Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Posts
1,805
Reaction score
1,876
1: Nigeria kulikuwa na Wole Soyinka, Chinua Achebe.
2: Kenya kulikuwa na mtu kama Ngugi wa Thiongo.
3: Uganda kulikuwa na Okot P'Bitek.

Wote hawa waliitwa African writers na vitabu vyao vilisomwa kwenye "english literature" katika nchi nyingi.

Ukiangalia list yote ya "African writers" huoni na kujivunia mtanzania hata mmoja. Tujiulize kwa sababu za ukweli, kwa nini Tanzania hatukupata wala mmoja kwenye hao "African writers"?
 
Msingi wa lugha ya kiingeleza hatukuwa nao.

Ukiziangalia hizo nchi zote ulizozitaja utaona kuwa zilitawaliwa na Mwingeleza.

Siye kijerumani kabla yakuota mizizi akaja mwingereza.
Naye toka 1920s akatupa Uhuru 1961.

Wakati huko Kenya na Uingeleza mkoloni alikaa tangu 1880s mpaka 1960s.

Msingi wetu ulikuwa hafifu.

Naye Nyerere akaupiga pigo la mwisho kwa kukifanya Kiswahili lugha rasmi ya taifa huku akikipa kiingereza nafasi ya pili.
 
Aina ya WaTz ni waswahili kwa tabia na matendo!! Na mtu kuwa mswahili kwa tabia ni kasoro. Rais wa awamu ya kwanza angalau alijitahidi, Lakini wa sasa na wale wengine mhhh.
 
1: Nigeria kulikuwa na Wole Soyinka, Chinua Achebe.
2: Kenya kulikuwa na mtu kama Ngugi wa Thiongo.
3: Uganda kulikuwa na Okot P'Bitek.

Wote hawa waliitwa African writers na vitabu vyao vilisomwa kwenye "english literature" katika nchi nyingi.

Ukiangalia list yote ya "African writers" huoni na kujivunia mtanzania hata mmoja. Tujiulize kwa sababu za ukweli, kwa nini Tanzania hatukupata wala mmoja kwenye hao "African writers"?
Peter Palangyo aliandika "Dying in the Sun" kwenye African Writers Series. So Tanzania did not miss out.
 
Na ukweli mchungu maarifa mengi yamewekwa kwa Lugha ya Kiingereza, hilo ndio tatizo ndio maana idadi ya wasomaji vitabu ni ndogo sana hapa bongo.
 
Ni shida tujitahidi labda tuwapachike akina Shaban Robert na mashairi yake, tupeane mawazo tuamke na tukimbie badala ya kutembea
 
New City

Wabongo tulikuwa tunanyooshwa kishezi kwenye hilo shindano.

Na kikubwa kilichokuwa kinatuangusha ni ukosefu wa General Knowledge.

We acha tu.

Unakuta hata zile obvious general knowledge za hapa Bongo zilikuwa zinawapiga chenga.
 
1: Nigeria kulikuwa na Wole Soyinka, Chinua Achebe.
2: Kenya kulikuwa na mtu kama Ngugi wa Thiongo.
3: Uganda kulikuwa na Okot P'Bitek.

Wote hawa waliitwa African writers na vitabu vyao vilisomwa kwenye "english literature" katika nchi nyingi.

Ukiangalia list yote ya "African writers" huoni na kujivunia mtanzania hata mmoja. Tujiulize kwa sababu za ukweli, kwa nini Tanzania hatukupata wala mmoja kwenye hao "African writers"?
Tatizo lilianzia kwenye chama kilichoitwa TANU ikazaa CCM hawa makanjanja walioifanya Tanzania shamba la bibi kwa kutuweka tuwe wajinga wa kudumu
 
Peter Palangyo aliandika "Dying in the Sun" kwenye African Writers Series. So Tanzania did not miss out.
Shukran ... Nilitaka nimpe jibu hili. Watanzania tunajishusha mno, mpaka tunatia huruma.
Bado thread hii itaendelea kwa comments za kujiponda na kujibeza, na wanetu watakua hivyohivyo watu wa kujibeza.
Nashukuru mimi sijakuzwa hivyo.
 
Ndio utambue hatuna wasomi bali wahitimu.
Zile kelele sijui Mimi shule na vyuo changu kipanga ww chako cha kata ni kujifariji.
Unakumbuka ile zain African challenge, watanzania walikuwa wanafanywa nini..!??

Wadesaji.
 
Back
Top Bottom