa na masupa star Wengi Sana na mabilionea?

nchi zote zenye population kubwa ni matajiri na wana kila aina ya kipaji....MF USA, China,India, Russia etc..Nigeria kwa population yake..jumlisha E.Africa na southern Africa yote ndo upate idadi ya wanaijeria
Kwahiyo idadi ya raia wa Rwanda ni sawa na China maana population ya Rwanda ni ndogo kulinganisha na Tanzania lakini kimaendeleo wapo mbali.. Muachage kula wali na sembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nigerians wapo karibia kila nchi katika hii Dunia.

Upande wa Intellectual pia wako njema sana, greatest Mathematicians wanao wakutosha..

Kuna mdau ameongelea suala la kutoathirika na Umagharibi, mpaka kesho hawajapoteza lafudhi yao.. Wengi wao akiongea maneno mawili unajua huyu mnigeria, akina sisi wengine mtu akienda UK au US ataStruggle kuongea kama Britons au Americans.. Kitu ambacho kinatupotezea identity yetu.

Halafu Kuna suala na majina, jamaa wanajua kuenzi majina yao ya asili, hawaoni hatari kuwa na jina refu kama 30cm ruler,

Kama idadi ya watu inawafanya kuwa hivi walivyo, inabidi tumuunge mkono namba 1, tufyatue watoto mazee..
 
Jicho Langu, Nijeria Ni Nchi Pekee Africa Inayotukuza Utamaduni Wao Kwa Kulinda Mila Na Desturi Zao....
Wanaamini Katk Wao Ndo Maana Hawajaathiriwa Sana Na Tamaduni Za Kimagharibi Tofaut Na Nchi Zngne Baada Yakuja Umagharibi Tumezificha Mila Zetu Na Kuhisi Ni Mambo Yakizamani....
Mfano Sisi Wabongo Hatuna Uhalisia Wowote Katka Kila Tulifanyalo Yaani Kila Kitu Ni Tunakopi Kwa Wazungu, Tujifunze Kwa Nijeria Maybe Twaweza Toboa
Aisee ! Nigeria wao Wana mavazi yao yanaitwa 'mavazi ya ki Nigeria '
 
Mkuu umesahau na Uchawi... Wachawi wa Nigeria ni hatari, wanaongoza afrika nzima... Hata sumbawanga hapo wanachemsha

Makanisa (Mbeya haigusi moto wa Nigeria), Mapastor (TB Joshua and alike, wetu Gwaji Boy Hahahaaah), na Waimbaji wa nyimbo za Injili (Mercy Chinwo, balaa lake hata kina Shusho wawe 100 hawaoni ndani)

NB: Mifano ni ya kitz tu ili tuwaelewe vizuri hawa jamaa ila kama wapo nchi nyingine wanaowazidi naruhusiwa kukosolewa
 
Kwa wale mnaokimbilia uchawi nadhani ni uvivu wa kufanya utafiti. Katika bara la Africa nadhani Wanigeria wanaongoza kwa exposure, kwa wale waliobahatika kupita Ulaya au USA wanajua hilo. Hivyo kinachowasaidia zaidi ni exposure na sio uchawi kama watu wanavyofikiria.
Kingine kikubwa walichonacho ni DIASPORA, hawa ndio wateja wakubwa wa kazi zao epecially za kidigitally, kwa diaspora kulipa $1 kustream nyimbo 1 sio big deal au kununua movie kwa $5 au $10 pia sio issue, hivyo ukiwa na diaspora kama 1 million hilo ni soko kubwa sana. Mengine ni matunda ya kazi nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nigeria ina dorminate kutokana na idadi ya watu. Kwa mujibu wa sensa yangu ya kwanza ni sensa ya mwaka 1978 sisi Tanzania tukiwa milioni 19, Nigeria walikuwa milioni 150!. Hivyo success kwenye kila kitu inatokana na idadi ya watu. Wachina wako bilioni 1.5 ndio wanatawala dunia.

Hata kwa Tanzania kati ya watu milioni 50, Wasukuma ni 10 million na ndilo kabila linaloongoza kwa fertility rate, procreation rate, na birth rate hivyo 2099 Wasukuma tutakuwa milioni 50 Watanzania tukiwa milioni 150 kama Nigeria ile.

P
Unakuwaga na kaukabila kisiri siri ,mbona pia mna IQ ndogo hatusemi ,msukuma mwenye akili ni magufuli tuu
 
Unakuwaga na kaukabila kisiri siri ,mbona pia mna IQ ndogo hatusemi ,msukuma mwenye akili ni magufuli tuu
Kuhusu IQ ya JPM, nakubali kwasababu jamaa amefanya Ph.D ya kemia kwa miaka 3 ambapo hilo linawezekana kwa full time tuu lakini yeye ameifanya kwa part time miaka hiyo hiyo mitatu huku akiwa mbunge, na Waziri na bila kuchukua likizo. Yaani amekuwa enrolled fulltime course ya course wark and dissertation, huku akiwa Waziri fulltime na Mbunge fulltime.

