Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

Peter Palangyo aliandika "Dying in the Sun" kwenye African Writers Series.
Pia yumo Ishmael MBISE. Huyu kwa sasa ni Profesa wa Literature, Chuo Kikuu Tumaini Makumira. Aliandika: Blood on Our Land. Waandishi wa Kazi za Fasihi wako WENGI tu. Pamoja na Shaaban Robert, wapo pia: Kezilahabi, Semzaba, Aldni Mutembei, Mulokozi, Angoro Anduru, Kaigarula, Penina Muhando-Mlama, Ebrahim Hussein, Richard Mabala, Profesa Mbogo, Julius Nyerere, Gabriel Ruhumbika, Amandina Lihamba, Balisidya, Ndulute, nk. Wengi wa hawa waliandika kazi zao za Fasihi kwa lugha ya Kiswahili.
Ieleweke pia kuwa Africa Writers' Series, ni kampuni la uchapishaji wa kazi za Fasihi za Kiafrika (zilizoandikwa na Waafrika) kuhusu Afrika. Lugha ya uchapishaji ni Kiingereza. Kwa maana hii, kukosa kuchapisha kazi ya Fasihi katika AWS, haimaanishi Watanzania Hawajabobea katika kazi za Fasihi. Kwa waliosoma Fasihi shule za sekondari na vyuo, wamesoma kazi nyingi tu za fasihi zilizotayarishwa na Watanzania.
 
Mbona wapo mkuu. Kwenye fasihi ya Kiswahili kuna waandishi wengi nguli kama Euphrase Kezilahabi, Shafi Adam Shafi, Mohamed Seif Khatib na wengineo wengi...
 
New City

Wabongo tulikuwa tunanyooshwa kishezi kwenye hilo shindano.

Na kikubwa kilichokuwa kinatuangusha ni ukosefu wa General Knowledge.

We acha tu.

Unakuta hata zile obvious general knowledge za hapa Bongo zilikuwa zinawapiga chenga.

Ndio mkuu nakumbuka vema, tena hao ndio walikuwa vipanga wa vipanga wetu.
Sasa hali hiyo hata uandike kitabu nani atasoma wakati hata ABC za nyumbani pako huzifahamu.
 
Peter Palangyo aliandika "Dying in the Sun" kwenye African Writers Series. So Tanzania did not miss out.

Gambanjeli,

Hicho kitabu unachosema ni kimoja tu na binafsi ndiyo kwanza nakisikia. Si kwa uvivu wangu bali nimetaja vitabu ambavyo tumefanyia mtihani kwenye sylabus ya Form IV ya Tanzania.

Sasa kama Tanzania yenyewe haikukiweka hicho kitabu kwenye syslabus, basi ama nchi ilijishusha au kitabu chenyewe nacho hakikuwa na mvuto. Na kama nchi ilikishusha thamani usitarajie mimi niibuke kama mwehu kukisifia wakati hata nchi yenyewe haikukithamini, tena enzi za Nyerere.

Shukran ... Nilitaka nimpe jibu hili. Watanzania tunajishusha mno, mpaka tunatia huruma.
Bado thread hii itaendelea kwa comments za kujiponda na kujibeza, na wanetu watakua hivyohivyo watu wa kujibeza.
Nashukuru mimi sijakuzwa hivyo.

Kobello, uko duniani mahala pa mashindano (competition). Usiwe mvivu kwa kutarajia mimi nitanunua bidhaa yako mbovu au kitabu chako cha kisicho na mvuto eti tu kwa sababu nikifanya hivyo nitakuwa najishusha.

Kama Tanzania haiwezi ku-compete na nchi zingine duniani, basi bidhaa sintakimbilia bidhaa zake niache quality nzuri.

Tumia watu wenye profession zao wakupe best quality of service ya kila kitu chako ikiwemo vitaub.

Lakini ukiajiri marafiki zako au watu wanajipendekeza hadi kukubebea begi unapoingia ofisini wakati kichwani hakuna kitu basi tarajia kila product yako ikiwemo vitabu hakuna anayevipenda labda maskini wa kutupwa, tena naye atanunua kwa sababu hana uwezo wa kununua vya nje.

Fanyia kazi ushauri wangu.
 
Tanzania wapo waandishi wazuri na mahili ambao vitabu vyao mpaka sasa vinasomwa na ulimwengu mzima na vinapatikana kwenye vyiuo vikuu vyote duniani vyenye kozi za kiswahili hasa ngazi ya PHD Kwa tamrini na tasnifu
Mfano
1.Mwl.nyerere aliandika vitabu kama Juliusi kaizari,Mabepari wa venisi -William shakespears

2.Shaban Robert - huyu ana vitabu vingi sana vinasomwa Kwa ngazi zote kuanzia sekondari mpaka vyiuo vikuu

3.prof.E.Kezilahabi huyu amepatakuandika kitabu ambacho kiliibua mikinzano na mivatano katika jamii kutokana na maudhui yake kuilenga dini Fulani na alipata kufikishwa mahakami kujibu mashitaka !kitabu kinaitwa. Rosa mistika.

