Kwanini Talimba Abbas hahojiwi kutokana na Gorofa lililoporomoka na kuua Kariakoo?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Mbunge wa jimbo la kinondoni kupitia CCM Mheshimiwa Talimba Abbas, alitakiwa ahojiwe japo Kidogo asaidie Polisi wajue sehemu ya kuanzia kutokana na kuporomoka kwa Gorofa la kariakoo lililoua Watu 29

Tofauti na kuwa mwanasiasa, Abbas ni mfanyabiashara pia zikiwemo za Michezo ya kubahatisha, pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (SportPesa)

Nina imani kama Serikali ingemhoji angeonesha njia. Angesema nini kilitokea.

Wasiwasi wangu ni kama haki inaweza kutendekea kwa sabababu Abbas ndo Mdhamini Mkuu wa Kampeni za CCM.
 
Qur'an

1. Surah An-Nisa (4:135): "Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimama kwa haki, kuwa mashahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili na jamaa zenu. Kama akiwa tajiri au maskini, Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Basi msifuate matamanio ili mwelekee upande. Na mkiupotosha ushahidi au mkakataa kuutoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda."

Aya hii inasisitiza uadilifu bila kujali uhusiano wa kifamilia au hali ya mtu mwingine.
 
Kwani Abbas ndiye mwenye ghorofa? Unataka kusema nini hapa?
 
Labda kama ungekuwa na udhibitisho kuwa yeye ndio mmiliki wa hilo jengo,tofauti na hapo umeandika kitu ambacho hakiingii akilini kabisa.
 
mambo ya diniya mini?
 
Hii inahusiana nini na Tarimba?
 
Imeshaundwa tume, kila mwenye maelezo yanayohitajika atahojiwa bila shaka. Tuipe muda hii tume, ikija majibu mepesi ndiyo turuke nao.

Ova
 
Ghorofa ni la mchaga kwa ninavyofahamu, liliuzwa miezi miwili kabla ya huo ukarabati kuanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…