Ingefanywa sensa ya makabila ya Ph.D holders, you'll be surprised!.
P
 
UFC
jat7jfbwvii31.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jicho Langu, Nijeria Ni Nchi Pekee Africa Inayotukuza Utamaduni Wao Kwa Kulinda Mila Na Desturi Zao....
Wanaamini Katk Wao Ndo Maana Hawajaathiriwa Sana Na Tamaduni Za Kimagharibi Tofaut Na Nchi Zngne Baada Yakuja Umagharibi Tumezificha Mila Zetu Na Kuhisi Ni Mambo Yakizamani....
Mfano Sisi Wabongo Hatuna Uhalisia Wowote Katka Kila Tulifanyalo Yaani Kila Kitu Ni Tunakopi Kwa Wazungu, Tujifunze Kwa Nijeria Maybe Twaweza Toboa
kweli mnaijeria hata azaliwe Los Angeles utakuta anaitwa Adegeyo Babatunde Okonukwo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu IQ ya JPM, nakubali kwasababu jamaa amefanya Ph.D ya kemia kwa miaka 3 ambapo hilo linawezekana kwa full time tuu lakini yeye ameifanya kwa part time miaka hiyo hiyo mitatu huku akiwa mbunge, na Waziri na bila kuchukua likizo. Yaani amekuwa enrolled fulltime course ya course wark and dissertation, huku akiwa Waziri fulltime na Mbunge fulltime.

Ingefanywa sensa ya makabila ya Ph.D holders, you'll be surprised!.
P
Kwa hilo alipigwa tafu sana tu.
 
Wana bodi, kwenye kufanya utafiti wangu mkubwa nimegundua na kuona kwamba taifa la Nigeria limedominate Karibu mambo mengi sana mfano kwenye muziki Muziki na Wana muziki wa Nigeria ni maarufu sana Africa na duniani kwa ujumla mfano Wizkid, patoranking, chidinma, yemi alade, femi kuti, davido, Mr favour, falz, tiwa savage, don Jazzy, p square, kipengele cha pili ambacho Nigeria wame dominate ni Kwenye fasihi na sanaa itakuwa movies za Nigeria zinatamba Africa na duniani kote kutokana na waigizaji mahiri na wenye passion na moyo na kazi yao mfano Hawa vijana Kama kina Aki na ukwa etc, kwenye uwanda wa Fasihi kwa Hapa Africa Nigeria imebeba wana fasihi wakubwa na mahiri mfano Huyu Wole Soyinka ambaye ni Mshindi wa tuzo ya amani ya 'Nobel Prize ' kwenye fasihi mwaka 1986, Mwingine ni huyu Chinua Achebe Wengi wetu tumemsoma kwenye 'Things Fall apart ' ni mwana fasihi aliyetukuka na kuheshimika
hapa barani Africa,

Kwenye kipengele cha michezo hususan mpira Nigeria wenyewe mnaona 'super eagles ' wakiingia Mara kadhaa kwenye kombe la dunia,
Kipengele kingine ni mabilionea Nigeria kuna mataycoon maarufu sana mfano tajiri Aliko dangote, Mike Adenuga, Alakija

Kipengele cha idadi ya watu Nigeria wanaongoza hapa Africa wapo milioni 200+
Kipengele kingine cha Uchumi nigeria wanawongoza hapa Africa
Kipengele kingine japo sio cha muhimu ni kwamba makabila ya Nigeria ni makubwa sana yaani yana idadi kubwa Sana ya watu mfano Wahausa, Yoruba etc

Hebu tujadili why Nigeria hawa wame dominate mambo mengi sana kiasi cha kwamba kuonekana Hawa wanaigeria kuonekana wao Kama hawapo Africa vile wao ni level ya mataifa makubwa duniani!

Nb Nigeria ni moja ya nchi ambazo Hapa Africa wamepinduana Sana /marais wamepinduliwa sana!
1.lugha ya kiingereza ni basic, sio anasa
2.population kubwa sana 200m+
3.vyuo vingi sana
4.makabilq zaidi ya 230 na culture zao wametunza

Tanzania na Nigeria Zina kubwa almost sawa Tanzania ikiwa juu kidogo

Tuko 50m, wako 209m

Ebu imagine rafiki.....ni survival la kufa mtu

Wanaenda nje ya nchi kutafuta maisha


Kwa wingi huo Bado wamekuwa unrest kwa sababu za Vita, uasi, na upinzani mkali......hizo kashikashi za ki nchi zinawanoa zaidi kupambana kiuchumi na viongozi wao kutobweteka
 
Back
Top Bottom