4.Mathiasi Mnyampala .huyu amepata kuweka rekodi katika utunzi wa Tenzi na Ngonjera pia na baadhi ya vitabu ameandika vinapatikana kwenye makavazi ya vyuo vyote nchini na nje

5.Prof.Harrison Mwakyembe huyu amepata kuandika kitabu kinaitwa Pepo ya mabwege .kikosafi kimeisaiwiri vyema jamii ya kitanzania kupitia wahusika wa josina na kalenga

6.Mohamedi .A. Katalambula huyu pia ameacha historia katika uandishi wa vitabu na amali zake nyingi zipo vyuo vikuu na sekondari zinatumiwa na wananzuoni
.......,...................
Vijana wengi mnapenda utamaduni wa wazungu kazi za hapa kwetu hamzithamini nakuona kama kuzisoma ni kupoteza muda wengi mnatembea na mizigo ya albam za akina diamond na kiba

Nchi yetu inakazi nyingi sana za fasihi zinapatikana bookshop karibia zote mikoani

Tujenge utamaduni wa kusoma kazi za nyumbani zipo nyingi sana

Lugha ya kiswahili sasa inafundishwa na mataifa zaidi ya 70 duniani

NB..Kitabu cha mabepari wa venisi cha mwalimu nyerere alikitafsiri kutoka Kwa mwandishi mashuhuri wa tamthilia uingereza anaitwa William Shakespears kitabu chake alikiita Merchant of Venese

William alikuwa na maana ya mfanyabiashara lakni nyerere yeye alimuona mfanyabiashara ni mnyonyaji hivyo akikiita bepari wa venisi ikumbukwe ilikuwa ni kipindi kile vita ya socialism opposed capitalism imepamba moto

Ahsante Kwa kusoma R.I.P. Julius kaizari(nyerere)
 
1: Nigeria kulikuwa na Wole Soyinka, Chinua Achebe.
2: Kenya kulikuwa na mtu kama Ngugi wa Thiongo.
3: Uganda kulikuwa na Okot P'Bitek.

Wote hawa waliitwa African writers na vitabu vyao vilisomwa kwenye "english literature" katika nchi nyingi.

Ukiangalia list yote ya "African writers" huoni na kujivunia mtanzania hata mmoja. Tujiulize kwa sababu za ukweli, kwa nini Tanzania hatukupata wala mmoja kwenye hao "African writers"?
Kiongozi wasomi wetu ni hawa akina Benson Bana et al, unatarajia waandike nini? Labda kuhalalisha wizi wa kura.
 
Kuna kina Shaban Robert, kizalahabi ,kina chande (kusadikika) na kwa sasa kuna shigongo hawa wote ni waandishi wazuri ni kazi serikali kutambua mchango wao na wananchi kuwatambua , kama serikali au wananchi hawathamini watu wao basi ni vigumu Raia wa nje kuwathamini, charity begins at home.
 
New City

Wabongo tulikuwa tunanyooshwa kishezi kwenye hilo shindano.

Na kikubwa kilichokuwa kinatuangusha ni ukosefu wa General Knowledge.

We acha tu.

Unakuta hata zile obvious general knowledge za hapa Bongo zilikuwa zinawapiga chenga.
Vyuo vya kibongo nilikuwa siangalii mimi...
 
Kujaza vitabu vya waandishi wengi au wote wa nje katika maskuli yetu ni wazi inaonyesha we are lacking
 
Tanzania wapo waandishi wazuri na mahili ambao vitabu vyao mpaka sasa vinasomwa na ulimwengu mzima na vinapatikana kwenye vyiuo vikuu vyote duniani vyenye kozi za kiswahili hasa ngazi ya PHD Kwa tamrini na tasnifu
Mfano
1.Mwl.nyerere aliandika vitabu kama Juliusi kaizari,Mabepari wa venisi

2.Shaban Robert - huyu ana vitabu vingi sana vinasomwa Kwa ngazi zote kuanzia sekondari mpaka vyiuo vikuu

3.prof.E.Kezilahabi huyu amepatakuandika kitabu ambacho kiliibua mikinzano na mivatano katika jamii kutokana na maudhui yake kuilenga dini Fulani na alipata kufikishwa mahakami kujibu mashitaka !kitabu kinaitwa. Rosa mistika.

