Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

Kwanini Tanzania haikupata waandishi vitabu maarufu yaani "African Writers"?

1: Nigeria kulikuwa na Wole Soyinka, Chinua Achebe.
2: Kenya kulikuwa na mtu kama Ngugi wa Thiongo.
3: Uganda kulikuwa na Okot P'Bitek.

Wote hawa waliitwa African writers na vitabu vyao vilisomwa kwenye "english literature" katika nchi nyingi.

Ukiangalia list yote ya "African writers" huoni na kujivunia mtanzania hata mmoja. Tujiulize kwa sababu za ukweli, kwa nini Tanzania hatukupata wala mmoja kwenye hao "African writers"?
Hoja:
Afrika ina nchi zaidi ya 50, mbona umezitaja nchi 3 tatu, iweje uishangae Tanzania wakati hata nchi nyingine hazina African writers mfano Malawi, Angola, Chad, Afrika ya Kati, Somalia na Msumbiji.

Nahisi exposure kutokana na elimu ya mkoloni ndio ilisaidia baadhi ya nchi kuchangamka mapema. Kwa mfano, Wanaijeria walianza kupata elimu nzuri na exposure kipindi cha mkoloni nahisi kuliko nchi nyingine ya Kiafrika. Chinua Achebe aliandika novel ya Things Fall Apart mwaka 1957 wakati Tanzania tupo na mapambano ya TANU.

Uganda ndiko kulikuwa na Makelele University, hivyo exposure ilikuwepo.

Kenya setlers walikuwepo, hivyo exposure ilikuwepo.

Afrika Kusini licha ya kuishi Wazungu kwa miaka zaidi ya 600 lakini kulikuwa na sera ya ubaguzi wa rangi hivyo ilikuwa ngumu kwa Waafrika kupewa elimu nzuri.

French Colonies wao walikuwa bize kwenda Ufaransa na kucheza mpira kutokana na sera ya Assimilation policy.
 
Back
Top Bottom