4.Mathiasi Mnyampala .huyu amepata kuweka rekodi katika utunzi wa Tenzi na Ngonjera pia na baadhi ya vitabu ameandika vinapatikana kwenye makavai ya vyuo vyote nchini na nje

5.Prof.Harrison Mwakyembe huyu amepata kuandika kitabu kinaitwa Pepo ya mabwege .kikosafi kimeisaiwiri vyema jamii ya kitanzania kupitia wahusika wa josina na kalenga

6.Mohamedi .A. Katalambula huyu pia ameacha historia katika uandishi wa vitabu na amali zake nyingi zipo vyuo vikuu na sekondari zinatumiwa na wananzuoni
.......,...................
Vijana wengi mnapenda utamaduni wa wazungu kazi za hapa kwetu hamzithamini nakuona kama kuzisoma ni kupoteza muda wengi mnatembea na mizigo ya albam za akina diamond na kiba

Nchi yetu inakazi nyingi sana za fasihi zinapatikana bookshop karibia zote mikoani

Tujenge utamaduni wa kusoma kazi za nyumbani zipo nyingi sana

Lugha ya kiswahili sasa inafundishwa na mataifa zaidi ya 70 duniani

NB..Kitabu cha mabepari wa venisi cha mwalimu nyerere alikitafsiri kutoka Kwa mwandishi mashuhuri wa tamthilia uingereza anaitwa William Shakespears kitabu chake alikiita Merchant of Venese

William alikuwa na maana ya mfanyabiashara lakni nyerere yeye alimuona mfanyabiashara ni mnyonyaji hivyo akikiita bepari wa venisi ikumbukwe ilikuwa ni kipindi kile vita ya socialism opposed capitalism imeoamba moto

Ahsante Kwa kusoma R.I.P. Julius kaizari(nyerere)

Yaani wewe umefunga mjadala, umeelezea mule mule, siku hizi vijana wanasomea instagram, twitter , facebook,na google. Mimi nilikuwa mvuvi sana wa kusoma hizi fasihi, lakini nikiwa kidato cha nne nilikuwa mpenzi na mfuatiliaji mzuri sana wa kitabu cha Kusadikika , na mashairi ya Shaban Robert, kwa kweli nili enjoy sana licha ya kuwa mimi nilikuwa mchepuko ya sayansi, hata nilipomaliza masomo bado ilibidi nivinunue hivi vitabu na huwa nasoma kila kila mara, Tatizo kubwa linalotuangusha watanzania nikung'ang'ania western culture na kuona vya kwetu ni bure, kumbe mataifa mengine yanataka lengo lao ni kuona lugha zao zinakuwa juu siku zote ili watutawale vizuri.
 
Tanzania wapo waandishi wazuri na mahili ambao vitabu vyao mpaka sasa vinasomwa na ulimwengu mzima

Hakuna mwenye shida navyo ndiyo maana hata kwenye "Africa writers" havimo, yaani hata waafrika hawana habari navyo na hawavihitaji.
 
Yaani wewe umefunga mjadala, umeelezea mule mule, siku hizi vijana wanasomea instagram, twitter , facebook,na google. Mimi nilikuwa mvuvi sana wa kusoma hizi fasihi, lakini nikiwa kidato cha nne nilikuwa mpenzi na mfuatiliaji mzuri sana wa kitabu cha Kusadikika , na mashairi ya Shaban Robert, kwa kweli nili enjoy sana licha ya kuwa mimi nilikuwa mchepuko ya sayansi, hata nilipomaliza masomo bado ilibidi nivinunue hivi vitabu na huwa nasoma kila kila mara, Tatizo kubwa linalotuangusha watanzania nikung'ang'ania western culture na kuona vya kwetu ni bure, kumbe mataifa mengine yanataka lengo lao ni kuona lugha zao zinakuwa juu siku zote ili watutawale vizuri.
Watanzania ni wavivu wa kusoma tena sana

Siri za dunia ziko kwenye vitabu

Vitabu vya wazungu sisi havitusaidii chochote maana mazingira ya wazungu siyo mazingira yaliyotukuza sisi

Tuendelee kusoma tusome bila kuchoka tena tusome usiku na mchana tusikubali kushikiwa akili
 
1.Mwl.nyerere aliandika vitabu kama Juliusi kaizari,Mabepari wa venisi

Usipojua jambo uliza ufundishwe. Nyerere hajawahi kuandika kitabu kiitwacho "Mabepari wa Venice". Tofautisha kati ya kuandika kitabu na kutafsiri kitabu, tena hichohicho cha "Merchant of Venice" cha wazungu unaotudanganya huwahusudu.
 
Kwa nini tung'ang'anie lugha ya kienyeji?! Isiyotutambulisha kokote?! Inayotufanya kuwa ma bubu once tunapovuka mipaka ya nchi yetu!!!

Halafu wanaolazimisha kiswahili iwe lugha ya kufundishia wanapeleka watoto shule zinazofundisha kwa kiingereza!! Kwa hapa Tanzania ukijua kiingereza fasaha unapata kazi haraka sana hata kama huna elimu nzuri. Alaaniwe aliyeondoa kiingereza kuwa lugha ya kufundishia toka elimu ya awali.
 
Back
Top Bottom